Kisiasa hakuwa na umuhimu sana kwa sababu nchi yake ilikuwa ndogo tena
nafasi ya mfalme katika Ubelgiji haikuwa na mamlaka kubwa. Lakini Leopold II
alifaulu kama mwanabiashara aliyetafuta kila njia ya kuongeza mali yake. Kwa
njia hii alianza kujihusisha na habari za Afrika na hasa Kongo.
1884 Marekani ilitambua "Dola huru ya Kongo". Sasa athira yake ilikuwa kubwa kiasi ya kusababisha mashindano kati ya mataifa mengine ya Ulaya juu ya athira katika Afrika. Mkutano wa Berlin wa 1885 ilikubali "Dola huru la Kongo" kama nchi ya kujitegemea iliyokuwa mkononi mwa shirika la Leopold.
Leopold mwenyewe hakukanyaga ardhi ya Kongo. Nia yake ilikuwa utajiri pekee. Alifaulu kijitajirisha lakini bei kali ililipiwa na watu wa Kongo.
Badala ya kulinda wenyeji dhidi ya biashara ya watumwa jinsi alivyotangaza
kote duniani alikodi malighafi za Kongo kwa watu na makampuni waliompa pesa.
Makampuni haya yalipewa mamlaka ya kulazimisha wenyeji kuwafanyia kazi ya
lazima kama kubeba mizigo na kukusanya mpira msituni. Leopold alitajirika kwa
sababu teknolojia mpya ya matairi ilihitaji kiasi kikubwa cha mpira
iliyopatikana pekee katika misitu ya nchi za tropiki kama Kongo. Baadaye
mashamba ya mipira ilianzishwa lakini wakati ule viwanda vilitumia mpira
asilia.
Baada ya upinzani kukua mwaka 1908 Leopold alikabidhi Kongo kwa serikali ya Ubelgiji ikawa Kongo ya Kibelgiji. Leopold alipokufa mwaka uliofuata watu barabarani walikashifu maiti yake ilipopita wakimwita aibu ya taifa.
Leopold II alikuwa mfalme wa Ubelgiji
tangu 10 Desemba
1865 hadi 17 Desemba
1909. Alimfuata babake
Leopold I aliyekuwa mfalme wa kwanza wa nchi baada ya kuanzishwa kwa taifa
hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni