Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Julai 22, 2012

BADILIKO KUBWA, CHANGAMOTO KUBWA

Image By: www.imkeepingup.com

 Mahali pengi ujana umekuwa mgumu kueleweka, na hasa siku hizi vijana wanapata matatizo ambayo wazazi wao, mabibi hata babu zao hawakuwahi kuyapitia.
 
VIJANA TOKA KENYA NA GHANA WANAELEZA HIVI:
 
Patric, kutoka Kenya (Umri,miaka 16)
“Nilichokifurahia katika ujana balehe wangu ni kuwajibika katika majukumu ya nyumbani hasa wazazi wanapokuwa hawapo. Majukumau haya nayapenda kwasababu ninadhani nimeshakua na ninaweza kujidhibiti mimi mwenyewe na wadogo zangu”.

Naana, kutoka Ghana. (Umri; miaka 17)
“Yapo mambo mengi yanayomhusu kijana balehe ambayo siyapendi. Ninakumbuka nilipokiwa na umri mdogo nilikuwa na uhuru zaidi kuliko sasa.Lakini kwa sasa zipo sheria na miongozo mingi.”

TUKIANGALIA;

Mwonekano wako mpya na kujitambua kwako kunawafanya wazazi, shangazi zako na wajomba kuwa na wasiwasi kwa sababu wasingependa upate matatizo na wala wasingependa ufanye makosa makubwa kama vile kupata mimba (au kwa kumpa mimba rafiki wa kike) wakati ungali unasoma. Zaidi ya yote wanakuwa na wasiwasi kwa sababu wanafahamu kwamba umri kati ya 10-19 unaweza kuwa na athari kubwa katika ukuaji wako na aina ya maisha utakayokuwa nayo.

JE UNAFAHAMU VIJANA HUFIKIRIA KWAMBA HAKUNA JANGA LINALOWEZA KUWAPATA?

Ni tabia ya vijana duniani kote, katika nchi tajiri na maskini – kufikiria kwamba mambo mabaya
hayawezi kuwatokea. Hujiambia,

“ Haitatokea kwangu”. Wakati mwingine hujiamini sana na kuhisi wako salama mno.

Je wewe uko hivi? 
Unadhani unaweza kujaribu kitu cha hatari na lisikupate jambo? 
Kwa mfano, wewe na rafiki yako wa kike (msichana) mnafahamu kuhusu dawa za kuzuia mimba. Lakini
mnadhani kwamba ili mradi hamjamiiani mara kwa mara, msichana hawezi akapata mimba.

Au unaweza ukawa na ufahamu mkubwa kuhusu VVU, virusi vinavyo sababisha UKIMWI. Unaweza
ukafahamu kwamba maambukizi yanaweza kutokea kwa njia ya kujamiiana bila kinga, lakini unafikiri kwamba rafiki yako wa kiume hawezi kuwa na maambukizo. Unakataa kufikiri kuwa unaweza kupata maambukizo ya VVU na haiwezekani pia kwa wale watu unaowafahamu kupata ugonjwa huo.

Je haya yanakuhusu? 
Kama ndivyo, hapa kuna mambo ambayo unahitaji kuyazingatia:

Nitarejea kukwambia kuhusu: 
WEWE, MAISHA YAKO NA NDOTO ZAKO.

Maoni 1 :