Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Machi 07, 2012

Migomo...Ni nini Utatuzi Wake?


Photo credit by: www. cycleracks.com


 
Wimbi la migomo na maandamano yameshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Tunisia, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya kujiri mapinduzi yaliyotia ukomo utawala wa muda mrefu wa dikteta wa nchi hiyo Zainul Abidin bin Ali. Mgomo mkubwa huko Tunisia ulisitisha baadhi ya shughuli katika mji wa Siliana huko kaskazini mwa nchi hiyo. Aidha shule na barabara kadhaa zilifungwa pia mkoani humo. Wananchi waliogoma huko Tunisia walikuwa wakilalamikia kuongezeka kwa kiwango cha watu wasio na ajira na ukosefu wa maendeleo katika mkoa huo.





Maandamano mengi yalishuhudiwa pia katika mji wa Jendouba kaskazini magharibi mwa Tunisia ambapo waandamanaji waliifunga barabara kuu na kusababisha foleni ya magari. Waandamanaji walisema kuwa serikali imepuuza matatizo ya kijamii na kisiasa yanayowakabili wananchi. Hii ni katika hali ambayo Muungano Mkuu wa Wafanyakazi wa Tunisia ulitangaza kuwa wafanyakazi elfu 35 kutoka sekta mbalimbali walishiriki kwenye mgomo mkubwa. 



Photo credit by: www. cycleracks.com



Jamhuri ya Tunisia - ni nchi ya Afrika ya Kaskazini inayopakana na Bahari ya Mediteranea, Libya na Algeria. Mji mkuu ni Tunis iliyoko mahali pa Karthago ya kale. Wakazi karibu wote hutumia lugha ya Kiarabu. Takriban watu 200,000 wanaendelea kuzungumza Kiberber ambacho ni lugha ya asili ya wenyeji lakini Waberber wengi wameshaanza kutumia Kiarabu. Tunisia ilikuwa jimbo la "Africa" katika Dola la Roma. Eneo lake limewahi kutawaliwa na Wafinikia wa Karthago, Waroma wa Kale, Wavandali, Waarabu, Waturuki na Wafaransa.


 NDIPO NINAPOWAZA KWA NINI MIGOMO

Maoni 2 :

  1. Utatuzi wa asilimia MIA kwa MIA wa MIGOMO,...
    ni kuto KUGOMA aisee!:-(

    JibuFuta
  2. @Simon.

    Japo umeonesha hamasa ya kukerwa na migomo, changamoto iliyopo ni kwa namna gani kutogoma kutawezekana?.

    JibuFuta