Photo Credit: www.microsoft.com |
Kuna wataalamu wanaojumlisha pia vitabu katika historia ya vyombo ya habari tangu kupatikana kwa uchapishaji vitabu; wengine wanaona pia aina za maigizo ya tamthiliya kama vyombo vya habari katika jamii za kale.
Kwa jumla maelezo ya kitaalamu ya vyombo vya habari ilikuwa hadi juzi:
- "Mawasiliano kwa vyombo vya habari ni mawasiliano ambako habari zinasambazwa wazi (bila kuzuia au kutenga sehemu ya watu kwa kusudi) kwa njia ya mbinu za teknolojia lakini si moja kwa moja (yaani kupitia umbali) na kutoka upande mmoja (watoa habari na wapokeaji hawabadilishani nafasi zao) kwa wapokeaji waliosambazwa."
Iko wazi ya kwamba tamthiliya haikubaliki na maelezo haya. Lakini tangu kupatikana kwa intaneti hasa Web 2.0 tofauti kati ya watoa habari na wapokeaji imeshaanza kuondolewa kwa mfano kwa njia ya blogu na mitandao ya kijamii.
Vyombo vya habari vya kwanza kwa maana iliyoelezwa juu vilikuwa
magazeti. Yalifuatwa na redio na baadaye televisheni. Katika miaka ya
kwanza ya sinema filamu fupi za habari zilizoonyeshwa kabla ya filamu
kuu zilikuwa pia chombo muhimu cha habari kwa umma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni