Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Desemba 12, 2014

MSITU MSITUNIUkiwa mbali na msitu, yaani kabla hujaingia msituni utauona msitu ni mkubwa sana. Utaona eneo lote la msitu limejaa miti na huwezi kuona hata ardhi. Kwa umbali uliopo unaweza kuamini kwamba hakuna hata sehemu ya kupita kwenye msitu huo.

Ila unapoingia kwenye msitu huo, huoni tena msitu. Yaani unapokuwa msituni huoni tena msitu, bali unaona mti mmoja mmoja na kuna sehemu kubwa ya kupita. Unaweza kuupita mti mmoja baada ya mwingine na kuendelea kufanya yako…

Kabla hujaingia kufanya jambo lolote utaona vikwazo vingi sana, utaona hatari na ilivyo rahisi kushindwa. Ila unapoingia kwenye jambo hilo, vikwazo vilivyokuwa vinakutisha mwanzo unakuta sio vikubwa kama ulivyokuwa unafikiri. Unakuta ni changamoto ndogo ndogo ambazo unaweza kuzimudu.

Usiogope tena kufanya kile unachotaka kufanya, huwezi kuona msitu ukiwa msituni…

Nakutakia kila la kheri.


Chanzo: Makirita Amani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni