Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Februari 15, 2011

FASIHI YA KIAFRIKA

Picha kwa hisani ya www.saibabamandirs.com

Fasihi ya Kiafrika inamaanisha maandiko kuhusu na kutoka Afrika. Kama George Joseph anavyodokeza katika ukurasa wa kwanza wa sura yake kuhusu Fasihi ya Afrika katika kitabu understanding Contemporary Africa, ' wakati mtizamo wa fasihi ya Ulaya kwa ujumla inahusu herufu zilizoandikwa, dhana ya Afrika inahusisha pia fasihi simulizi.


Kama George Joseph anavyoendelea kuandika, wakati maoni ya Ulaya kuhusu fasihi yalisisitiza mgawanyo wa sanaa na maudhui, mwamko wa Afrika unajumuisha:

"Fasihi" inaweza pia kuashiria matumizi ya maneno kisanaa kwa ajili ya sanaa pekee. Bila kukana jukumu muhimu la somo la sanaa katika Afrika, tunapaswa kukumbuka kwamba, tangu jadi, Waafrika huwa hawatenganishi sanaa na kufundisha. Badala ya kuandika au kuimba kwa sababu ya uzuri ulioko, Waandishi wa Afrika, kwa kufuata fasihi simulizi, hutumia uzuri kusaidia kuwasiliana ukweli na taarifa muhimu na jamii. Hakika, kitu huchukuliwa kizuri kwa sababu ya ukweli kinachoonyesha na jamii kinachosaidia kujenga.

Maandiko ya kitambo

(Misri ya Kale) ulikuwa miongoni mwa tamaduni za kale zaidi za Kiafrika zenye desturi ya kuandika, ambao baadhi ya maandishi yake yaliyotumia picha na alama kuashiria kitu au jambo huishi mpaka waleo. Kazi kama vile Kitabu cha Wafu cha Misri kawaida hutumiwa na wasomi kama rejeleo la msingi la imani ya kidini ya Misri ya kale na sherehe. Maandiko ya Kinubi, yanakubalika lakini kwa wakati huu hayasomeki. Awali yaliandikwa kwa kutumia picha na alama na hatimaye kwa kutumia alfabeti yenye miundo 23, kutafsiri kumekuwa kugumu.


Mrisho Mpoto.
Picha kwa hisani ya www.haki-hakingowi.blogspot.com

Fasihi simulizi

Fasihi simulizi inaweza kuwa katika nathari au ushairi. Mara nyingi, nathari huwa hadithi au historia na inaweza kujumuisha hekaya zenye wahusika walaghai. Wasimuliza katika Afrika wakati mwingine hutumia mbinu ya kuuliza-na-majibu kusimulia hadithi zao. Mashairi, mara nyingi huimbwa, hujumuisha: masimulizi ya visa, aya ya shughuli, aya ya kidini, mashairi ya kusifu watawala na watu wengine maarufu. Waimbaji wa sifa, husimulia hadithi zao kwa kuimba. Nyimbo za upendo, za kazi, za watoto, misemo, mithali na vitendawili pia husomwa au huimbwa.

Fasihi kabla ya Ukoloni

Mifano ya fasihi ya Kiafrika kabla ya ukoloni ni mingi. Fasihi simulizi ya Afrika ya magharibi inajumuisha visa vya Sundiata vilivyotungwa katika Mali ya kitambo, Visa vya zamani vya Dinga kutoka Dola la kitambo la Ghana. Nchini Ethiopia, iliyoandikwa awali kwa miundo ya Ge'ez ni Kebra Negast au kitabu cha wafalme. Aina moja maarufu ya ngano za kiafrika ni hadithi za "ulaghai", ambapo wanyama wadogo hutumia akili zao kushinda mapambano na wanyama wakubwa. Mifano wa wanyama laghai ni pamoja na Anansi, buibui katika ngano za Waashanti kutoka Ghana; Ijàpá, kobe katika ngano za Wayoruba kutoka Nigeria; na Sungura, ambaye hupatikana katika ngano za Afrika ya Mashariki na kati. Kazi zingine zilizoandikwa ni tele, yaani katika Afrika kaskazini, kanda ya Sahel ya Afrika magharibi na pwani ya Kiswahili. Kutoka Timbuktu peke yake, kuna wastani nakala 300,000 au zaidi zilizowekwa katika maktaba mbalimbali na mikusanyiko ya kibinafsi, hasa zilizoandikwa kwa Kiarabu, lakini baadhi yazo katika lugha za wenyeji (yaani Peul na Songhai) Nyingi ziliandikiwa katika Chuo Kikuu maarufu cha Timbuktu. Kazi hizi zinaongelea mada nyingi, ambazo ni pamoja na Unajimu, Ushairi, Sheria, Historia, Imani, Siasa na Falsafa miongoni mwa zingine. Fasihi ya Kiswahili vile vile, imehamasishwa na mafundisho ya Kiislam lakini ilikua katika mazingira ya kienyeji. Mojawapo wa vipande vya fasihi ya Kiswahili vinavyojulikana na vya kitambo sana ni Utendi wa Tambuka au "Hadithi ya Tambuka". Katika nyakati za Kiislamu, Waafrika wa Magharibi kama vile ibn Khaldun walitia fora sana katika fasihi ya Kiarabu. Afrika Kaskazini ya kitambo ilinufaisha Vyuo vikuu kama vile vya Fez na Cairo, kwa kiasi kikubwa mno cha maandiko ili kuongeza yao.

Fasihi ya Kiafrika wakati wa ukoloni

Kazi nzuri za Kiafrika zinazojulikana Ulaya kutoka kipindi cha ukoloni na kile cha biashara ya utumwa ni za masimulizi ya utumwa, kama vile The Interesting Narrative of the Life of Olaudah Equiano (1789) cha Olaudah Equiano.


Katika kipindi cha ukoloni, Waafrika walioadhiriwa na lugha za ulaya walianza kuandika katika lugha hizo. Mwakani 1911, Yusufu Efraimu Casely-Hayford (ajulikanaye pia kama Ekra-Agiman) kutoka Pwani ya Dhahabu (sasa Ghana) alichapisha ile pengine ni riwaya ya kwanza ya Kiafrika kundikwa kwa Kimwombo, Ethiopia Unbound: Studies in Race Emancipation Ingawa kazi hii iligusia hadithi na utetezi wa kisiasa, uchapishaji na kupitiwa upya na wanahabari wa Ulaya kulimaanisha wakati muhimu katika fasihi ya Kiafrika.


Katika kipindi hiki, tamthlia za Kiafrika zilianza kuibuka. Herbert Isaka Ernest Dhlomo wa Afrika ya Kusini alichapisha tamthlia ya kwanza ya Kiafrika kwa Kiingereza, [10] katika mwaka wa 1935. Mwakani 1962, Ngugi wa Thiong'o kutoka Kenya aliandika mchezo wa kuigiza wa kwanza wa Afrika ya Mashariki, The Black Hermit, hadithi iliyohadhari "ukabila" (ubaguzi kati ya makabila ya Afrika).


Fasihi ya Afrika mwishoni mwa kipindi cha ukoloni (kati ya mwisho wa Vita Vikuu vya Kwanza Vya Dunia na uhuru) iliendelea kuonyesha mandhari ya ukombozi, uhuru, na (kati ya Waafrika kwenye maeneo yaliyodhibitiwa na Ufaransa ) kutambua weusi wa Waafrika. Mmoja wa viongozi wa harakati za kutambua weusi, mshairi na hatimaye Rais wa Senegal, Sédar Léopold Senghor, alichapisha mkusanyiko wa kwanza wa mashairi ya lugha ya Kifaransa yaliyoandikwa na Waafrika mwakani 1948, Anthologie de la Nouvelle poésie nègre et malgache de langue Française (Anthology of the New Black and Malagasy Poetry in French Language), akishirikisha utangulizi kutoka kwa mwandishi wa Kifaransa, Jean-Paul Sartre.


Sio kwamba waandishi wa fasihi ya Afrika wakati huu walikuwa mbali na masuala waliyoyakabili. Wengi, kwa hakika, waliteswa kwa undani na pia kwa kuelekezwa: Akilaaniwa kwa kuyaweka kando majukumu yake ya kisanaa ili kushiriki kikamilifu katika mapambano, Christopher Okigbo aliuawa katika vita ya Biafra dhidi ya wanaharakati wa Nigeria katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1960; Mongane Wally Serote aliwekwa kizuizini chini ya sheria ya Afrika Kusini ya Terrorism Act No 83 ya 1967 kati ya 1969 na 1970, na hatimaye kutolewa bila hata kujibu mashtaka; mjini London mwaka 1970, mwananchi mwenzake Arthur Norje alijiua; Jack Mapanje wa Malawi aliwekwa kizuizini bila kesi au mashtaka kwa sababu ya matamshi aliyotoa katika baa ya chuo kikuu ; na, mwakani 1995, Ken saro-Wiwa alikufa kwa kutiwa kitanzi na serikali ya wanajeshi ya Nigeria.


Picha kwa hisani ya:
www.udadisi.blogspot.com


Fasihi ya Afrika baada ya ukoloni

Kwa ukombozi na kuongezeka kwa kusoma na kuandika kwani mataifa mengi ya Afrika yalipata uhuru wao katika miaka ya 1950 na 1960, fasihi ya Afrika imeongezeka kwa kasi kwa wingi na katika kutambuliwa, kwa kazi nyingi za Afrika kuonekana katika mitaala ya kielimu ya Ulaya na katika orodha ya "bora ya" vilivyoandikwa mwishoni mwa karne ya 20. Waandishi wa Afrika katika kipindi hiki waliandika katika lugha za Ulaya (hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno) na pia lugha za Afrika za jadi.


Ali A. Mazrui na wengine hutaja migogoro saba kama mandhari: Mfarakano kati ya Afrika iliyopita na iliyopo, kati ya Utamaduni na Usasa, kati ya wazawa na kigeni, kati ya kujijali na kujali jamii, kati Ujamaa na Ubepari, kati ya maendeleo na kujitegemea na kati Uafrika na ubinadamu. Mandhari mengine katika kipindi hiki ni pamoja na matatizo ya kijamii kama vile ufisadi, tofauti za kiuchumi kati ya nchi ambazo zimepata uhuru maajuzi, na haki na majukumu ya wanawake. Waandishi wa kike sasa wamewakilishwa vyema katika fasihi ya Afrika iliyochapishwa kuliko walivyokuwa kabla ya uhuru.


Mwakani 1986, Wole Soyinka alikuwa mwandishi wa Afrika wa kwanza baada ya uhuru kushinda Tuzo la Nobel katika fasihi. Camus Albertmzaliwa wa Algeria alipokea tuzo hilo katika mwaka 1957.

Tuzo la Noma

Tuzo la Noma, lilianza mwaka wa 1980, hupatianwa kwa kazi bora ya mwaka katika fasihi ya Afrika.


Jumamosi, Februari 12, 2011

WILLIAM A, IZUNGO


NI MIONGONI MWA MARAFIKI NILIONAO, NAJIVUNIA KUFAHAMIANA NAYE, NI MWEZI HUU HUU ANACHUKUA JIKO (kuoa) JAPO MASKANI YAKE NI NCHINI CANADA.



NI MWANA HARAKATI NGULI KATIKA KUHAKIKISHA KONDOO WA BWANA WANABAKI ZIZINI, ELIMU YAKE YA UCHUNGAJI AMEIPATIA KATI CHUO KIKUU CHA WAADVENTISTA WASABATO KILICHOPO ARUSHA (University of Arusha)



LEO KWA SABABU YA UPEKEE NA UNYETI WA SIKU SIO VIBAYA TUKIBARIKIWA NA MIONGONI MWA NYIMBO ALIZOZIIMBA NA KUZIREKODI, MPAKA SASA ANA ALBUM MBILI ZILIZO SOKONI NA HII NI MOJA YA KAZI YAKE.



NAKUTAKIA SABATO NJEMA...Enjoy Blessings.



Jumatano, Februari 09, 2011

Hivi Naelewa Kwa Kiasi Gani.

Picha na:
www.
fadhymtanga.blogspot.com

Hii ni hoja nzito mno kuliko unavyoweza kuelewa, hasa kwa kuwa kiasi cha kuelewa si suala la mtu binafsi.

Je, uelewa juu yako binafsi ni wa kiasi gani?

Na je uelewa juu ya nchi yako ni mkubwa kuliko uelewa juu ya nchi jirani?

Picha kwa hisani ya:
http://simon-kitururu.blogspot.com


Tatizo si katika hilo tu, bali je elimu yetu imekuwezesha kuelewa mambo kwa kiasi gani?

Mambo yatakayo kuwezesha kutatua matatizo yako binafsi?

Wakati tukiendelea kutafakari tafakari na ujumbe katika wimbo huu:

MAISHA YANGU NI MLIMA.



Jumatatu, Februari 07, 2011

Jumamosi, Februari 05, 2011

02. ‘Waliopewa Kitabu’!

Assalamu’ alaikum!

Kurani Tukufu huelekeza kidole chake kwenye kundi lile liitwalo “Waliopewa Kitabu”. Msomaji anaombwa asome Sura 3:113-115. Aali Imran.

003:113 “Wao (Waliopewa Kitabu) si wote sawa. Katika (hao) Waliopewa Kitabu wamo watu waliotengenea - wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu (yaani wamesilimu).”

003:114 “Wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanayaendea mbio mambo mema. Na hao ndio miongoni mwa hao watendao mema (kweli kweli).”

003:115 “Na heri yo yote watakayoifanya hawatakanushiwa (thawabu zake). Na Mwenyezi Mungu anawajua wanaomcha (wakajiepusha na makatazo yake na wakafanya maamrisho yake).”

Watu hao wanajulikana kama ‘Wakristo’. Hao wanaitwa ‘Waliopewa Kitabu’ (Maandiko ya Biblia). Lakini miongoni mwao limo kundi la pekee. Kurani Tukufu yasema kwamba ipo tofauti kati ya hao ‘Wakristo’ na ya kwamba ‘si wote sawa.’
Je, kundi hilo la pekee ni akina nani ambao Nabii Muhammad (jina lake na liheshimiwe) alivuta mawazo ya watu kuelekea kwao kwa namna ya ajabu kama hiyo, ya kuwa wao ni ‘miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli’!
Hebu zingatia tabia zinazolitambulisha kundi hili la pekee kutoka katika Sura 3:113-115
1. si (Wakristo) wote sawa
2. katika (hao) waliopewa Kitabu wamo watu waliotengenea
3. wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu
4. wanasujudu
5. wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho
6. wanaamrisha mema [wanafundisha kwa mamlaka yaliyo ya haki]
7. wanakataza maovu
8. wanayaendea mbio mambo mema [wanajitahidi kufanya yale yenye sifa njema]
9. hao ndio miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli
10. na heri yo yote watakayoifanya hawatakanushiwa. [Mwenyezi Mungu anawajua]

Kurani Tukufu yasema hivi kuhusu kundi hilo la pekee, kwamba hao “ndio miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli”. Iwapo hao ni miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli, basi yale wayasadikiyo hayana budi kuwa ndiyo kweli yenyewe. Kama Mwenyezi Mungu anawaita kuwa wamo miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli, basi, sisi hatuthubutu kabisa kuwakosoa. Lakini je! si afadhali sisi pia tungeweza kujifunza kitu kwao? Twaona ya kwamba watu hao wa pekee wanakishikilia kile ‘Kitabu’ (Maandiko ya Biblia) ambacho Nabii Muhammad kwa makusudi mazima alituelekeza sisi kwenye [Kitabu] hicho katika Kurani Tukufu (Al Maidah) Sura 5:46 … “Na tukawafundisha (Mitume hiyo) Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uongozi na nuru na isadikishayo yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uongozi na mauidha kwa wamchao (Mwenyezi Mungu).”
Watu hao wanasadiki kwamba ni jukumu lao kujitoa kabisa kwa Mwenyezi Mungu pasipo kuzuia kitu, kuwa na utii kwake usio na swali. Watu hao wana maadili ya kiwango cha juu, ambayo yamejengwa juu ya Maandiko ya Biblia. Wanamheshimu Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mkuu kuliko wote, tena hawana mshirika ye yote (kama vile Maryamu au wale wengine waitwao watakatifu wanaoabudiwa) ambaye wanamfungamanisha na huyo Mungu kama Wakristo wengi sana wafanyavyo. Katika Injili maneno haya hunenwa: Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema.” … na katika Marko (Isa al-Masih) Kristo Mwenyewe alisema… “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja”. Watu hao hawazisujudu sanamu katika ibada yao kama wafanyavyo Wakristo wengi sana. Wanasadiki kwamba kuabudu sanamu au mifano iwayo yote kumekatazwa kabisa na Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika Taurati, Kutoka 20:4-5 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia”. Watu hao wanajua kwamba kuabudu hiyo mifano na sanamu kumekatazwa kabisa katika Maandiko ya Biblia.
Yaendelea [Kurani Tukufu] kusema kwamba watu hao katika ibada yao kwa Mwenyezi Mungu ‘wanasujudu’, yaani, wanapiga magoti mbele zake Mwenyezi Mungu kama Daudi alivyoandika katika Zaburi (Taurati), Zaburi 95:6 “Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.”

Katika Sura 3:114 inatuambia sisi kwamba ‘wanakataza maovu’. ‘Hao’ miongoni mwa “wao Waliopewa Kitabu” wanakataza kula vyakula najisi (haramu) kama ‘Nyama ya nguruwe’. (Taurati) Mambo ya Walawi 11:7 “Na nguruwe, … yeye ni najisi kwenu.” Wanakataza matumizi ya vileo, tumbako, na vitu vingine vinavyodhuru (haramu) afya ya mwili ambavyo vinauangamiza. Wanaziheshimu Amri Kumi za Mwenyezi Mungu kama zilivyoandikwa katika (Taurati) Kutoka 20. Watu hao wanasadiki kwamba tunaishi katika “Siku za Mwisho” za historia ya dunia hii…

Waadventista Wasabato
Je! kundi hilo la pekee la “Waliopewa Kitabu” ambao juu yao Kurani Tukufu inaongea sifa nyingi sana ni akina nani? Lipo kundi la watu miongoni mwa “Waliopewa Kitabu” lijulikanalo kama: “Waadventista Wasabato (Seventh.Day Adventists)”. Hapa chini yapo maelezo mafupi kuhusu yale wanayoyaamini. Linganisha yale wayaaminiyo na kuelewa iwapo yanapatana na maelezo yaliyotolewa katika Sura 3:113-115? Je, hao ndilo lile kundi la “si wote” miongoni mwa waliopewa kitabu, yaani, ambao wamo miongoni mwa hao watendao mema kweli kweli?
Waadventista Wasabato wanaamini:

1. Kwamba wanamtumikia Mungu Mmoja [Allah] na kwamba hawamhesabii Mwenyezi Mungu kuwa anao washirika kama vile Bikira Maria na wengine waitwao watakatifu wanaoabudiwa. Injili Yakobo 2:19 ‘Wewe waamini kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema..’…

2. Wanampa Mwenyezi Mungu roho zao zote. (Injili) Luka 10:27 ‘Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.’
3. Hawamtumikii Mwenyezi Mungu kwa njia ya sanamu na mifano, vitu hivyo vimekatazwa kabisa. Kutoka 20:4-6 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote …Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako [Allah], ni Mungu mwenye wivu…”

4. Wanaamini kwamba siku ya saba (siku ya mwisho) ya juma ni siku bora kuliko zote. Wanaiheshimu siku ile kwa kumfanyia ibada Muumbaji [Allah]. Ni siku ile iitwayo “Sabt” ambayo ina maana ya ‘pasipo kazi’ katika lugha ya Kiarabu. Wanazifuata amri zote za Mwenyezi Mungu kama zilivyotolewa katika (Taurati) Kutoka 20:8-11 ‘Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.’ Wao wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Muumbaji na ya kwamba aliiumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake kwa siku sita na kupumzika siku ya saba.
Sura 10:3

10:003 ‘Bila shaka Mola wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Arshi yake [Kiti chake cha enzi]. Yeye ndiye anayepitisha mambo yote. Hakuna Muombezi ila baada ya idhini yake (Mungu). Huyu ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Basi Muabuduni Yeye. Je! hamkumbuki (kuwa hayo mliyo nayo siyo mambo ya haki)? Sura 10:003 Yunus

Hebu fikiria tu jinsi wewe mwenyewe uwezavyo kuitumia siku nzima, yaani, siku ile ya mwisho, (ya saba) ya juma, siku bora kuliko zote, kwa ajili ya kujitoa kabisa kwake Mwenyezi Mungu! Kuitumia siku hiyo kumwabudu na kumsifu Mwenyezi Mungu, kushirikiana na kutiana moyo kila mmoja na mwenzake. Kuweka kando biashara yote na mambo ya ulimwengu huu, mambo yote yanayosambaratisha mawazo yako, na kuichukua familia yako kwenda kumwabudu Mwenyezi Mungu na kutumia muda huo pamoja na kila mmoja pengine kwa kutembea kimya kimya kuangalia viumbe vya asili. Kweli huu ndio mbaraka ambao wachache mno huutambua. Je, huo usingejumuisha kumpenda Mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote?
Jambo la mwisho, watu hao ni wafuasi wa Isa al-Masih (Kristo aitwaye Masihi). Sura 3:055

3:055 (Kumbukeni) Mwenyezi Mungu aliposema: ‘Ewe Isa! Mimi nitakutimizia muda wako wa kuishi (hawatakuua hao maadui). Na nitakuleta kwangu, na nitakutakasa na wale waliokufuru, (hawataweza kukudhuru) na nitawaweka wale waliokufuata, juu ya wale waliokufuru, mpaka siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyokuwa mkihitilafiana.’ 3:055 Aali Imran. Msomaji anaombwa ajifunze juu ya Waadventista Wasabato.

BISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Aya zimenukuliwa kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913

Mafungu ya Biblia yanatoka katika Toleo la King James (KJV)

Kwa maelezo zaidi: www.salahallah.com

‘Waliopewa
Kitabu’

… si wote sawa!

Sura 3:113-115

Aali Imran

Mfululizo na. 02

SABATO NJEMA

Jumanne, Februari 01, 2011

MLANGONI PA MOYO MGENI AMESIMAMA

Kuna kisa cha tajiri mmoja aliekuwa na utaratibu wa ajabu kwamba, alipokuwa akifika nyumbani kwake! akishafunga milango hata ugongeje, jibu lake huwa ni kwamba akishafunga hafungui.
Ikatokea siku moja bwana akawa amejifungia ndani moto ukachoma nyumba jirani zake wakaja kumuokoa, walipogonga mlango na kumueleza moto unachoma nyumba yake afungue mlango atoke, jibu alilosema! NIKISHAFUNGA MLANGO SIFUNGUI.
Waishio mjini inasadikiwa sio wastaarabu ingawa wanapaswa wawe wastaarabu kwa sababu wanaishi na wastaarabu.
Tunajifunza kuwa Yesu naye ni mstaarabu.
Vipi kwa mtu alietoka kijijini akaja mjini, kwa sifa anazozifahamu za watu wa mjini akifika asizikute, unadhani atakuwa katika khali gani.
Au ndio ukishafika toka huko ulipokuwa na kuja mjini, basi wewe ni wa kimjini?