Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Mei 04, 2014

Vita vya YOM-KIPPUR na funzo kwa dunia


Photo Credit By: Wikipedia

Tupo kwenye miaka 40 toka vita vya YOM-KIPPUR kuanza vita hii ilianza tarehe 06-10-1973 nchi za kiarabu zilijipanga vilivyo ili tu kurejesha ardhi zao walizopoteza katika vita vilivyovunja record ya Dunia vita vilivyopiganwa kati ya nchi za Ki-arabu na Israel kwa mda wa siku sita Mwaka 1967 na majeshi ya nchi za Ki-arabu kusalimu Amri na kuacha ardhi zao kutekwa na askari wao kwa mamia kupoteza maisha yao na Maelfu kutekwa.

 Vita hii iliacha maumivu na makovu makubwa sana katika ulimwengu wa Kiarabu hata kupelekea nchi hizo hasa Misri na syria kuanza mikakati ya kukomboa ardhi zao zilizotekwa na Mjeshi ya Israel,kwa maana syria milima ya Ki-mbinu ya Golan ilikuwa imetekwa na kwa upande wa Misri ilipoteza Jangwa lote la sinai ikiwa pamoja na Mfereji wa Suez nchi hizi zilikuwa na machungu sana hasa ikichukuliwa kuwa nchi iliyowashinda ni ndogo sana hivyo mipango iliyofanywa mwaka 1973 ni kuzikomboa ardhi zilizotekwa baadaye kuifutilia mbali Israel katika uso wa Dunia.

 Mipango ya kuivamia Israel ilipangwa ifanyike siku ya Jumamosi ambapo kulikuwa na sikukuu ya Kiyahudi inayojulikana kama YOM-KIPPUR,Siku hiyo Israel ilipata changamoto kubwa ambayo katika historia ya nchi hiyo Kivita haijawahi kutokea, maana siku hiyo Maelfu ya vifaru na Makumi elfu ya Majeshi na ndege za kijeshi zilifanya shambulizi la kushitukiza na kwa pamoja katika mipaka ya Israel ya kusini na kaskazini hii ilikuwa Ishara tosha kuwa Syria na Misri zilikuwa zinataka kurudisha ardhi zao zilizotekwa katika vita vya siku sita vya mwaka 1967.

 CHANZO CHA VITA YA YOM-KIPPUR.  Baada ya Israel kushinda vita vya 1967 Israel ilipata ardhi kubwa ambayo ilipaswa kulindwa kwa gharama yoyote ili kupata Muafaka wa kisiasa kati ya nchi hiyo na nchi za Kiarabu kwa upande wa Misri Israel ilichukua Sinai na Suez canal hivyo Jeshi la Israel lilipata changamoto kubwa sana kulinda mpaka wote wa sinai na Mfereji wa Suez,Majeshi ya Israel yaliweka vituo vya ulinzi vilivyojulikana kama BAR-LEV line,na kwa upande wa Syria Israel ilichukua Milima ya Golan ambayo kwa Israel lilikuwa eneo jipya lililotakiwa kulindwa kwa nguvu zote maana Ki-Jeshi lilikuwa ni strategic la kimbinu sana Maana milima hiyo ya Golan iko kwenye mwinuko kwa hiyo eneo hilo likishikiliwa na Syria ina maana Majeshi ya Syria yana Uwezo wa kumiliki Kijeshi ndani ya Israel kilomita zaidi ya 25 na wakati huohuo Israel haingekuwa na uwezo wa kupata target Shabaha nzuri kupiga majeshi ya Syria yaliyoko kwenye milima hiyo ya Golan na ndiyo maana mpaka leo Israel haiwezi kuiachia milima hiyo maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA kwa jeshi la Israel,Badala yake Inataka kuirudisha milima hiyo kwa kubadilisha na AMANI na Syria ili wawekeane mkataba wa AMANI na kutoshambuliana na Israel ili iweze kupata uhakika wa kutoshambuliwa toka milima hiyo ya Golan.

 Baada ya vita vya 1967 Msri na Syria zilianza kujenga majeshi yao ili waweze kukomboa ardhi zao zilizotekwa, Nchi hizo zilihitaji zana za kivita zaa kisasa ili kuweza kummaliza adui yao Israel walihitaji sana kupata silaha toka Urusi wakati huo USSR Walihitaji kupata Ndege aina ya MIG na vifaru aina ya T-62 Vilevile makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-2,3,6 na SA-7 pamoja na silaha za kubomolea Vifaru aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES.

 Kufikia mwezi October 1972 Rais wa misri wakati huo Anwar Sadat aliwahi kuongea na makamanda wake kuhusu kuishambulia israel na ilipofikia mwezi may 1973 vyombo vya kijasusi vya Israel vilikuwa vimepata habari kuwa Misri itaishambulia Israel kupitia mfereji wa Suez Misri walikuwa wanajua kuwa kama Misri itaishambulia Israel basi Syria nayo ingejiunga na kuishambulia Israel kutokea Kaskazini. Vilevile Israel walidaganyika kuwa Misri itaishambulia Israel mara tu itakapopokea ndege aina ya MIG-23 na SCUD-D toka Urusi Jeshi la Israel lilijua kuwa Misri haijapokea silaha hizo toka Urusi hivyo iliamini Misri haiwezi kuanzisha vita hivyo kabla ya kupokea silaha hizo toka Urusi.

 Mwezi May na Mwezi August 1973 Majeshi ya Misri yalifanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la mpaka na Israel,Israel nayo ilipoona hivyo ilianza kukusanya askari wake kwa maandalizi ya vita lakini baada ya pale hakukuwa na harakati zingine za kijeshi katika eneo hilo la mpaka hivyo Jeshi la Israel liliona kuwa hiyo ilikuwa kawaida tu yaani waliona kama yalikuwa mazoezi ya kawaida tu.

 Septemba 25,1973 Mfalme hussein wakati huo alikutana na waziri mkuu wa Israel wakati huo Mama Gold Meir wakati huo Mfalme Hussein alishakutana na Rais Sadat na Assad wa Syria na alimwonya waziri mkuu wa Israel kuhusiana na kukalia eneo la Syria la milima ya Golan na Sinai eneo la Misri,Baada ya kumalizika kikao hicho na Mfalme Hssein waziri mkuu wa Israel pamoja na waziri wa ulinzi wa Israel wakati huo MOSHE DAYAN pamoja na vyombo vya Kijasusi vya Israel waligundua moja kwa moja kuwa Misri ingewashambulia wakati wowote.

 Masaa machache tu kabla ya Misri kuishambulia Israel tarehe 06-10-1973 waziri mkuu Golda Meir na waziri wa Ulinzi Moshe Dayan na Mkuu wa utawala jeshini Gen.David Elazar kwa pamoja waliamua kuwaita wanajeshi wa anga wale wa akiba na wale wa vifaru wale wa akiba maana walijua hapo sasa vita haiepukiki.

 Kabla ya vita siku hiyo majeshi ya pande zote mbili yalikuwa na zana zilizokuwa zinakisiwa kuwa hivi:
 ISRAEL        
       
 Ndege za kivita 358 
 Vifaru 2100
   Meli za kivita 37

MAADUI ZAKE

Ndege za kivita 998
Vifaru 4350
Meli za kivita 137
 Ilipofika saa nane kamili mchana majeshi ya Msri na yale ya Syria yalianza kumimina makombora kuelekea katika sehemu zilizokuwa zinakaliwa na Israel,Misri na Syria zilichagua siku ya jumanosi maana ilikuwa ni sikukuu ya kiyahudi ya YOM KIPPUR waliona siku hiyo wayahudi wote huwa wanasherehekea hivyo ilikuwa upenyo mzuri sana kwao.

 Kwa upande wa Sinai majeshi ya Msri yaliweza kuvuka mfereji wa Suez kupitia sehem tano tofauti na kwa upande wa mizinga Misri iliweza kukipiga kituo cha wanaanga wa Israel waliokuwa Refidim katika jangwa la sinai na vikosi vingine vya mizinga vya Israel vilishasmbuliwa na mizinga ya Misri,na kufikia saa 11 jioni maelfu ya Wanajeshi wa misri walikuwa wamefika upande na kulikamata eneo lote la mashariki mwa mfereji wa Suez na wakati wa usiku vikosi vya vifaru vilivuka mfereji wa Suez hapo ndipo hali ya uwanja wa vita ilibadirika kabisa kwa Israel uwepo wa askari wa miguu wa Israel na mizinga yao hakukuweza kuyasimamisha majeshi ya Misri. Division ya 252 na Brigedi ya 14 ya kikosi cha vifaru viliadhirika vibaya sana asilimia kubwa ya vifaru vyao vilikuwa vimeangamizwa na silaha aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES toka Misri.

 Jeshi la anga la Israel lilipoitwa ili kudhibiti majeshi ya Misri,Ndege hizo zilijikuta zinaangushwa na mizinga ya kuangushia ndege, Misri iliweza kuzitungua ndege za Israel kiasi cha kuzimalizia uwezo wa kushambulia na baada ya kujipanga vizuri na kujua namna ya kukwepa makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-7 ndege za Israel ziliweza kuziangamiza helcopter zilizokuwa zimebeba Makamandoo wa misri na kuweza kuzitungua ndege 7 aina ya MIG kwenye uwanja wa mapambano. mapambano hayo yalifanyika kusini mwa mfereji wa Suez ndege hizo ziliangushwa na ndege za Israel aina ya PHANTOM.

 Kwa upande wa milima ya Golani majeshi ya Syria yaliweza kusonga mbele huku mizinga na vifaru pamoja na askari wa miguu waliweza kumiminia mizinga,risasi majeshi ya Israel kwa saa nzima mfululizo wakati huo Israel ilikuwa na Brigedi mbili za vifaru Division ya 36th ndiyo ilikuwa mstari wa mbele na Brigedi 188th nayo ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kusini ya mlima wa Golani na Brigedi ya 7th ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kaskazin mwa mlima Golan hivyo vifaru vya Israel havikuweza kuvishambulia vikosi vya Syria sababu havikuwa kwenye RANGE ya kuweza kushambuliwa.

 Mapigano ya vifaru yalianza tu siku hiyo baada ya jua kuzama majeshi ya Syria yaliweza kupenya ngome za Majeshi ya Israel kwa kuwa walikuwa wanatumia NIGHT-VISION viona usiku hivyo vilisaidia sana majeshi ya vifaru vya Syria vifaru vya Israel vilivyokuwa upande wa kaskazini havikuweza kufua dafu mbele ya vikosi vya Syria,vifaru vya Syria viliweza kushika sehemu ya kusini mwa mlima Golan na ilipofika asubuhi ya tarehe 07-10-1973 vifaru zaidi ya 600 vilikuwa vimeingia ndani ya ardhi ya Israel na vilikimbilia kwenda kulishika Daraja mhimu la nto Jordan na kambi ya kijeshi ya Nafar,Israel pia ilipoteza mlima wa HELMON ambao ulikuwa wa kimbinu strategic nao uliangukia mikononi mwa majeshi ya Syria hili lilikuwa pigo kubwa kwa majeshi ya Israel.

 Kwa upande wa majini majeshi ya Israel yaliweza kuziangamiza boat zilizokuwa zinabeba makombora za Syria na miji yote iliyokuwa inazunguka milima ya Golan wakazi wake waliondolewa na majeshi ya Israel.na baada ya siku 18 Majeshi ya Israel yaliweza kujijenga upya na kuchukua tena eneo lote la milima ya Golan na mlima Hermon.

Chanzo: http://wikileaks01.wordpress.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni