Kijitabu kinachoelezea kwa Lugha rahisi Mkakati wa Kupunguza Umasikini
Maelezo yametolewa na Hakikazi Catalyst
Katuni zimechorwa na Ally Masoud (Kipanya)
Dibaji
Imeelezwa katika Mkakati wa upunguzaji Umasikini (PRSP) kwamba "Serikali
inakusudia kuendelea kuhimiza uwakilishi kamili wa watu masikini na washika dau wengine
katika kutekeleza, kusimamia na kutathmini mbinu za upunguzaji umasikini".
Kijitabu hiki kilichoeleza mkakati huu kwa lugha rahisi ni mchango wa mawazo kutoka
jumuiya za wananchi yaliyoratibiwa na Hakikazi Catalyst. Hakikazi Catalyst ni mojawapo wa
mashirika yaliyopo kwenye mtandao wa kupunguza madeni na kuhamasiaha maendeleo (TCDD).
Nakala elfu tano za Kiswahili na elfu mbili za Kiingereza zimetolewa kwa Serikali kuu,
Mikoa, Wilaya na Jumuiya huru za Wananchi. Mawazo yaliyomo katika kijitabu hiki yanabaki
kama yalivyo katika mkakati wa awali wa serikali (Toleo la Novemba 2000) isipokuwa picha
za kuchorwa (katuni) na vidokezo vilivyoongezwa pamoja na sehemu ndogo inayoeleza baadhi
ya maana ya maneno muhimu. Aidha, kumeongezwa maswali kumi yanayochochea jamii kufikiri
kwa makini kuhusu jitihada za kuondoa umaskini. Ziada hizi zitamsaidia msomaji kuelewa
vizuri kijitabu hiki.
Tumeomba nafasi katika magazeti ya Daily News na Majira kutoa mchango huu katika mwezi
wa Mei na Juni 2001 mara moja kwa wiki ili kupata maoni, majibu na uchambuzi wa upunguzaji
wa umasikini kwa ujumla kutoka kwa watu mbalimbali. Maoni hayo yatanakiliwa katika mtandao
(website, - angalia chini.)
Unakaribishwa kama mtu binafsi au kikundi kutoa maoni yako kuhusu maswali yaliyoulizwa
katika kijitabu hiki na kutoa ushauri unaoona unafaa. Maoni yatumwe kwa:
Tanzania Without Poverty Campaign
Hakikazi Catalyst
P.O. Box 781 Arusha
Simu: 255 27 2509860
E-mail: hakikazi@cybernet.co.tz |
“Sasa hivi tunataka mipango
yote ya maendeleo itokane na wananchi wenyewe badala ya kutoka serikali kuu”
[Rais Benjamin Mkapa – gazeti la
Guardian 31 Machi 2001]
|
|
Tafadhali zingatia kuwa tuna website http://www.hakikazi.org
na pia tunaendesha e-mail ya majadiliano. Unaweza kujiunga na mjadala kwa njia ya e-mail
toka hapa
Jiunge kwenye orodha yetu ya barua pepe (e-mail)!
Bonyeza kitufe kilichoandikwa 'Jiunge kwenye orodha'
Kisha jaza anwani yako ya barua pepe!
|
Yaliyomo
| Waonavyo Wataalamu |
| Tofauti Kimkoa |
| Picha kubwa zaidi |
| Umasikini wa Mapato na usio wa Mapato |
| Mpango Mzima |
| Ubunifu wa Malengo ya Kitaifa yaliyo wazi |
| Ubunifu wa mazingira ya Kiuchumi ambayo yatachochea Maendeleo |
| Zingatia Mawazo Matatu ya Mwongozo |
| Haja ya kuwa na Viashirio |
| Kujenga Mfumo wa Usimamizi na Tathmin i |
| Maendeleo ya Vijijini na Ukuaji wa Biashara ya Nje |
| Uendelezaji wa Sekta Binafsi |
| Utawala Bora |
| Uchumi Mkuu Imara |
| Elimu |
| Afya |
| Ustawi wa Jamii ? Ushirikishwaji katika shughuli za Kisiasa |
| Njia za Mapato |
| Kipaumbele katika Matumizi |
| Upunguzaji wa Umasikini: Vipengele muhimu vya ziada |
| Jinsi mpango ulivyobuniwa |
| Namna mipango ya baadaye itakavyobuniwa |
SURA YA 1
UMASIKINI NI NINI?
Watu tofauti hufasiri maana ya umasikini kwa njia mbalimbali. Viongozi kwa kawaida
hufikiria juu ya umasikini kwa kuangalia uwezo wa watu katika kununua mahitaji yao na
kuuza bidhaa zao. Lakini fasiri ya umasikini ni kubwa zaidi. Kuna fasiri ya kuzingatia
matatizo ya kuwa na mgawanyo sawa katika kupata elimu na afya bora, kuwa na heshima na
hadhi katika jamii, kujisikia kuwa una uwezo wa kutatua tatizo lolote linalotokea katika
maisha yako, na hivyo kuwa na matumaini ya maisha. Kwa hiyo kuna mengi ya kufikiria wakati
unapotaka kuondoa umasikini. Kwa hakika fikra nyingi haziko wazi mpaka unapofikiria kwa
makini yanayotendeka katika jamii.
Watu wa kawaida, wafanyabiashara, wafanyakazi serikalini, Mawaziri na
viongozi wa nje wana mawazo tofauti kuhusu swali la umasikini ni nini. Wana mawazo tofauti
kuhusu sababu za umasikini na jinsi ya kuuondoa. Hata hivyo, kuna mawazo ya jumla
yafuatayo yanayokubalika: |
Kama jamii huru
haiwezi kuwasaidia watu wengi ambao ni masikini, haiwezi kuwaokoa wachache ambao ni
matajiri.
[John Fitzgerald Kennedy 1917 – 63, Raisi wa 6
wa Marekani].
|
|
Wataalamu wanavyoliona suala la Umasikini
Katika dunia ya sasa watu hununua mahitaji yao kwa kutumia pesa. Kama hawana njia za
kupata pesa watakuwa maskini. Umasikini mbaya zaidi ni ule ambao unawafanya watu wasiweze
kupata chakula. Kwa hali hiyo, wanakuwa dhaifu na wanaweza kufa kwa njaa. Hali nyingine ya
umasikini ni ile ambayo watu wanaweza kuwa na chakula kiasi au kidogo lakini hawana maji
salama, huduma za matibabu, nyumba au mavazi bora.
Takwimu za mwaka 1992 zinaonyesha kuwa karibu robo ya Watanzania wanaangukia katika
kundi la kwanza la umasikini na nusu ya Watanzania wanaangukia katika kundi la pili.
Katika mwaka 1995 karibu theluthi (1/3) ya idadi ya Watanzania walikuwa masikini. Hali
hiyo huenda ni mbaya zaidi hivi sasa. Lakini umasikini una vipengele vingine zaidi licha
ya kutokuwa na fedha za kutosha kununulia chakula, nguo, kujenga nyumba na kumudu gharama
za matibabu. Utafiti kuhusu umasikini unaonyesha kuwa watu maskini zaidi:
| Wamedumaa kwa sababu ya lishe duni |
| Wanapata vifo zaidi vya watoto wachanga, vijana na kuwa na maisha mafupi |
| Wanapata maji yasiyo salama · |
| Wanapata elimu duni |
|
| Umasikini unajitokeza katika maeneo tofauti: Sehemu fulani
za nchi zina unafuu zaidi kuliko sehemu nyingine. |
| Kuna umasikini zaidi vijijini kuliko mijini, japokuwa
dalili zinaonesha ongezeko la umasikini kwa kasi mijini. |
| Vijana na wazee na wale ambao wanatoka katika familia kubwa
zisizo na uwezo wanakuwa masikini zaidi kuliko wengine |
|
|
Utafiti unaonyesha pia kuwa watu masikini: · Hawalindwi kikamilifu na sheria ·
Hawashirikishwi katika maamuzi katika nyanja za kisiasa · Hawasaidiwi wakipata majanga
kama vile ukame, mafuriko, n.k.
Watu wa kawaida wanavyoliona suala la umasikini
Watu wa kawaida walipoulizwa wajiepushe na nini ili wasiingie katika hali ya umasikini
walitoa mawazo yafuatayo: · Wamiliki ardhi · Wapate zana za kilimo na teknolojia
inayofaa · Wapate misaada na mikopo · Wawe na usafiri mzuri (barabara na magari) ·
Waweze kupata masoko kwa urahisi · Wawe na mipango bora ya matumizi ya maji · Kujenga
uwezo wa kuweka akiba · Usalama kazini · Wapate huduma bora za jamii na miundo msingi
(hasa afya ya elimu) · Kupunguza rushwa, kuwe na uwazi zaidi, kuimarisha uwajibikaji na
ushirikishwaji katika kuchangia kutoa maamuzi katika kiwango cha Serikali za mitaa na
Serikali kuu · Kujijengea fikra za kimaendeleo · Kujenga uwezo wa mipango mizuri katika
ngazi ya kijiji · Kuunda upya na kuimarisha vyama vya Ushirika · Kuwawezesha Wanawake
wawe na madaraka zaidi katika kudhibiti mali ya familia · Kujenga umoja, mshikamano,
kuaminiana na hali ya kushirikiana
Tofauti Kimkoa
Mwaka 1999 Serikali ilitathmini mikoa ambayo ina umasikini zaidi. Tendo hili halikuwa
rahisi kwa sababu kulikuwa na njia nyingi za kupima umasikini. Mambo ambayo yalijumuishwa
katika zoezi hili ni pamoja na afya, lishe, chakula, elimu na ukuaji wa uchumi.
Haikukusudiwa kuonyesha nani kashinda au kashindwa, lakini matokeo yalionyesha kuwa mikoa
ambayo ni masikini zaidi ni Dodoma, Kagera, Lindi, Kigoma na Pwani. Mikoa ambayo ni
masikini kidogo ni Dar es Salaam, Ruvuma, Kilimanjaro, Singida na Tabora.
Picha Kubwa zaidi
Wakati wa mkutano wa kitaifa uliojadili mkakati wa kwanza kuhusu mbinu (njia) za
kuondoa umasikini (PRSP), mawazo yote yaliyotajwa hapo juu yalikubaliwa. Hata hivyo watu
waliona kuwa palikuwa na haja ya: · Kushughulikia tatizo la ajira kwa vijana na hasa
mijini · Kuzuia uharibifu wa mazingira · Kuzuia ajira ya watoto ·
Kuongeza fedha zilizopo kwa ajili ya kuondoa umasikini (hii ni pamoja na
kufutiwa madeni ya nje na kutafuta njia nyingine ya misaada ya nje) · Kuendeleza mfuko wa
fedha ili kusaidia wakulima wadogo wadogo · Kuwasaidia watu kuendeleza biashara ya kati
· Kuifanya nchi ivutie biashara kubwa · Kufanya utafiti zaidi ili kutambua jambo gani
linapaswa kufanywa na tuna uwezo gani wa kulifanya jambo hilo. |
“Watu wa asili duniani wana mali chache, lakini si masikini.
Umasikini si kuwa na mali chache, wala si uhusiano kati ya uwezo na ukomo wa mali; kwa
hakika ni mahusiano kati ya watu. Umasikini ni hadhi katika jamii. Kwa hakika ni matokeo
ya hali bora ya kuishi.”
[Marshall Sahlins, Mwana athropolojia wa Kimarekani]
|
|
Umasikini wa Mapato na Usio wa Mapato
Kwa kuwa kuna njia nyingi za kuzingatia suala la umasikini ni vyema kuwa na makubaliano
ya fasili za umasikini. Fasili hizi zitasaidia katika majadiliano na katika kufanya
mipango. Kutokana na tulivyosema hapo juu, ni vyema kufikiria juu ya umasikini kwa namna
mbili:
Umasikini ulio na kipato kidogo:
Kinafikiriwa kuwa wakati mapato ya watu ni chini ya dola moja kwa siku (kama shilingi
800/= za Tanzania). Hii ina maana kwamba hawatakuwa na chakula cha kutosha, uwezo wa
kupata tiba, watakuwa na mavazi na nyumba duni.
Umasikini Usio wa Kipato:
Kuna wakati watu wanakuwa na fedha kidogo na hivyo hawawezi kumudu shule nzuri au kuwa
na maji salama. Watu wanaoishi katika umasikini usio na kipato wanategemewa kudumaa na
kufa mapema. Aidha, watu wa aina hiyo hawategemewi kushirikishwa katika kutoa maamuzi
yanayohusu maisha yao.
Kipato
cha kimasikini kinapima watu wananunua na kutumia pesa kwa kiasi gani. Umasikini usio na
kipatounahusu ubora wa maisha na maisha ya kijamii. Unapima vitu vingi ambavyo vinawaondoa
watu katika hali duni ya umasikini na kuwaingiza katika hali bora.
|
Kutoka hali duni ya umasikini |
Kuingia hali bora |
Rushwa |
Uaminifu na haki |
Vurugu |
Amani na usawa |
Kutokuwa na uwezo |
Demokrasia ya watu |
unyonge |
Uwezo wa kutenda |
Riziki ndogo Mali na
amani
|
Mali na amani |
|
Mtaji wa Jamii
Watu wote wana utaratibu ulio rasmi na usio rasmi wa makundi ambayo hujihusisha nayo
katika kuendeleza maisha yao. Hali hii ndiyo inayoitwa “mtaji wa jamii”(social
capital) na tunaweza tukaikuza. Njia za kuondoa umasikini ni pamoja na kuzingatia wakati
ujao ambapo mtaji huu wa jamii hukua na kuingiza ushirikishwaji na ushirika katika ngazi
zote hadi taifa na hata kimataifa. Ikiwa tutafikiri na kufanya kazi pamoja basi Watanzania
wote wataishi katika hali njema.
Habari hii nimeipata...HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni