Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Februari 01, 2011

MLANGONI PA MOYO MGENI AMESIMAMA

Kuna kisa cha tajiri mmoja aliekuwa na utaratibu wa ajabu kwamba, alipokuwa akifika nyumbani kwake! akishafunga milango hata ugongeje, jibu lake huwa ni kwamba akishafunga hafungui.
Ikatokea siku moja bwana akawa amejifungia ndani moto ukachoma nyumba jirani zake wakaja kumuokoa, walipogonga mlango na kumueleza moto unachoma nyumba yake afungue mlango atoke, jibu alilosema! NIKISHAFUNGA MLANGO SIFUNGUI.
Waishio mjini inasadikiwa sio wastaarabu ingawa wanapaswa wawe wastaarabu kwa sababu wanaishi na wastaarabu.
Tunajifunza kuwa Yesu naye ni mstaarabu.
Vipi kwa mtu alietoka kijijini akaja mjini, kwa sifa anazozifahamu za watu wa mjini akifika asizikute, unadhani atakuwa katika khali gani.
Au ndio ukishafika toka huko ulipokuwa na kuja mjini, basi wewe ni wa kimjini?

Maoni 3 :

  1. Inasemekana mjini wezi wengi na wote wako mlangoni na labda wote wanaita BWANA BWANA! Na twajua sio kila aitaye BWANA BWANA atauona ufalme.


    Kwa hiyo labda tatizo ni tutambuaje MGENI aliyepo mlangoni sio kibaka wakati siku hizi hata kwa kucheki wingi wa makanisa na wanaomuhubiri BWANA kwa kupigia watu hodi hata kwa kuonyesha miujiza wengi yasemekana ni FEKI TU?

    JibuFuta
  2. Falsafa na wazo ndani ya neno...mawazoni.

    JibuFuta