Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Julai 23, 2012

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Photo By: www.rhodayouths.wordpress.com


Ukijua unachokithamini itakusaidia kuwa mkweli kwako binafsi, hata wakati mtu mwingine
anapokulazimisha kufanya kitendo unachodhani ni makosa. Maadili yako yatakusaidia kuchagua
lililojema kwako; ambalo wakati mwingine, baada ya kuchagua, itabidi uishi nalo daima.

StaDi Za MaiSha
Unahitaji stadi za maisha pia ili uwe salama. Kusema kweli “Stadi za maisha” zinaweza kuwa stadi za kuokoa maisha, kama vile;

Kuelezea hisia zako. 
Hisia zako ni muhimu, lakini watu wengine hawawezi kujua unavyojisikia mpaka uwaeleze. Jifunze jinsi ya kuwafanya watu wengine wajue kile unachofikiri na unachokitaka kwa kusema moja kwa moja na kutumia sentensi zinazoanzia na “mimi” – “mimi ninataka” “mimi ningelipenda” “mimi ninahitaji”“mimi Sipendi” ………… .” Fanya mazoezi ya kutumia sentensi zinazoanza na “mimi” mpaka utakapozoea na kujisikia huru kuzitumia.

Tetea hoja yako. 
Una uhuru wa kufikiri na kujihisi unavyopenda. Ni vema kujifunza jinsi ya kuwasilisha
mawazo yako kwa wengine bila ya kuwaudhi au kuwafanya wajisikie vibaya, usionyeshe uadui, ugomvi wala kukosoa sana.

Tetea unachoamini bila kujali wanayosema watu wengine.
Kila mtu ana imani na yaliyo sahihi na yasiyo sahihi, mazuri na mabaya. Imani hizi zinaitwa kanuni. Wakati mwingine unaweza ukawa unajua kanuni zako lakini mambo yanaweza yasiwe wazi sana kiasi cha kukufanya utumie muda kufikiria lipi ni sahihi kwako na ni kwa nini. Iwapo unao uhakika wa usahihi wa kile unachofikiria na kwa nini unakifanya, na kwa nini hupendelei kukifanya utaweza kusimama imara na lile unaloamini. Hivyo basi msimamo wa namna hii utakupa heshima mbele za watu.

Jihadhari na yanayotokana na shinikizo.
Jinsi unavyoelekea kwenye utu uzima unatakiwa kufanya maamuzi mengi peke yako. Wakati mwingine watu wengine wanaweza kukuhimiza na kukusukuma kufanya maamuzi fulani na ukushawishika kufanya hivyo.

Lakini ufahamu kuwa kufanya maamuzi mazuri maana yake ni kupima chaguo zote zilizopo na kufikiria matokeo kwa kila chaguo.Inaweza ikawa kazi ngumu iwapo kuna mtu anakuharakisha au anakushinikiza uamue haraka. Kitu muhimu katika kufanya maamuzi bora ni kuwa na uhakika wa kanuni zako na malengo yako ya maisha kwa ujumla.
Kuwa na msimamo wa pekee ndiyo stadi za Maisha.

Maoni 1 :