Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Septemba 02, 2012

MAZOEZI NI DAWA

Katika ripoti kuhusu faida za mazoezi, mtandao wa ''exercise is medicine''(mazoezi ni dawa) ulioanzia nchini marekani, umetoa ushahidi wa kitafiti kwamba, mazoezi yakifanyika mara kwa mara na katika kiwango kinachotakiwa:

1. Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 40
2. Huzuia kupata kiharusi(stroke) kwa asilimia 27
3. Huzuia kupata kisukari kwa zaidi ya asilimia 50
4. Huzuia kupata shinikizo la damu(hypertension) kwa asilimia 50
5. Huweza kuzuia kufa kutokana na saratani, au kuzuia kujirudia kwa saratani ya matiti kwa asilimia 50
6. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo mpana(colob cancer) kwa zaidi ya asilimia 60.
7. Hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kusahau kwa asilimia 33.
8. Hutibu msongo wa mawazo(depression) kwa kiwango sawa na dawa za kutibu ugonjwa huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni