Kila Mmoja Bila Kutegeana.
Inawezekana
kuwa na furaha na amani katika ndoa au uhusiano ulionao kama wote wawili
mtawajibika bila kutegeana,kwani ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha uhusiano
alionao unakuwa na furaha wakati wote,haiwezekani katika muungano wa watu
wawili kama mke na mume mmoja akaonekana kufaidi zaidi ya mwingine tupeane
haki sawa kila mmoja amfurahishe mwenzie.
|
Inapendeza kuwa na amani na furaha kwa wote wawili kwani kila mmoja anajua jukumu lake kwa mwenzi wake ikiwa ni baba au mama alimradi kuwepo na maelewano baina yao,na kama utafahamu nini mwenzio anakipenda naye pia akawa anatambua kipi unapenda ni rahisi kudumu katika ndoa hata mahusiano kutokana na maelewano mazuri
Kama
itatokea mahusiano yana mapungufu ya mmoja kukosa kujituma ili kutimiza
mahitaji ya ndoa kwasababu zilizo ndani ya uwezo,,basi uwezekano wa kuwepo na
migogoro ni mkubwa,na katika hali kama hii haitashangaza suala la uaminifu
kukosekana kutokana na kwamba mmoja anaona hapati mahitaji ya msingi kutoka
kwa mwenzake mume au mke.maisha ya ndoa yanaitaji mawasiliano ya mara kwa
mara,kwani kwa kufanya hivyo inaleta ushirikiano ,na uwazi ukiwa ni silaha ya
kujenga zaidi..usinyamaze kimya kwa matatizo yanayojitokeza kwani kwa kufanya
hivyo ni kuhatarisha mahusiano yenu.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni