Malengo, shughuli na Viashirio
Inasemekana kuwa “kama hujui uendako basi barabara yoyote itakufikisha”. Watu
ambao hutekeleza mambo wanayoyataka wana mwelekeo sahihi wa kitu wanachotaka kufanya,
watakifanya vipi, na hasa, jinsi watakavyofahamu kuwa wamefaulu.
Lile lililo kweli kwa mtu binafsi ndilo lililo kweli kwa jamii, katika nyanja
mbalimbali na kwa serikali. Kama uko makini kutenda jambo basi lazima uwe wazi kuhusu
malengo, shughuli na viashirio.
MALENGO |
Wazo lililo wazi kwa lile unalotaka kulifanya litakusaidia kuamua
utalitekeleza kwa kiwango gani na muda wa kukamilika. |
SHUGHULI |
Wazo lililo wazi kuhusu shughuli utakayotekeleza litakusaidia kuorodhesha
hatua mbali mbali za kufuata |
VIASHIRIO (DALILI) |
Wazo lililo wazi kuhusu utakachopima litakusaidia kujua shughuli
zinazotekelezwa zinafikia lengo au kuvuka. |
Sehemu hii inaorodhesha malengo, shughuli na viashirio ambavyo vimebainishwa kwa mawazo
yanayoongoza katika Mkakati wa Kuondoa Umasikini (PRSP) ambazo ni:
| Kupunguza umasikini wa mapato |
| Kuendeleza ubora wa maisha na ustawi wa jamii |
| Kupunguza madhara yanayoweza kuwapata watu masikini |
Kwa ujumla njia ya kupunguza umasikini wa mapato ni kuziwezesha shughuli za kuzalisha
mapato ya aina mbalimbali zistawi ili pawe na kazi nyingi zaidi na fedha nyingi ziwepo
kwenye mzunguko. Njia ya kuendeleza ubora wa maisha na ustawi wa jamii ni kuhakikisha kuwa
watu wote wanapata nafasi sawa ya kupata elimu, afya bora, maji salama na chakula bora.
Njia ya kwanza ya kupunguza madhara ni kuainisha watu ambao wako katika hali mbaya na
kugundua matakwa yao ni yapi na kuweka bayana malengo, shughuli na viashirio.
Kupunguza Umasikini wa Kipato
Kama nchi kwa ujumla ingekuwa tajiri zaidi basi panatakiwa pawe na umasikini mdogo. Kwa
hiyo inabidi tuifanye nchi iwe tajiri zaidi na tuhakikishe kuwa utajiri huo unagawanywa
sawasawa na kwa haki. Aidha, makundi ya watu dhaifu wanaoathirika na mabadiliko ya hali ya
kiuchumi walindwe kwa utaratibu wa tofauti.
Mpango wa miaka mitatu ijayo ni kuongeza mapato zaidi kutokana na sekta za kilimo, na
viwanda na huduma.
Mpango huu utawezekana kwa sababu ya mabadiliko yanayofanywa na serikali ya kuweka
mazingira bora na uchumi imara.
Tukichukulia kuwa uchumi mpya unawafikia watu masikini zaidi basi tutakuwa tumepiga
hatua ya kupunguza umasikini.
Malengo
|
Hadi 2003 |
Hadi 2010 |
Kupunguza sehemu ya idadi ya watu fukara |
Toka 48-42% |
Toka 48-24% |
Kupunguza idadi ya watu masikini wa vijijini |
Hadi kufikia 7.5% |
Toka 57-29% |
Kupunguza idadi ya watu masikini wa chakula |
Hadi kufikia 3.5% |
Toka 27-14% |
Shughuli
Shughuli ambazo ziatapunguza umasikini wa mapato zinaelezwa katika kurasa zifuatazo:
| Kukuza maendeleo vijijini na kukua kwa biashara ya nje |
| Kusaidia kukuza sekta binafsi |
| Kufanya kazi kwa ajili ya kuboresha na kutoa madaraka zaidi ya serikali |
| Kuhakikisha kuwa uchumi unaimarika |
Viashirio
| · Kupungua kwa umasikini wa chakula |
| · Kupungua kwa umasikini wa mahitaji muhimu |
| · Kupata na kumiliki vifaa kama redio, jokofu (friji), televisheni, n.k. |
| · Kupata na kutumia vifaa vya kisasa katika ujenzi wa nyumba. |
Maendeleo Vijijini na Ukuaji wa Biashara ya nje
Tanzania ina historia ndefu ya maendeleo vijijini. Juhudi za mwanzo zilidhibitiwa na
taifa na kusaidiwa na mfumo mzima wa serikali kwa wazalishaji wa vijijini. Baadaye juhudi
zilitawaliwa na nguvu za soko huria, huku serikali ikijiondoa polepole. Njia iliyo bora
zaidi haijaeleweka. Katika miaka mitatu ijayo Serikali itamwomba kila mmoja kufanya kazi
kwa ushirikiano ili kutafuta ufumbuzi na kuendeleza Mbinu za Maendeleo Vijijini.
Watu masikini na wafanya biashara binafsi wataombwa kuwa mstari wa mbele katika
kutafuta njia mpya za kufaa na madhubuti.
Malengo na Shughuli
| Mikopo itatokana na kwa wanunuzi wa mazao, benki na vyama vya ushirika badala ya kutoka
serikalini |
| Wakulima watajisimamia wenyewe katika makundi au vyama vya ushirika ili kurahisisha
kupata mikopo toka katika taasisi za fedha |
| Wakulima watashirikishwa kufanya utafiti wa mazao na shughuli nyinginezo ili kuongeza
wingi na ubora wa mazao |
| Wanunuzi binafsi wa mazao wataendelea kutumia mpango wa vocha na mipango mingine ili
kurahisisha ununuzi wa mbolea na dawa za kuulia wadudu |
| Jamii zitajishighulisha zaidi katika ujenzi na ukarabati wa barabara za vijijini na
kuendeleza kilimo cha umwagiliaji maji (panapowezekana kwa msaada wa serikali) |
Serikali itajishughulisha tu na kutengeneza sera za kuwasaidia wananchi wa vijijini kwa
kutekeleza yafuatayo:
| Kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, benki za ndani na Washirika wa Kimataifa
katika kutoa mafunzo na mifumo mingine ya misaada kwa jumuiya na makundi kuhusu: |
| Utaratibu wa stadi za uongozi na fedha |
| Kutengeneza na kukarabati barabara vijijini |
| Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji |
| Kuweka mazingira yatakayoendeleza shughuli ndogo ndogo na za kati za biashara |
| Kuendeleza sekta isiyo rasmi |
| kufanya utafiti unaotakiwa na kupanua huduma za mazao |
| Kuendeleza na kuboresha mazao ya kilimo hasa katika zao la korosho, pamba, kahawa n.k.
kwa kutumia nguvu kazi iliyopo. |
| Kueleza mfumo wa uthibiti wa usafirishaji wa mazao ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi |
| Kuhakikisha sheria ya ardhi inamsaidia kila mtu awe masikini au tajiri, mwanamke au
mwanaume na kuhakikisha kuwa sheria nyingine zinazohusiana zinamwezesha mtu kuweka dhamana
ya ardhi ili kupata mikopo. |
| Kuhakikisha kuna sehemu za nchi zilizo nyuma zinapata msaada wa ziada unaotakiwa. |
Serikali itasaidia mahali panapohusika katika kutoa mazungumzo endelevu, huduma za
kilimo na kuwasaidia wawekezaji hodari. Malengo ya siku zijazo ni ongezeko la idadi na
ubora wa mazao ya asili na ya sasa kwa ajili ya biashara ya nje.
Viashirio (dalili)
| Kilomita nyingi za barabara zilizokarabatiwa |
| Ongezeko la thamani ya mazao ya kilimo |
| Uzalishaji wa msimu wa mazao ya chakula muhimu na mazao ya biashara |
Uendelezaji wa Sekta Binafsi
Serikali imekuwa ikisaidia maendeleo ya biashara ya sekta binafsi tangu mwaka 1993 kwa
kushughulika na:
| Sheria ya uwekezaji Tanzania |
| Ubinafsishaji wa shughuli za biashara zilizomilikiwa na serikali |
| Uundaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) |
Hata hivyo, licha ya viwanda vya madini na Utalii, mwitikio wa Wawekezaji binafsi bado
haujawa mzuri.
Malengo na Shughuli
| Kujenga upya uwezo wa kituo cha Uwekezaji Tanzania ili kutilia mkazo ukuzaji wa
uwekezaji |
| Kuwasilisha sheria mpya za makampuni Bungeni |
| Kuanzisha mfumo wa mafaili unaotumia kompyuta kwa ajili ya Mahakama |
| Kuwarahisishia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Tanzania (pamoja
na kulindwa kikamilifu) |
| Kufanya mabadiliko ambayo yatapunguza gharama ya huduma za umma ikiwa ni pamoja na umeme
katika viwanda |
| Kutekeleza kwa haraka mabadiliko muhimu ya Mbinu za Kuzuia Rushwa Kitaifa |
Serikali pia itabuni Mkakati wa kuendeleza Sekta Binafsi ifikapo kwa mwaka 2003.
Hii itasaida:
| Kuendeleza uratibu mzuri kati ya serikali na michango ya Wafadhili |
| Kuweka mazingira bora yanayoimarisha biashara kubwa, ndogo, ya kati na isiyo rasmi |
| Kubadili mfumo wa kodi |
Utawala Bora
Serikali nzuri ni ile ambayo inaweza kutoa huduma bora kwa wananchi wake wote kwa
wakati wote. Pia ina utaratibu mzuri ambao unaiwezesha kukusanya fedha na kuzitumia kwa
uwazi kwa manufaa ya wananchi wote. Kwa sababu ya matumizi ya fedha kuwa wazi na dhahiri
Serikali ya aina hiyo itakuwa inawatumikia watu.
Shabaha zilizotolewa katika Mkakati wa Kuondoa Umasikini (PRSP) ni:
| Kuendeleza utendaji kazi wa serikali katika kutoa huduma za jamii |
| Kuendeleza njia ambazo zinawapa motisha watendaji ili kuboresha kazi |
|
“Viongozi
wazuri wanapoondoka katika nafasi zao watu husema, “tulifanya sisi
wenyewe””.
[Tao te Ching]
|
|
| Kupunguza “upotevu wa fedha” na kuwa na njia ya kuwaadhibu wafanyakazi
wabadhirifu. |
Malengo:
| Mfumo wa Serikali ambao ni madhubuti na unaofaa unawapa watu madaraka ya kujiamulia
maendeleo yao |
| Kupunguza rushwa |
| Kustawisha ubingwa na matumizi bora ya fedha katika mfumo wa serikali |
| Kuimarisha uwezo wa utendaji kazi serikalini |
| Kuimarisha uongozi wa bajeti katika ngazi ya juu na ngazi ya chini serikalini |
| Kuunganisha Mfumo wa Taarifa za Utawala wa Fedha (IFMS) ulioundwa katika wizara zote na
Hazina ndogo. Fedha zote ambazo zinatolewa katika ngazi ya wizara ya Fedha na Hazina ndogo
zitapitia katika Mfumo wa Taarifa za Uongozi wa Fedha (IFM) na mipango yote ya matumizi na
malipo ya nyuma yatawekwa katika kumbukumbu |
Viashirio (Dalili) |
Shughuli |
Imarisha uaminifu na udhahiri katika uhasibu |
Imarisha mfumo madhubuti zaidi wa utawala wa fedha, udhibiti wa malipo na
matumizi, orodha ya vifaa na rasilimali na ripoti za ukaguzi |
Bajeti zitayarishwe kwa wakati katika ngazi zote |
|
Sekta muhimu ya utendaji kazi iliyoendelezwa na kuboreshwa |
|
Mipango iliyoendelezwa na kukubaliwa dhidi ya rushwa katika Wizara za
Kilimo na Ushirika, Elimu na Utamaduni, Afya na Maji, ikilenga katika mbinu dhidi ya
Rushwa Kitaifa |
Fanya ukaguzi wa Mbinu za utekelezaji zilizokubaliwa na timiza mipango
dhidi ya rushwa katika Wizara za Sheria, Ujenzi, Elimu na Utamaduni, Afya, Mambo ya ndani,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, na Mamlaka ya Mapato Tanzania |
|
Tangaza Zabuni za Serikali katika vyombo vya Habari |
Yaruhusu mashirika mbalimbali kutoa huduma za jamii Timiza majukumu chini
ya Programu ya Mageuzi ya Sekta za Umma |
Timiza majukumu chini ya Programu ya mageuzi ya Sekta za Umma |
Mfumo wa Taarifa za Utawala wa Fedha (IFM) utumike katika kutengeneza
bajeti ya serikali, uhasibu na mfumo wa maelezo ya Fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaidaBajeti
ya maendeleo iliandaliwa kwa utaratibu wa GFS |
Panua mfumo wa Taarifa za Utawala wa Fedha kwa wizara zote, idara na
wakala wa serikali Dar es Salaam na Hazina ndogo katika mikoa yote ifikapo 2002 |
Uchumi Mkuu Imara
Wakati uchumi imara unapokua, upandaji wa gharama za maisha unakuwa mdogo na serikali
inakuwa na mlingano wa mahesabu. Serikali ya Tanzania ina rekodi nzuri ya kupunguza
upandaji wa gharama za maisha na malengo kwa miaka mitatu ijayo yatajiegemeza katika hii
njia.
Malengo na Shughuli
| Harakisha ukuaji wa uchumi (GDP) hadi asilimia 6 |
| Upandaji wa gharama za maisha ubakie asilimia 4 |
| Weka akiba ya serikali katika kiwango cha miezi 4 ya bidhaa zinazotoka nchi za nje na
huduma |
| Weka mahesabu katika hali ya usawa (ongezeko la matumizi liwe dogo) |
| Panua wigo wa kodi (na zuia ukwepaji wa ulipaji kodi) |
| Imarisha utawala wa mfumo wa kodi |
| Endeleza uwezo wa mameneja wa Fedha katika ngazi ya Taifa na mitaa |
Viashirio (Dalili)
| Ukuaji wa jumla wa uchumi wa Tanzania |
| Kiasi cha upandaji wa gharama za maisha |
| Jumla ya rasilimali ya akiba ya kimataifa |
| Mabadiliko katika kima cha mabadilishano ya fedha |
| Sazo la fedha katika uchumi |
| Ugawaji wa rasilimali – ugawaji halisi wa fedha kwa ajili ya elimu, afya ya jamii,
maji, barabara za vijiji, kilimo na uzuiaji wa kuenea kwa Virusi vya UKIMWI/UKIMWI |
Matendo yafuatayo ambayo baadhi yameelezwa katika sehemu zilizotangulia katika kijitabu
hiki yatawezesha kuwa na hali imara ya uchumi
Viashirio (Dalili) |
Matendo |
Ukuaji wa jumla wa Uchumi wa Tanzania |
Imarisha uthabiti wa uchumi |
Panua vitega uchumi (vya asili na vya binadamu) |
| Imarisha barabara vijijini na huduma za miundo msingi (maji, umeme, mawasiliano n.k.) |
| Elimisha watu katika stadi zinazotakiwa na katika kazi na utoaji ushauri |
|
Imarisha vitega uchumi vya uzalishaji |
| Endeleza nyenzo za uchumi mdogo |
| Stawisha hali nzuri ya vitega uchumi ambayo inaendana na programu
| kukuza sekta binafsi na thabiti |
| kupunguza gharama za uendeshaji biashara |
| kuunda mfumo wa sheria ambao ni thabiti na unaofaa |
|
|
Endeleza Mbinu za Sekta Binafsi ifikapo mwaka 2003 |
| Hakikisha uratibu mzuri kati ya serikali na mashirika ya wafadhili |
| Hakikisha kuunda mazingira yanayowezesha biashara kubwa, ndogo na ya kati. Aidha kuwa na
biashara isiyo rasmi |
| Ulipaji kodi – viwango na viwango vilivyo dhibitiwa |
|
Ukuaji wa kilimo kwa asilimia 5 ifikapo 2003 |
| Endeleza upatikanaji wa matokeo ya tafiti za kilimo |
| Rahisisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kilimo |
| Kuza upatikanaji wa fedha za maendeleo vijijini, na biashara ya mazao na futa urasimi |
| Kuza biashara ya nje ya bidhaa za kilimo · |
| Gawa ardhi ambayo inafaa kwa umwagiliaji kwa watu masikini |
|
Uimarishaji wa barabara za vijijini |
| Ongeza mgao wa bajeti kwa ajili ya ukarabati na uimarishaji wa barabara za vijijini |
| Endeleza na tumia teknolojia ya nguvukazi kwa ajili ya ukarabati na uimarishaji, na
tumia makandarasi wa nchini |
| Imarisha uwezo wa kudhibiti ukarabati wa barabara ambazo zinajengwa na makandarasi |
|
Kuza ubora wa maisha na Ustawi wa Jamii
Umasikini wa kutokuwa na mapato unatokana na elimu ndogo, afya mbaya na ustawi wa jamii
ambao ni wa mashaka. Kwa ujumla, inaonekana wazi lipi linahitaji kutendwa bali itachukua
muda kugundua vipengele vyote vinavyohitajiwa. Aidha itachukua muda pia kujua gharama
inayotakiwa. Mipango ifuatayo imekwisha buniwa:-
Mpango wa Taifa wa Mbinu za uendelezaji Elimu ya Msingi |
Ifikapo Julai 2001 |
Mpango wa Taifa wa Mbinu za uendelezaji Kilimo |
Ifikapo Juni 2001 |
Mpango wa Taifa wa Mbinu za uendelezaji Vijiji |
Ifikapo Desemba 2001 |
Programu ya mageuzi ya Serikali za Mitaa imekwishaanza kutekelezwa katika wilaya zote.
Hii inasaidia Serikali za Mitaa kutekeleza huduma muhimu.
Mipango hii itaruhusu:
| Majengo chakavu na huduma dhaifu kurekebishwa (Serikali za Mitaa zitaamua mahali pa
kujenga majengo mapya) |
| Misaada mbalimbali ipatikanayo toka kwa wafadhili na hivyo kuwa nje ya bajeti (serikali
itafanya kazi ya uratibu na wafadhili) |
| Upunguzaji wa umasikini utagharimu pesa nyingi zaidi kuliko ilivyo sasa (serikali
itashughulikia upatikanaji zaidi wa fedha) |
Elimu
Shabaha kuu ni kuwa na elimu zaidi na bora zaidi. Hii itajumuisha ufutaji wa ujinga
ifikapo mwaka 2010. Aidha inakusudia kuleta uwiano sawa kati ya wasichana na wavulana
katika shule za msingi na sekondari ifikapo mwaka 2005.
Malengo
|
Hadi kufikia 2003 |
Uandikishaji wa wanafunzi shuleni kijumla |
Hadi kufikia 85% |
Kiwango cha wanaoacha shule |
Toka 6.6% hadi 3% |
Uandikishaji wa wanafunzi kihalisi |
Toka 57% hadi 70% |
Wanafunzi wanaoshinda mtihani wa darasa la 7 |
Toka 20% hadi 50% |
Wanafunzi wanaoingia sekondari |
Toka 15% hadi 21% |
Mipango ya Elimu ya Watu Wazima |
Iongezeke |
Shughuli
| Upimaji wa mshule na uendelezaji wa mipango utafanywa |
| Serikali itagharimia gharama za muhimu za shule za msingi (hasa mishahara ya walimu) |
| Ada za shule zitafutwa ifikapo Julai 2001 |
| Shule zitaendelezwa kwa kupatiwa vitabu, vifaa, madawati, vyoo, vyumba vya madarasa,
nyumba za walimu, n.k. |
| Uwiano thabiti kati ya wanafunzi – walimu utatumiwa |
| Walimu wataendelezwa na kuhamasishwa |
| Kitengo cha ukaguzi kitaimarishwa |
| Shule binafsi na elimu ya jumuiya (ikiwa pamoja na elimu ya watu wazima) itaimarishwa. |
Viashirio (dalili)
| Ongezeko halisi la kiwango cha uandikishaji wanafunzi katika elimu ya msingi |
| Ongezeko halisi la wanafunzi wanaoanza shule |
| Ongezeko halisi la wanafunzi wanaosoma darasa la saba |
| Ongezeko halisi la wanaoshinda mtihani wa darasa la saba |
|
“Mwanadamu anakuwa mwanadamu kwa sababu ya wanadamu wengine”
[Methali ya Kiafrika]
|
|
Afya
Umri wa kuishi unapungua (hasa kwa sababu ya ugonjwa wa UKIMWI). Lengo ni kuongeza umri
hadi kufikia miaka 52 ifikapo 2010. Hili litawezekana kwa kuboresha lishe na kuwa na
huduma bora za afya pamoja na maji salama.
Malengo
|
Ifikapo mwaka 2003 |
Kiwango cha vifo vya watoto wachanga |
Toka 99 hadi 85 kwa kila watoto 1000 |
Chini ya umri wa miaka 5 |
Toka 158 hadi 127 kwa kila watoto 1000 |
Vifo vya akina mama wakati wa kujifungua |
Toka 529 hadi 450 kwa kila watoto 1000 |
Vifo kutokana na malaria kwa watoto chini ya miaka 5 |
Toka 12.8 hadi 10 % |
Watu wanaopata maji salama |
Toka 48.5 hadi 55% |
Uchanjwaji wa watoto chini ya miaka 2 dhidi ya surua, dondakoo
na pepopunda |
Toka 71 hadi 85% |
Wilaya ambazo zina kampeni dhidi ya UKIMWI |
Hadi kufikia 75% |
Punguza hali ya kudumaa |
Toka 43.4 hadi 20% |
Punguza upotevu |
Toka 7.2 hadi 2% |
Wafanyakazi wenye taaluma ya uzazi |
Toka 50 hadi 80% |
Tekeleza kikamilifu sera ya maji ya mwaka 2000 kama
inavyotakiwa |
|
Shughuli
| Ongeza kiwango na imarisha ugawaji wa fedha za serikali kwa ajili ya afya ya jamii |
| Toa afya bora karibu na mahali wanapoishi watu wote wa mijini na vijijini |
| Hakikisha misaada inatolewa kwa afya za jamii kwa kuimarisha vituo vya afya na hospitali
na kubadili mfumo wa utendaji wa kazi |
| Imarisha mfumo wa kutoa misaada kwa wafanyakazi, madawa na vifaa vingine vya afya |
| Tekeleza programu ya udhibiti wa malaria kama ilivyopangwa kati ya mwaka 2000/01 hadi
2002/03 |
| Kuza sekta binafsi na shirikisha makundi ya jumuiya katika utoaji wa huduma za afya |
VIRUSI VYA UKIMWI/UKIMWI
Kuza utambuzi wa ugonjwa wa UKIMWI na afya ya jamii – pamoja na
wanafunzi kufundishwa mashuleni |
“Uchungu na huzuni huja kwa kuangalia uwapendao wakifa kwa sababu ya
kukosa fedha za matibabu na hali hii ni upeo wa juu wa matatizo ya umasikini unaokuja
kimya kimya”
[Deepa Narayan] |
|
Lishe
Kuza elimu ya lishe, hasa kwa akina mama na imarisha afya ya uzazi na mpango wa uzazi
Anzisha programu ya mfuko wa fedha wa shule
Maji
| Ongeza matumizi ya serikali katika huduma za maji vijijini |
| Tathmini mahitaji ya makundi tofauti ya watu vijijini |
| Imarisha vianzo vya maji na data za maji salama |
| Fanya ukaguzi wa upimaji maji |
| Fanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ubora wa huduma za maji na tumia vipimo vya shirika la
Afya Duniani (WHO) |
| Kuza uvunaji maji ya mvua |
| Karabati mipango yote ya usambazaji maji ambayo haifanyi kazi. Aidha karabati vifaa vya
kutoboa udongo |
| Imarisha sheria, kanuni na taratibu za kuhifadhi maji katika vyanzo vya maji |
| Zipe uwezo Serikali za Mitaa na jumuiya kulinda vyanzo vya maji |
Viashirio (Dalili)
| Watoto wachanga na viwango vya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano |
| Asilimia ya watoto ambao wamepata chanjo kamili baada ya mwaka mmoja |
| Uwiano wa wilaya zenye kampeni za utambuzi wa UKIMWI |
|
“Afya inahusisha mwili mzima, akili, na ustawi wa jamii na si tu
kutokuwa mgojwa na kutojiweza.”
[Shirika la Afya Duniani – WHO]
|
|
| Uwiano wa kaya ambazo zinapata maji salama |
Ustawi wa Jamii – Kushiriki katika shughuli za Siasa
Kati ya vitu vingine ambavyo vinahusiana na ustawi wa jamii ni kuhusu kushiriki katika
maamuzi ya kisiasa yanayohusu maisha yako, na kujiona wanalindwa na sheria na kanuni.
Pametokea maendeleo mazuri katika eneo hili katika miaka mitatu iliyopita na mengi
yanapangwa.
Serikali imekuwa wazi katika shughuli inazofanya na imekuwa sikivu kwa watu wa kawaida.
| Watu wa kawaida sasa wanaweza kujua serikali inatumiaje fedha zao na kushiriki katika
mikutano inayoamua sera zipi zifuatwe na serikali |
| Magazeti, Redio, Televisheni vinaeleza watu wa kawaida mambo yanayoendelea |
| Kuna Jumuiya hiari za Wananchi ambazo hutoa mchango na changamoto |
| Serikali za Mitaa zitapewa uwezo zaidi wa kuamua yapi yatekelezwe katika mikoa yao baada
ya kutekeleza Programu ya Mageuzi ya Serikali za Mitaa. |
Linapozingatiwa suala la sheria na taratibu, watu lazima wajione salama kutembea
mitaani, kuweza kutumia mahakama, na kujua kuwa mfumo wa serikali ni thabiti, wa haki na
uko wazi. Mipango ifuatayo inafanywa katika kiwango cha Serikali za Mitaa:
Malengo
| Tekeleza kikamilifu njia za Kupunguza Umasikini kama zilivyopangwa |
| Tekeleza kikamilifu Programu ya Mageuzi ya Serikali za Mitaa ifikapo mwaka 2003 katika
wilaya zote |
| Hakikisha ushirikishwaji wa washika dau wote katika kuunda, kutekeleza na kutathmini
mipango yote ya maendeleo |
Shughuli
| Kuza mfumo wa usalama wa jamii |
| Karabati majengo ya mahakama za mwanzo na vifaa vya jumuiya |
| Ajiri mahakimu ili kesi zilizoko katika mahakama za Mwanzo ziweze kuamuliwa mapema |
Katika Kiwango cha Taifa:
|
Hadi mwisho wa mwaka 2003 |
Uwiano wa vikao vilivyopangwa vya Mahakama za Rufaa na vile vilivyotimizwa |
Toka 50% hadi 100% |
Uamuzi wa Mahakama |
Uharakishwe |
Uwiano wa kesi zilizoamuliwa na zile zilizoletwa |
Toka 63% hadi 80% |
Wastani wa muda uliotumiwa katika kuamua kesi za biashara |
Zipunguzwe hadi miezi 18 |
Kutakuwa pia na uchunguzi wa rushwa katika :
| Wizara ya Sheria |
| Wizara ya Ujenzi, Elimu, Afya na Mambo ya Ndani na ofisi zao za Mikoani na Wilayani |
| Ofisi ya Mwanasheria Mkuu |
| Mamlaka ya Mapato Tanzania |
Viashirio (Dalili)
Viashirio vya ushirikishwaji:
| Idadi ya washiriki na ushiriki katika warsha za mashauriano |
| Ushiriki wa makundi ya jumuiya |
| Usambazaji wa ripoti za serikali |
Ripoti za kila miezi minne kuhusu maendeleo ya mageuzi ya mfumo wa mahakama na
uchunguzi wa rushwa.
Kupunguza Madhara katika Makundi Masikini
Serikali za Mitaa zitaombwa kupambanua makundi ambayo yamo hatarini kupata
madhara zaidi na ziamue matakwa yao ni yapi na yanaweza kupatikanaje. Baadhi ya majukumu
ya kutekeleza ili kusaidia makundi haya ni:
|
Programu za kazi za kulipwa chakula
|
|
Miradi maalum inayohusisha yatima na walemavu
|
|
Mfumo wa awali wa kugundua mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri
mazao
|
|
Kutekeleza mpango wa umwagiliaji katika sehemu zenye ukame
|
|
Kuweza kufika kwa urahisi katika mikoa yenye ziada ya chakula
|
|
Kuendeleza mazao yanayohimili ukame
|
|
Kuendeleza misitu
|
Benki ya Dunia imetoa mkopo kwa ajili ya mradi wa mfuko wa Kuinua Jamii
Tanzania (TASAF) katika ngazi ya wilaya.
Watu wengi masikini Tanzania wanategemea mazingira asilia kwa ajili ya
chakula chao na pia kukabili mahitaji yao kwa kuuza kuni, mkaa, asali na matunda mwitu.
Hatujui shughuli hizi kikamilifu kiasi cha kupunguza na kuweka malengo kwa ajili ya kuzuia
uharibifu wa mazingira. Taarifa zitakusanywa ili zitumike katika nakala mpya ya mpango wa
kusaidia Kupunguza Umasikini (PRSP).
Utaratibu utafanywa wa kuhusisha
mipango mingine kama vile kuimarisha matumizi ya mazao yanayostahimili ukame na mpango wa
umwagiliaji unaofanywa na jamii. Aidha upandaji miti na upunguzaji wa mifugo nao pia
utahusishwa.
|
“Mpangilio wa maisha unaonyesha kuwa watu masikini ambao wana mali
kidogo wanaweza kwa kutumia nguvu kidogo kuneemeka polepole kiuchumi, na kushtukia
wamerejea tena katika ufukara wao kwa sababu ya maradhi, kuachishwa kazi, kupata mazao
hafifu na wanawake kutelekezwa . Hakuna kitu kinachowazuia kuangukia katika lindi la
kukata tamaa. Na wakati wanapotumbukia huko, panaweza pasiwe na mtu yeyote anayewangoja
kuwadaka huko chini wanakoangukia. Aidha hakuna anayewapa mkono wa msaada ili waanze
upya.”
[Deepa Narayan]
|
|
Malengo
Jenga uwezo wa jumuiya zote zinazohitaji programu za usalama.
Shughuli
|
Kuza programu za jumuiya za kusaidia watu ambao wanakabiliwa na matatizo
mbalimbali
|
|
Unda mfuko wa kuleta usawa ili kusaidia sehemu zilizo nyuma
|
|
“Tunamsaidia
mwanachama yeyote wa kundi letu anapopata matatizo; tunamliwaza yeyote yule anayepata
matatizo”
[Kundi la akina mama, Tabora]
|
|
Viashirio (dalili)
Namba ya data za uchumi zinazoonyesha makundi ya watu wenye matatizo
zilizoundwa katika ngazi za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.
Tutagharamiaje Upunguzaji wa Umasikini?
Hatuna hakika tunahitaji fedha kiasi gani na kiasi gani cha fedha kitakuwepo katika
siku zijazo. Hata hivyo ni wazi kuwa hatutakuwa na fedha za kutosha na zile ndogo
tulizonazo itabidi tuzitumie kwa uangalifu mkubwa.
Hatutaweza kujua kwa hakika ni fedha kiasi gani zitapatikana hasa kwa ajili ya
kupunguza umasikini mpaka mipango yote mingine iwe imekamilika.
Njia za Mapato kwa ajili ya Upunguzaji Umaskini
| Kiasi fulani cha fedha kitatokana na bajeti ya Serikali lakini hatutaweza kujua kiasi
cha fedha kitakavyokuwa hadi mfumo wa kodi utakapoboreshwa. · |
| Kiasi cha fedha kitatoka kwa wafadhili, lakini kiasi hicho hakiwezi kujulikana katika
muda mfupi na muda mrefu · |
| Serikali itatumia fedha zake kupata fedha zaidi kwa kutoa mikopo na michango kwa watu wa
kawaida na wafanyabiashara ambao wana mawazo mazuri na miradi mizuri · |
| Serikali inaweza kukopa fedha kuziba pengo |
Kwa kuzingatia hali hii ya mashaka, na umuhimu wa kuwa na uchumi thabiti, matarajio
yaliyowekwa kwa miaka mitatu ijayo ni kuwa jumla ya bajeti ya matumizi itaongezeka toka
asilimia 15.5 hadi 17-18% ya mapato yote ya serikali. Kati ya fedha hizo asilimia 70%
itatoka serikalini na asilimia 30% itatoka kwa wafadhili kama misaada au mikopo. Kama
Mageuzi ya Serikali yatafaulu basi Tanzania itatimiza masharti ya mpango nafuu yaliyowekwa
kwa ajili ya nchi zenye madeni makubwa (HIPC) hadi kufikia katikati ya mwaka 2001.
Shughuli nyingi za upunguzaji wa umasikini zitafanywa na Serikali za Mitaa. Ufafanuzi
wa shughuli hizi utafanywa katika Programu ya Mageuzi ya Serikali za Mitaa (LGRP)
yanayoendelea.
Kipaumbele katika Matumizi
Katika majibu ya watu waliyotoa wakati wa kutayarisha Mkakati wa Kupunguza Umasikini
(PRSP), serikali imeamua kuwa matendo muhimu katika upunguzaji wa umasikini yanapaswa
kuwa; matengenezo na uimarishaji wa huduma za sekta muhimu na sehemu inyohusika. Matendo
hayo ni kama yafuatayo:
|
Shilingi Milioni
|
|
Elimu ( Elimu ya Msingi) |
|
Afya (Afya ya Msingi kwa Jamii) 65970 42314 Barabara (Vijijini) |
|
Barabara (Vijijini) |
|
Mfumo wa Mahakama |
|
Kilimo (Utafiti na huduma) |
|
Maji |
|
VIRUSI VYA UKIMWI/UKIMWI |
|
Upunguzaji wa Umasikini: Vipengele Muhimu vya Ziada
Ufutaji wa ada za Shule \
Serikali itaacha kutoza ada za shule ifikapo Julai 2001. Hii ni kwa sababu serikali
inaamini kwamba kwa kutolipa ada watoto wengi watasoma hasa watokao katika familia
masikini
Kuhimiza michango kutoka katika Jumuiya na Washika dau wengine
Jumuiya zimeshiriki kikamilifu daima katika kupunguza umasikini kwa kufanya kazi za
kujitolea kama kujenga madarasa, vituo vya afya, maji, barabara za vijijini, n.k. Serikali
itahimiza moyo huu kwa kuchangia gharama za miradi hii na kuwahamasisha wafadhili kufanya
hivyo hivyo.
Mafunzo ya Kazi
Serikali inakusudia kutumia karibu shilingi milioni 100 kila mwaka ili kuwasaidia watu
waweze kujifunza mambo yatakayowasaidia kupata kazi. Fedha hizi zitawalenga watu ambao
hasa ni masikini zaidi.
Mipango Imebuniwaje?
Tangu wakati wa uhuru mwaka 1961 serikali imejitahidi kushughulikia tatizo
la ujinga, maradhi na umasikini. Kumepatikana maendeleo kwa kutumia mipango ya serikali
kuu hadi mwaka 1970 ambapo hali ya kimataifa na kitaifa ilidhoofisha juhudi hizo na
kuzirudisha nyuma. Licha ya mageuzi ya kiuchumi na |
“Ni vigumu kwa
watu wa kawaida kuitikia kwa moyo mkunjufu kwenye wito wa kazi za maendeleo ambazo
zinaweza kuwa ni za manufaa kwao, lakini ambazo zimeamuliwa na kupangwa na mamlaka ambayo
iko mbali mno nao.”
[Mwalimu Julius K. Nyerere]
|
|
kisiasa tangu katikati ya mwaka 1980, nusu ya Watanzania wote wanahofiwa kuwa masikini
na theluthi wanaishi katika ufukara mkubwa.
Lakini hali sasa inaweza kuwa inabadilika. Mwishoni mwa miaka ya 1990 serikali ilitoa
mwelekeo wa 2025 ukionyesha malengo ya muda mrefu ya kiuchumi na kijamii. Haya yalifuatwa
na Mbinu za Kitaifa za Ufutaji wa Umasikini (NPER) ambapo malengo ya ufutaji wa umasikini
hadi mwaka 2010 yalifafanuliwa. Jumuiya ya Kimataifa iliiunga mkono serikali kwa kutoa
Mbinu za Usaidizi wa Tanzania (TAS) ambapo ilieleza kwa muhtasari mbinu iliyoratibiwa
katika utoaji wa misaada. Tangu wakati huo muundo wa matumizi ya kati (MTEF) na mapitio ya
matumizi ya serikali (PER) vimetolewa. Aidha, orodha ya tathmini ya viashirio vya ustawi
na umasikini (PM) imetengenezwa.
Sasa tuna waraka wa Mkakati wa Upunguzaji wa Umasikini Tanzania (PRSP). Hii inaeleza
mbinu za muda mfupi wa kupunguza umasikini na ni sehemu ya mpango wa Nchi Masikini zenye
Madeni Makubwa (HIPC). Mbinu hii in maana kwamba serikali inapaswa kupunguza matumizi na
huku ikiruhusu shughuli za matumizi ya kuondoa umasikini kwa bajeti ya ziada na kukuza
hatua mbalimbali zisizo ingiza gharama ambazo zaweza kuondoa umasikini.
Watu wengi walihusika katika kuandaa Mkakati wa Kupunguza Umasikini
Tanzania (PRSP) na watu watahusika katika utekelezaji wake. Mpango unaorodhesha sababu
zinazowafanya watu wawe masikini na kutoa mapendekezo ya njia za kuuondoa umasikini huo. |
“Kama watu elfu moja watapiga risasi wakilenga shabaha moja tu na kwa
wakati mmoja, hakuna sehemu ya shabaha ambayo haitapigwa.”
[Methali ya Kichina]
|
|
Baadhi ya ufumbuzi huihusisha serikali na mashirika ya wafadhili na ufumbuzi mwingine
huwahusisha watu wa kawaida.
Watu hawaendelezwi ila wanajiendeleza wenyewe. [Mwl. Julius K. Nyerere] |
Mpango wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania (PRSP) ni tofauti na mipango ya awali
kwa sababu unatoa malengo thabiti na unawashirikisha watu wa kawaida. Watu wa kawaida
walihusishwa katika kutengeneza mpango huo na watahusishwa katika kuutekeleza. Na hasa
lililo muhimu ni kuwa watahusishwa katika kuhakikisha kwamba malengo yaliyobainishwa
katika mpango huo yanapatikana.
Mpango huu Uliandaliwaje?
Mwezi Oktoba 1999 kamati ya mawaziri kumi na wawili na Gavana wa Benki ya Tanzania
iliundwa kuandaa waraka wa mpango wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini (PRSP). Kamati hii
ilisaidiwa na kamati ya wataalamu (iliratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais) ambayo
iliwahusisha maofisa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Tume ya Mipango, Wizara Kuu na Benki Kuu
ya Tanzania.
Waraka wa msingi (waraka wa awali) wa Mpango wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania
(PRSP)) ulitolewa kama muswada wa kwanza mwanzoni mwa mwezi Januari 2000. Waraka huu
ulijadiliwa katika mkutano wa mashauriano ambao uliwahusisha wawakilishi wa serikali na
watu waliotoka katika jumuiya ya wafadhili na makundi ya kijamii.
Waraka ulihakikiwa na kuidhinishwa na baraza la mawaziri mwanzoni mwa mwezi Februari
2000. Aidha, waraka huo ulijadiliwa na Shirika la Fedha Duniani mjini Washington mwezi
Machi 2000. Hili liliiwezesha Tanzania kuendelea na kutoa waraka kamili wa Mbinu za
Kupunguza Umasikini.
Mwezi Machi mwaka 2000 kamati ya wataalamu ilitayarisha vidokezo vya waraka wa mwanzo
kwa ajili waraka kamili wa mpango wa Mkakati za Kupunguza Umasikini Tanzania (PRSP).
Waraka huu ulijadiliwa katika warsha za kanda saba kati ya tarehe 11-12 Mei 2000. Warsha
hizi zilihudhuriwa na washiriki 804 na zilihusisha vijiji 426, madiwani 215, Wakurugenzi
wa Halmashauri 110 na watu 53 waliotoka katika mashirika yasiyo ya kiserikali. Chini ya
robo ya washiriki walikuwa wanawake. Ripoti za kila kanda zilitolewa kwa kamati ya
wataalamu tarehe 16 Mei 2000.
Mkutano wa mashauriano kati ya serikali na wafadhili uliofanywa tarehe 22 Mei 2000 na
ulifuatwa na kamati ya wataalamu ambayo ilitengeneza waraka wa mwanzo wa Mbinu za
Upunguzaji wa Umasikini Tanzania. Waraka huu ulitumia taarifa zilizotoka katika tafiti
zilizotangulia, waraka za sera na matokeo ya warsha za kanda. Tarehe 30 Juni waraka
ulijadiliwa katika mkutano ambao uliwashirikisha jumuia ya wafadhili kutoka Benki ya Dunia
na Shirika la Fedha Duniani. Tarehe 1 Julai 2000 Wabunge walijulishwa juu ya maendeleo
yaliyokwisha fikiwa na waliombwa kutoa mawazo yao.
Tarehe 3-4 Agosti 2000 kulifanyika warsha ya kitaifa ikiwa na washiriki 25 ili kupata
maoni zaidi kuhusu malengo, na kutathmini mambo muhimu ya kufanya ambayo yalikuwa
yameainishwa katika waraka wa awali. Waliohudhuria warsha hiyo ni pamoja na Makatibu
Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wawakilishi na Wafadhili, Mashirika ya Kimataifa, sekta binafsi,
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, vyombo vya habari na wawakilishi wa sekta zisizokuwa
rasmi. Aidha tarehe 3 - 4 Agosti 2000 waraka wa awali ulijadiliwa na Makatibu Tawala wa
Mikoa (RAS) huko Lobo, Serengeti.
Waraka uliorekebishwa uliidhinishwa na Baraza la Mawaziri tarehe 31 Agosti 2000.
Marekebisho zaidi yalifanywa na Serikali na Shirika la Fedha Duniani/Benki ya Dunia na
Waraka wa mwisho uliidhinishwa na Bodi za Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia mwezi
Oktoba 2000.
Mipango ya baadaye itafanywaje?
Tafiti mbalimbali zinafanywa ili kupata takwimu bora za kusaidia mipango ya baadaye.
Hizi ni pamoja na: · Ukaguzi mpya wa bajeti za kaya zaidi ya 24,000 · Ukaguzi wa nguvu
kazi ili kuanzisha msingi wa soko la kazi · Sensa ya idadi ya watu na nyumba katika mwaka
2002 · Ukaguzi wa taarifa za uzazi na vifo pamoja na afya katika mwaka 2003
Shirika la Fedha Duniani/Benki ya Dunia inashauri kutengenezwa upya kwa
mahesabu ya kijamii ili kupima kama mapato na matendo ya sera yana matokeo yoyote juu ya
upunguzaji umasikini |
“Watu masikini ndio wataalamu wa umasikini”
[Deepa Narayan]
|
|
Kuna umuhimu wa haraka wa kuimarisha uwezo wa watu wa aina mbalimbali ili kutathmini
shughuli ambazo zimeanzishwa pamoja na waraka wa Mkakati wa Upunguzaji wa Umasikini
Tanzania (PRSP). Watu wanahitaji pia kufasili taarifa ambazo zinakusanywa na kubainishwa,
taarifa hizo zina maana gani katika masuala ya sera.
Inategemewa kuwa vikao mbalimbali vitafanywa ili kuanzisha utaratibu wa uoanishaji wa
shughuli mbalimbali katika ngazi tofauti. Aidha vikao hivi vitatafuta njia za kuhusisha
sera na ushirikishwaji wa watu. Kama ilivyoelezwa katika Mkakati wa Upunguzaji wa
Umasikini Tanzania (PRSP), “Serikali imekusudia kuendeleza ushirikishaji wa watu
masikini na washika dau wengine katika utekelezaji, usimamizi na tathmini ya mbinu za
upunguzaji umasikini, na kisha kurekebisha waraka huo”.
Maana za Baadhi ya Maneno
Uchumi Mkuu: (macroeconomics) ni elimu juu ya picha kamili ya uchumi,
yaani njia ambayo utajiri unapatikana na unagawanywa. Inaweza kuwa elimu kuhusu nchi
maalum au dunia nzima na jinsi tofauti zinavyoingizwa katika picha nzima ya dunia. Kuna
majadiliano kama ya:
| Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kuwa masikini zaidi. Tufanye nini
kuhusu jambo hili? |
| Serikali ijiingize kiasi gani katika uendeshaji wa soko huru? |
| Kwa kuzingatia na uharibifu wa mazingira, je, ukuaji wa uchumi usiodhibitiwa unatakiwa? |
Uchumi Mkuu Imara (Macroeconomic Stability) ni matokeo ya kuwa na kodi
ya hazina, sera za fedha na kiwango cha kubadilishana fedha inayokusudia kufikia malengo
ya uchumi mkuu kama vile ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, madeni ya nje na
akiba halisi ya kimataifa.
Uchumi Mdogo (Microeconomics) ni elimu kuhusu jinsi viwanda, sekta
fulani, biashara au kaya zinavyofanya kazi.
Jumla ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product - GDP) ni kipimo cha
jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana nchini katika muda maalum. Kwa maneno mengine
Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa
fedha. Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1% zaidi kuliko ya
mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1%. Lakini jumla ya pato la taifa
(GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa – kwa mfano,
uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga
nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi
yao.
Jumla ya Pato la Taifa (GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini
unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.
Ukuaji Halisi (Real Growth): Kwa vipengele vyote viwili jumla ya pato
la utajiri (GDP) na ukuaji wa pato la utajiri (GNP), kama ukuaji ni asilimia 7% kwa mwaka,
lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5% basi Ukuaji Halisi ungekuwa asilimia 2% tu kwa
mwaka.
Mfumuko wa Bei (Inflation): Kipimo cha kupanda kwa bei kati ya mwaka
mmoja na mwaka unaofuata – hasa ukizingatia wazo la kupata vifaa vya madukani/sokoni.
Mtaji wa jamii (Social Capital) ni kama “gundi”
inayounganisha pamoja familia, makundi na jumuiya. Inahusisha imani, desturi na tabia za
jamii ambazo husaidia kufanya kazi pamoja kwa uthabiti katika makundi yaliyo rasmi na
yasiyo rasmi.
Vyama vya Jumuiya (Civil Society Organisation):Inahusisha vyama rasmi
ambavyo vimesajiliwa na serikali na vile visivyo rasmi. Vyama hivyo ni pamoja na vile vya
hisani, dini, vya shughuli maalumu, kundi shawishi, kitaaluma, na vyama vya makundi
maalumu kama vile vyama vya wafanyakazi na vyama vya wanafunzi. Vyama visivyo rasmi ni
pamoja na Upatu, vyama vya makabila, mpira wa miguu ambavyo vinaundwa na vijana wa kiume
na netiboli vinavyoundwa na vijana wa kike.
Matayarisho Ya Bajeti inayozingatia maskini (Pro-poor Budgeting): na
usimamizi wa matumizi (and expenditure monitoring). Fedha zinatengwa katika bajeti kwa
ajili ya programu zinazowalenga watu masikini. Lakini fedha hizi zinapaswa kupitia Hazina,
wizara inayohusika, serikali za Mikoa na Halmashauri za Wilaya/ Miji na kitengo cha huduma
(k.m. shule au hospitali) kabla ya mtu masikini kupata faida. Kwa usimamizi thabiti fedha
hizi zinaweza kutumika vizuri.
Mapitio ya Matumizi ya Serikali (Public Expenditure Review). Timu ya
Matumizi ya Serikali hukutana mara moja kila baada ya majuma mawili ili kutafakari jinsi
serikali inavyopata na kutumia fedha zilizo kwenye bajeti. Timu hii iliundwa mwaka 1997
inawajumuisha viongozi wakuu wa serikali na wawakilishi kutoka katika jumuiya ya
wafanyabiashara, makundi ya jumuiya na makundi ya wafadhili wa nje.
Bajeti za Serikali (Government Budgets). Serikali ni kama familia
ambayo inapaswa kuweka uwiano kati ya fedha zinazoingia na fedha zitumikazo. Kama hakuna
fedha zinazoingia serikali inapaswa kuamua itumie kiasi gani na isitumie kiasi gani.
Utaratibu wa kukusanya taarifa hii na kufanya uamuzi ndiyo huitwa Bajeti
Njia za Mapato ya Serikali (Source of government income):
| Kodi ya moja kwa moja k.m. kodi ya mapato, kodi ya mali |
| Kodi isiyo ya moja kwa moja k.m. kodi ya ushuru wa forodha, kodi ya mauzo |
| Mapato yasiyo na kodi k.m. liseni na ada |
| Mikopo k.m. toka Mashirika ya Fedha Duniani na Benki ya Dunia · |
| Misaada k.m. toka serikali nyinginezo na toka mashirika yasiyo ya kiserikali |
Kuongeza kodi ni jambo lisilopendwa na baadhi ya kodi nyingine ni mzigo mkubwa kwa watu
masikini kuliko watu matajiri. Mikopo ni mizuri kuziba mapengo ya muda mfupi na kuanzisha
biashara mpya, lakini lazima mikopo hiyo ilipwe. Misaada inakaribishwa bali hatuwezi
kupata misaada wakati wote.
Mishahara na Gharama Nyinginezo (Personal Emoluments (PE) and other
charges (OC)): Wizara inatumia sehemu ya bajeti yake kwa mishahara na sehemu nyingine
kulipia gharama nyinginezo. Kama sehemu ya kutekeleza waraka wa Upunguzaji wa Umasikini
(PRSP), Serikali itaongeza bajeti ambayo inatengwa kwa ajili ya gharama za matumizi
mengine – kwa mfano, kati ya mwaka 1999/2000 hadi 2002/2003 bajeti itaongezwa toka
asilimia 2 hadi 3.8% kwa ajili ya elimu ya msingi na toka asilimia 2.1 hadi 3.8% kwa ajili
ya Afya ya Jamii.
Vifupisho
-
BoT Bank of Tanzania – Benki Kuu (ya Tanzania)
-
CAS Country Assistance Strategy – Mbinu za Kusaidia Nchi
-
CSO Civil Society Organisation – Jumuiya Hiari za Wananchi
-
DED District Executive Director – Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
-
ELCT Evangelical Lutheran Church of Tanzania – Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania
-
ESAF Enhanced Structural Adjustment Facility – Uharakishaji
Mabadiliko ya Kimuundo
-
GDP Gross Domestic Product – Pato Ghafi la Ndani
-
GNP Gross Nationa Product – Jumla ya Pato la Taifa
-
HBS Household Budget Survey (1991/92) – Mapitio ya Bajeti za Kaya
(1991/92)
-
HIPC Highly Indebted Poor Countries – Nchi Masikini zenye Madeni
Makubwa
-
HRDS Human Resource Development Survey (1993) – Ukaguzi wa Maendeleo
ya Nguvu kazi (1993)
-
HRS Human Resource Survey (1983) – Ukaguzi wa Nguvu kazi
-
IBRD International Bank for Reconstruction and Development (World Bank)
– Benki ya Dunia ya Urekebishaji na Maendeleo
-
IFMS Integrated Financial Management Information System – Mfumo wa
Pamoja wa Taarifa za Uendeshaji wa Fedha
-
IMCI Integrated Management of Childhood Illness – Uendeshaji wa
Pamoja wa Magonjwa ya Watoto
-
IMF International Monetary Fund – Shirika la Mfuko wa Fedha Duniani
-
LGRP Local Government Reform Programme – Mpango wa Mageuzi wa
Serikali za Mitaa
-
M & E Monitoring and Evaluation – Usimamizi na Tathmini
-
MDF Multilateral Development Fund – Mfuko wa Shughuli mbali mbali za
Maendeleo
-
MSME Micro, Small and Medium Enterprises – Viwanda Vidogo na vya
Kati
-
MTEF Medium-term Expenditure Framework - Muundo wa Matumizi ya Muda wa
Kati
-
NBS National Bureau Statistics – Kitengo cha Taifa cha Takwimu
-
NGO Non-Government Organisation – Shirika lisilo la Kiserikali
-
NPES National Poverty Eradication Strategy – Mpango wa Taifa wa
Mkakati waKupunguza Umasikini
-
OPM Oxford Policy Management – Manejimenti ya Oxford kuhusuSera ya
Uongozi
-
PER Public Expenditure Review – Mapitio ya Matumizi ya Serikali
-
PL Poverty Line – Mstari wa Umasikini
-
PMI Poverty and Welfare Monitoring Indicators – Viashirio vya
Uratibishaji wa Umasikini na Usawa
-
PPA Participatory Povery Assessment (1995) – Tathmini ya
Ushirikishwaji juu ya Umasikini
-
PRGF Poverty Reduction and Growth Facility – Mfumo wa Ukuaji na
Upunguaji wa Umasikini
-
PRSC Poverty Reduction Support Credit – Mikopo ya Kusaidia Kupunguza
Umasikini
-
PRSP Poverty Reduction Strategy Paper – Mkakati wa Mbinu za
Upunguzaji Umasikini
-
PSAC-I Programme Structural Adjustment Credit – Programu ya Mikopo
ya Urekebishaji Miundo
-
PSRP Public Service Reform Programme – Programu za Mageuzi ya Huduma
za Umma
-
RAS Reginal Administrative Secretaries – Makatibu Tawala wa Mikoa
-
SME Small to Medium Enterprises – Viwanda Vidogo hadi vya Kati
-
TAS Tanzania Assistance Strategy – Mbinu za Kusaidia Tanzania
-
TIC Tanzania Investment Centre – Kituo cha Uwekezaji Tanzania
-
TIPER Tanzania-Italian Petroleum Refinery – Mtambo wa Kusafisha
Mafuta Tanzania na Italia
-
TRCHS Tanzania Reproductive and Child Health Survey (1999) - Mpango wa
Uzazi na Afya ya Watoto
-
TSED Tanzania Socio-Economic Database – Mfumo wa Utunzaji wa Taarifa
za Jamii na Uchumi
-
TTC Teacher Training College – Chuo cha Ualimu
-
VPO Vice President's Office – Ofisi ya Makamu wa Rais
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni