Photo credit by: www. cycleracks.com |
Wimbi la migomo na maandamano yameshuhudiwa katika
baadhi ya maeneo ya Tunisia, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya kujiri
mapinduzi yaliyotia ukomo utawala wa muda mrefu wa dikteta wa nchi hiyo Zainul
Abidin bin Ali. Mgomo mkubwa huko Tunisia ulisitisha baadhi ya shughuli katika
mji wa Siliana huko kaskazini mwa nchi hiyo. Aidha shule na barabara kadhaa
zilifungwa pia mkoani humo. Wananchi waliogoma huko Tunisia walikuwa
wakilalamikia kuongezeka kwa kiwango cha watu wasio na ajira na ukosefu wa
maendeleo katika mkoa huo.
Maandamano mengi yalishuhudiwa pia katika mji wa Jendouba kaskazini magharibi
mwa Tunisia ambapo waandamanaji waliifunga barabara kuu na kusababisha foleni
ya magari. Waandamanaji walisema kuwa serikali imepuuza matatizo ya kijamii na
kisiasa yanayowakabili wananchi. Hii ni katika hali ambayo Muungano Mkuu wa
Wafanyakazi wa Tunisia ulitangaza kuwa wafanyakazi elfu 35 kutoka sekta
mbalimbali walishiriki kwenye mgomo mkubwa.
Photo credit by: www. cycleracks.com |
Jamhuri ya Tunisia - ni nchi ya Afrika ya
Kaskazini inayopakana na Bahari ya Mediteranea, Libya na Algeria. Mji mkuu ni
Tunis iliyoko mahali pa Karthago ya kale. Wakazi karibu wote hutumia lugha ya Kiarabu.
Takriban watu 200,000 wanaendelea kuzungumza Kiberber ambacho ni lugha ya asili
ya wenyeji lakini Waberber wengi wameshaanza kutumia Kiarabu. Tunisia ilikuwa jimbo la "Africa" katika
Dola la Roma. Eneo lake limewahi kutawaliwa na Wafinikia wa Karthago, Waroma wa
Kale, Wavandali, Waarabu, Waturuki na Wafaransa.
NDIPO NINAPOWAZA KWA NINI MIGOMO
Utatuzi wa asilimia MIA kwa MIA wa MIGOMO,...
JibuFutani kuto KUGOMA aisee!:-(
@Simon.
JibuFutaJapo umeonesha hamasa ya kukerwa na migomo, changamoto iliyopo ni kwa namna gani kutogoma kutawezekana?.