Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Machi 21, 2012

MORNING STAR RADIO 105.3 FM




Njozi za kuanzishwa kwa Radio hii, zilianza mnamo miaka ya tisini, ambapo mwaka 2000 viongozi wa makanisa ya Dar es salaam walikutana na kuweka mkakati madhubuti ya kuanzisha radio,kwa wakati huo ikijulikana kama TAWR (Tanzania Adventist World Radio).

Mwaka 2001, uchunguzi yakinifu wa kuanzishwa kwa Kituo hiki ulianza chini ya kitengo cha mawasiliano cha Makao makuu ya Kanisa Tanzania kijulikanacho kama TAMC (Tanzania Adventist Media Center).

Baada ya mikakati madhubuti kukamilika, ujenzi wa kituo cha radio ulianza rasmi mnamo mwaka 2002, katika eneo la Mikocheni B, jijini Dar es salaam, ujenzi ambao uliendelea na kukamilika kwa sehemu kubwa mnamo mwaka 2003.

Mnamo tarehe moja mwezi wa kumi mwaka 2003, kituo kilirusha matangazo yake kwa mara ya kwanza kama majaribio, kwa kutumia mtambo wa kurushia matangazo wenye uwezo wa watt 500, na tangu hapo safari ya matangazo kusikika hewani iliendelea!

Mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2003, kituo kilifunguliwa rasmi na Mgeni aliyehudhuria
shughuli hiyo, Mchungaji Jan Paulsen, akija kama Rais wa kanisa la Waadventista wasabato
Duniani, akitoea Nchini Marekani ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Duniani, yalipo.

Majuma mawili baada ya kufunguliwa rasmi kwa kituo, Mtambo wa kurushia matangazo
uliokuwa umefungwa mikocheni B mahali zilipo studio, ulishindwa kufanya kazi
kutokana na hitilafu iliyosababishwa na umeme, tatizo lililojitokeza baada ya mvua kali kunyesha.

Jitihada za kujaribu kuirejesha katika hali ya kuendelea kufanya kazi zilishindikana,
jambo lililopelekea muingiliano na vyombo vingine vya habari, na kituo kufungwa kwa muda
na tume ya mawasilianona, ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa marekebisho. Kituo kilirejea
tena katika hali yake na kuendelea na matangazo baada ya miaka miwili baadae.


Mwaka 2005 mwezi wa tano,vifaa vipya vya kurushia matangazo viliagizwa ili kurejesha matangazo tena. Uagizaji huo  ulichukua muda wa miezi mitatu, na mwezi wa nane vifaa viliwasili na ufungaji ukaanza mara moja, wakati huu mtambo ukiwa umehamishiwa eneo la kisarawe, mkoa wa Pwani.

Baada ya ufungaji mtambo kukamilika, mnamo mwezi wa nane mwaka 2005, urushaji wa matangazo ya majaribio  ulianza mara moja, ambapo majaribio hayo yalichukua takribani mwezi mmoja, hadi mnamo mwezi wa tisa!

Ilipofika tarehe 26, mwezi wa tano mwaka 2006, saa 11:00 jioni, kituo kilirusha
matangazo moja kwa moja kwa mara ya kwanza, baada ya matangazo ya majaribio
kukamilika!

Tangu hapo, Morning Star Radio imeendelea kurusha matangazo yake hadi hivi sasa,
ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakibarikiwa sana na matangazo haya, na kwa
hakika kituo hiki kimekuwa ni mbaraka sana kwa ma elfu ya wakaazi wa Tanzania
na dunia kwa ujumla ambapo matangazo
ya Redio hii yanasikika!

MAWASILANO:
Mahali:                 P.O.BOX 77170, Dar es Salaam, Tanzania
Simu:                     +255 222 780 680
Anwani Pepe:    morningstarradio@gmail.com




Maoni 1 :

  1. Mbona blog ikowzi sana haina vitu? Hainyeshi sehem ya kupunguzia na kuongezea sauti. Na ingekua nivyema kama mjadala ya kwenye radio ingekua inajadiliwa pia hapa

    JibuFuta