Kijitabu kinachoelezea kwa Lugha rahisi Mkakati wa Kupunguza Umasikini
Tutapunguzaje Umasikini?
Mpango Mzima
Baada ya kuzungumza na watu wa kawaida na mabingwa mbalimbali; Serikali imeamua kwamba mambo matatu lazima yafanyike kama tutakuwa makini katika kupunguza umasikini.Kuweka malengo ya kitaifa yaliyo wazi:
· Badala ya kuwa na hotuba nyingi zenye nia nzuri lakini utakelezaji wake ni duni, Serikali imeamua kuweka malengo yanayoeleza yanayopaswa kutendwa. Kwa mfano, kuongeza idadi ya watoto waliochanjwa dhidi ya surua wenye umri chini ya miaka miwili na kupata chanjo ya Donda Koo, Kifaduro na Pepo Punda (DPT) toka asilimia 71% hadi kufikia 85% mwaka 2003. | |
· Jozi ya kwanza ya malengo inawezekana isiwe sahihi. Kwa hiyo kila mmoja anapaswa kuzingatia kwa makini yanayotokea na asaidie kubadili malengo au namna ya kuyatekeleza. Matendo mengi hayawezi kutekelezeka hadi mipango ya mabadiliko ya serikali za Mitaa imetekelezeka. |
Kubuni Mazingira ya Kiuchumi ya Kitaifa ambayo yatachochea Maendeleo
|
|
Kufanya kazi pamoja na Serikali za nje na mashirika ya kimataifa
|
Zingatia mwongozo wa mawazo matatu:
Watu wengi walihusishwa katika kutayarisha makala ya Njia za Upunguzaji Umasikini. Katika siku zijazo serikali itawahusisha watu wengi zaidi katika maamuzi ya yanayopaswa kufanywa, katika kutenda, na katika kuhakikisha kuwa yaliyoamuliwa yanatekelezwa kwa kuzingatia mipango ya awali.Kila jambo ambalo lipo katika mpango wa kupunguza umasikini linaongozwa na mawazo matatu yafuatayo:
Je, tunawezaje kusimamia kwa ukamilifu zaidi na kuona kuwa tunatekeleza tuliyokusudia?
kupunguza umasikini wa kipato kuendeleza ubora wa maisha na ustawi wa jamii kupunguza dhiki za makundi ya umasikini
Haja ya kuwa na Viashirio
Tunapaswa kufahamu kuwa fedha zetu zinatumika vyema. Maana yake ni kuwa inabidi tuwe na hakika na kile tunachotaka kufanya. Aidha, tunapaswa kuangalia kama tunafaulu katika yale tunayoyafanya.Awali tuliona kuwa malengo yaliwekwa kwa ajili ya matendo mbalimbali ya kupunguza umasikini. Kwa kila tendo tunapaswa kuwa na dalili (viashirio) zinazotuwezesha kupima kama tunatekeleza malengo yetu au hapana. Serikali imeweka njia za ushauri ili kuonyesha dalili za umasikini zinakuwaje.
Viashirio (dalili) vya aina tatu
Si rahisi kuamua mapema ni dalili zipi bora na rahisi za kutumia. Kuna aina mbalimbali zilizo katika mfumo wa kubuni viashirio. Kimsingi, kuna aina tatu za viashirio:Dalili za athari na matokeo
Ni za msingi na zinaweza kupima kwa urahisi uthabiti wa matendo ya mara kwa mara (kwa mfano idadi ya watoto chini ya miaka miwili ambao wamechanjwa dhidi ya surua kila mwezi).Dalili za kati
Zinapimwa katika kipindi cha muda mrefu. (Kwa mfano, idadi ya familia ambazo zinapata maji safi na salama) ·Dalili za uwakilishi
Hupima vitu vya nje vinavyowakilisha vitu vya msingi ambavyo si rahisi kupimwa (kwa mfano, matumizi ya vifaa vya kisasa vya ujenzi wa nyumba kama njia ya mapato).Kujenga Mfumo wa Usimamizi na Tathmini
Muda mwingi, nguvu na fedha vinaweza kupotea kama mfumo wa ukusanyaji taarifa utakuwa mgumu na wenye urasimu. Kazi ni kuwa watu wote wanaohusika kufikiria viashirio bora ambavyo vinaweza kupimwa mara kwa mara na kwa urahisi.Taarifa zinaweza kukusanywa kuhusu watu binafsi, kaya, wilaya, mikoa au nchi nzima. Ukusanyaji huu unaweza kuwa wa mara kwa mara au wa kufanya mara moja. Unaweza pia kufanywa baada ya kila miaka kadhaa. |
|
Taarifa kuhusu elimu, afya na maji zinaweza kukusanywa kupitia mfumo wa utawala uliopo. Serikali za mitaa hutuma taarifa kwa ngazi ya juu ya serikali. | |
Taarifa nyingine zitakusanywa kwa sensa au kwa ukaguzi kama vile ukaguzi wa bajeti za kaya au ukaguzi wa nguvukazi. Zinaweza kuelezea mada nyingi. · | |
Taarifa za kiwango cha serikali za vijiji zinaweza kukusanywa kwa ajili ya matumizi katika kiwango cha kijiji. Taarifa hizi zinaweza kukusanywa kwa kutumia rejista za vijiji na kuhoji wanajumuia. Ingawa taarifa za vijiji zitatumiwa katika kiwango cha serikali za vijiji, lakini data hizo zinaweza pia kutumiwa kwa kulinganisha na takwimu za kiserikali. Njia hii itawawezesha viongozi kujua jinsi watu, hasa watu masikini, wanavyoona hali zao. |
Mashirika mengi yatahusishwa katika ukusanyaji na ufafanuzi wa taarifa na pia kuelezea taarifa hizo zina maana gani katika utungaji sera kwa siku zijazo. |
|
Kwa hiyo, ni lazima tuwe tayari kukabili changamoto hii. Bado kuna udhaifu mwingi katika kusimamia shughuli za kuondosha umasikini. Mkakati wa umasikini (PRSP) ni nafasi nzuri ya kujenga mfumo bora na madhubuti. Kama ilivyotajwa katika mkakati huo (PRSP), “Serikali inakusudia kutafuta uwakilisho wa watu masikini na washika dau wengineo katika utekelezaji, uangalizi na kufanya tathmini ya mbinu za kupunguza umasikini na baadaye Kubadili Mbinu zitumikazo”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni