Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Januari 25, 2012

Mifano kutoka Methali za Tanzania

UKIMWI umeendelea kuleta changamoto katika maisha ya binadamu. Ni janga ambalo
linagusa maisha ya kila siku ya binadamu katika nchi nyingi na hasa zilizo fukara.
Kutokana na kugusa sehemu mbalimbali za maisha, janga hili limejadiliwa katika nyanja
mbalimbali za kitaaluma ikiwa ni pamoja na tabia na mahusiano ya watu (Nelkin na
wenzie 1991). Katika Tanzania, UKIMWI umejadiliwa kihistoria (Kaijage, 1993) na hata
katika sanaa mbalimbali ikiwamo lugha na fasihi (Mutembei 2001,
2002)

 na wenzie) wanavyosema katika
Wala sio kifua kikuu, lile gonjwa, kigaga cha magonjwa ya mlipuko, ambalo kwa
kulinganisha na magonjwa mengine lenyewe linaweza kutoa maandishi mengi ya kifasihi
kwa muda mfupi.

Mbali na kulinganishwa na kifua kikuu, UKIMWI nchini Marekani, unajitokeza zaidi
katika maandishi kuliko homa ya manjano, kipindupindu na magonjwa mengine mengi.
Kwa muda mfupi tu, UKIMWI umejitokeza katika maandishi ya kifasihi sawa na gonjwa
la tauni lilivyojitokeza katika maandishi ya namna hiyo huko Ulaya. Kwa sababu ya hali
hii, janga hili linavuta hamu ya kitaaluma ya kutaka kutafiti ni kwa vipi na kwa kiasi gani
limejipenyeza katika sanaa za jamii, na hususani limejipenyeza katika tanzu zipi za fasihi
ya jamii.

Kwa mfano, ni kwa kiasi gani UKIMWI umejipenyeza katika fasihi ya
Kiswahili? Ni kwa namna gani athari za UKIMWI zinaweza kuonekana kama kipengele
cha ujumi katika maisha ya Watanzania? Katika fasihi, ni tanzu zipi zimeitikia mguso wa
janga hili na kulielezea kisanii? Na maelezo hayo yanamaanisha nini katika maendeleo ya
utanzu husika na kwa fasihi kwa ujumla? Katika mantiki hii, makala haya yanajadili jinsi
utanzu wa methali unavyoguswa na janga hili.

Lengo la makala haya kwanza, ni kuelezea ni kwa kiasi gani UKIMWI umejipenyeza
katika fasihi na athari yake ni nini. Katika kufanya hivyo, mifano itatolewa kutoka katika
utanzu mdogo kuliko tanzu zote za fasihi yaani methali. Hoja ni kwamba, kama
UKIMWI umeweza kujipenyeza hadi katika utanzu wa fasihi ulio mdogo kabisa, basi
inawezekana katika tanzu nyingine, janga hili likaonekana waziwazi kifasihi.
Lengo la pili ni kuonesha ni kwa kiasi gani UKIMWI, ama umebadili methali
zilizokuwapo kabla ili ziweze kuakisi kuwepo kwa UKIMWI, au umeleta methali mpya.

Katika makala haya nimetumia zaidi methali kutoka katika kabila la Wahaya kwa kuwa
UKIMWI ulijitokeza mkoani Kagera mapema zaidi kuliko ulivyojitokeza katika mikoa
mingine yote ya Tanzania; na kutokana na hali hiyo athari za ugonjwa huu mkoani humo
ni za zamani, na pengine, kubwa zaidi kuliko katika mikoa mingine. Malengo haya
mawili ndiyo yaliyonisukuma niizungumzie dhana ninayoiita
kama nitakavyoielezea katika sehemu zinazofuata.

  ukimwishaji katika methali

Maana ya methali imeelezwa na kufafanuliwa na wanataaluma wengi wa fasihi. Baadhikeshatajwa: 8)). Wataalamu hawa wawili kama walivyoukweli na kuenea
Vipengele viwili zaidi vinapatikana katika kuiona methali kuwa ni "usemi mfupi
wa mapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na
tajriba" (Mulokozi 1996:36). Vipengele hivyo ni
inamaanisha uzoefu au "ujuzi" (Senkoro,
uzima (Madumulla,
ujuzi huu unaosemwa, au tajriba katika methali sio sifa miongoni mwa watoto au vijana.
Wazalishaji wakuu wa methali ni wazee, huku watoto na vijana wakiwa watumiaji tu.

Kwa hakika wengi walioandika kuhusu maana ya methali, hawakukimakinikia
kipengele cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia na uwezo wa mabadiliko hayo katika
kuathiri utamaduni wa mawasiliano katika jamii. Kwa sababu, kama tutakavyoona
baadaye, zamani usemi (methali) mmoja ulichukua muda mrefu sana kuweza kuenea
mahali pengi na katika jamii nyingi. Utamaduni huo sivyo ulivyo leo.

Dhana ya utamaduni na uhusiano wake na methali inajadiliwa na Knappert (1986)
ninayemuona hapa kuwa anahitimisha makabala huu unaoiona methali kimapokeo. Hata
hivyo, Knappert anapingana na Mulokozi na Madumulla ambao wanaelekea kutoa hoja
kuwa methali ni utanzu wa wazee na sio wa vijana; kwa kuwa wazee, kutokana na
maisha yao marefu, basi wameona mengi na wana busara ionekanayo kupitia katika
methali.

Akielezea kwa nini methali inahusishwa na wazee, Knappert anasema:
umapokeo na tajriba. Sifa ya tajribakeshatajwa) unaokwenda sambamba na utukeshatajwa). Ukiangalia kwa makini mawazo haya utagundua kuwa
Na hii inafafanua ni kwa nini methali zihusishwe na wahenga, na wale wenye umri
mkubwa katika jamii, sio ati kwa sababu wana uzoefu mkubwa zaidi, na kwa hiyo
wanakumbuka zaidi maneno ya busara, lakini ni kwa kuwa ni shauku yao kushikilia
muundo wa jamii yao uliopo...

methali. Hizi ni pamoja na ufupi wa usemi, ukweli wa yale yasemwayo, muda wake
katika jamii, kusambaa au kuenea kwake na mawazo yake mazito au ya busara. Makala
haya yanalenga kuziangalia tena sifa hizi na kutoa maoni kuwa baadhi yake hazina budi
kuangaliwa upya kwani zimepitwa na wakati.


Tuanze na sifa ya ukweli wa usemi. Hoja kwamba methali husema ukweli,
imejadiliwa kwa kina na Mineke Schipper (2004) katika andiko lake lililokusanya
methali elfu kumi na tano kutoka mataifa mbalimbali duniani. Akiangalia jinsi mataifa
mbalimbali yanavyomzungumzia mwanamke kupitia methali Schipper anadai kuwa
"ukweli" unaosemwa katika methali ni "ukweli" wa kundi fulani la jamii, na sio
wanajamii wote kwa pamoja.

Kwa mfano, Schipper anaonesha jinsi ambavyo wanawake
wanavyotazamwa na wanaume kutoka mataifa mbalimbali –kupitia methali. Anaonesha
pia jinsi ambavyo wanaume hutofautiana kijamii na kiuchumi kutokana na nafasi zao.
Kwa hiyo "ukweli" unaosemwa kupitia katika methali ni ukweli wa watu fulani tu na
kwa sababu fulani tu; na wahenga wanaosemwa huwakilisha mawazo ya kundi
linalohusika , siyo yale ya jamii yote kwa ujumla.

Mkabala huu wa kimapokeo wa wataalamu wachache tuliowaona unatoa sifa tano za
Mara nyingi wazungumzaji wa methali za Kiswahili huanza kwa kusema ‘wahenga
walisema....’ au ‘kama wahenga walivyosema....’
huwa zinaitwa methali kutokana na umri wake katika jamii ina "ukweli" kiasi gani? Je,
vijana hawawezi kuwa na methali zao? Je methali hutokeaje? Na je, ili usemi uweze
kuitwa methali hauna budi uwe na umri gani katika jamii? Maswali haya nilijiuliza baada
ya mjadala kwamba UKIMWI haujakaa katika jamii kwa muda mrefu wa kutosha
kuweza kuzua methali.

Suala la methali hutokeaje, na umri gani uwe wa kutosha limeangaliwa na akina
Omari, Kezilahabi na Kamera (1975). Wao wanasema kwamba misemo ikikaa kwa muda
wa kutosha katika jamii, hata kuwa na kufanana toka jamii moja hadi nyingine, ikisema
kwa kifupi "busara" za wahenga, basi hubadilika kuwa methali. Je umri wa kutosha ni
upi? Tunaikubali fikra kwamba ili usemi uitwe methali hauna budi kuwa umeenea katika
jamii mbalimbali.

Jambo muhimu la kujadiliana ni kuhusu misemo na methali. Je ni wakati gani
msemo hukoma kuwa msemo na kuanza kuwa methali? Bila shaka mojawapo ya sifa
zitakikanazo ni msemo kuwa umeenea mahali pengi. Uwe unafanana katika jamii nyingi.
Hiki ni kigezo cha msingi. Hata hivyo, ikumbukwe kuwa namna za kueneza usemi kama
huo leo ni tofauti kabisa na jinsi ilivyokuwa miaka ishirini na mitano iliyopita. Ni tofauti
na jinsi ilivyokuwa miaka hamsini iliyopita. Leo hii kutokana na mapinduzi katika
mifumo ya mawasiliano, jambo linaweza kusemwa sehemu moja na likasikika sehemu
nyingi kwa wakati mmoja na kwa upesi sana. Leo hii, radio na televisheni zinarusha
matangazo dunia nzima katika jamii nyingi na kwa lugha mbalimbali kwa kasi ya hali ya
juu.

Uwezo huu wa teknolojia unalazimisha mabadiliko katika nadharia mbalimbali
zilizokuwapo hapo awali. Hii leo usemi mmoja unaweza kuenezwa kwa njia mbalimbali
kwa haraka na kwa mvuto tofauti. Kwa mfano matangazo ya biashara katika televisheni
yanavutia zaidi leo na yanaweza kuenezwa kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa hapo
mwanzo. Uanzishwaji wa matumizi ya simu za mikononi umeleta mapinduzi makubwa
katika mawasiliano. Leo hii usemi mfupi uliobeba muhtasari wa mawazo fulani ya jamii,
unaweza kuenezwa kwa siku moja na ukaanza kutumika haraka miongoni mwa vijana,
watu wazima au watoto kwa kadri utakavyokuwa umewekwa. Kwa mtindo huu huu, leo
hii matangazo kuhusu UKIMWI yanarushwa kwa haraka, yanawafikia watu wengi zaidi
na kwa njia mbalimbali.

Tukiangalia hali ya teknolojia Tanzania na wakati wa UKIMWI, tunaona kuwa janga
hili "limezushwa" duniani si zaidi ya miaka thelathini iliyopita. Huu ni wakati ambapo
nchini Tanzania kulikuwa na mabadiliko makubwa katika teknolojia ya habari na
mawasiliano. Zilianzishwa redio kadhaa, na nchi ikapata televisheni zaidi ya moja.
Mabango ya matangazo yalianza kujaa barabarani na simu za mikononi zilianza kuenea
nchini. Njia hizi zote ziliwezesha kuanzishwa kwa misemo na semi mpya na kuzieneza
kwa haraka katika jamii za Waswahili, Afrika ya Mashariki. Aidha, baadhi ya semi na
misemo mingine iliyokuwapo ilibadilishwa na kuenea kwa haraka hasa miongoni mwa
vijana.

Katika mtazamo huo basi tunaweza kusema makala haya yanatoa changamoto
kubwa katika kuangaliwa upya kwa utanzu wa fasihi na uhusiano uliopo kati ya utanzu
huo na mabadiliko katika teknolojia ya habari na mawasiliano. Ni jambo la kuzingatia
kwamba yafaa maana za tanzu mbalimbali za fasihi ziendane na jamii iliyopo, na wakati
huo huo ziwe na sifa za kukivuka kizingiti cha wakati.

Umuhimu mwingine wa makala haya ni kuchochea udadisi mpana zaidi katika
tanzu za fasihi. Ni matarajio yangu kuwa msomaji atataka kujua hasa maana ya leo ya
methali ni nini. Mwingine baada ya kusoma makala haya anaweza kusema, 'utanzu
mmoja wa methali hautoshi kuonesha athari za UKIMWI katika tanzu za fasihi', hivyo
akatafiti na kuandika kuhusu athari za UKIMWI katika tanzu nyingine mbili au tatu.
Ikitokea hivyo, makala haya yatakuwa yamefanikiwa kuchochea udadisi sio tu wa ni nini
maana ya methali, bali pia athari ya UKIMWI katika tanzu nyinginezo za fasihi.

Labda nihitimishe sehemu hii kwa kusema kuwa kuendelea kutumiwa kwa misemo
hiyo na wanajamii, hasa misemo inayohusu UKIMWI, kunanifanya nijiulize swali moja
ambalo ndilo linalonishughulisha katika makala haya. Ninataka kujua athari za UKIMWI
katika tanzu za fasihi. Nitafanya hivyo kwa kuitazama athari hiyo katika utanzu wa
methali kwa kutumia dhana ya ambayo nimeamua kuiita
Je, hoja kwamba methali ni za wazee naukimwishaji.
yao ni Roger (1981); Roger (1982); Senkoro (1982); Schipper (1991); Madumulla
(1995); na Abrams (1999). Methali imefafanuliwa kuwa ni usemi mfupi wenye maana na
ambao unaelezea ukweli fulani ulioenea mahali pengi ukizungumzia maisha ya kila siku
(Cuddon 1991:752; Abrams (
waliowatangulia, wanaongelea vipengele viwili vilivyo muhimu:
mahali pengi.


Kuhusu lugha na fasihi kwa ujumla, UKIMWI ndio ugonjwa ambao kwa muda
mfupi umejitokeza katika maandishi zaidi kuliko magonjwa mengine yoyote yale. Hata
katika nchi za ki-Magharibi kwa mfano, kifasihi UKIMWI umejitokeza katika maandishi
zaidi kuliko saratani. Nchini Marekani, UKIMWI umejadiliwa zaidi katika maandishi
kuliko kifua kikuu katika miaka ya 1990 kama Goldstein (
nukuu hii:

Maoni 1 :