Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Januari 27, 2012

MATENDO YA SHETANI

Neno hili hutumika mara 35 katika Agano Jipya. Iblisi kwa Kigiriki diabolos ni jina linalomaanisha "Mtapitapi" "Mpinzani"; "Mshtaki" - sawa na Shetani.
Kadiri ya imani ya dini mbalimbali, hasa zile zinazokubali ufunuo waliopewa Waisraeli, shetani ni malaika, roho, au mungu mdogo anayewakilisha uovu unaopingana na Mungu. 

Shetani aajulikana pia kwa jina la Ibilisi (kutoka Kigiriki Diabolos, -ou, "Anayetenganisha"), Mtawala wa giza, Mkuu wa ulimwengu huu, Belzebub (jina la dhihaka kwa mungu Baal linalotafsiriwa "Bwana wa nzi"), Belial, Lusiferi (kutoka Kilatini Lucifer, "Mleta mwanga"). 

Baadhi ya watu, kwa mfano Wakristadelfiani, hufundisha kwamba Shetani ni mfano tu wa uovu na dhambi.
Shetani kwa Kiebrania  Satan, kwa Kigiriki Satanâs, kwa Kilatini Sátanas ni jina linalomaanisha "Mpinzani"; "Mshtaki".

******************************* 

RAFIKI, UMEISOMA HII...!!!!????????????

*******************************
KATIKA PEKUA PEKUA KWENYE FACEBOOK NIMEKUTANA NA HII HABARI HaPa. TAFADHALI SOMA KWA MAKINI NA UTAFAKARI UKWELI WAKE.....

Lucifer, Mkuu wa mashetani aliitisha semina elekezi kwa mashetani wote Duniani na katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano
huo alisema:-

"Tumeshindwa kuwazuia WANADAMU wasiende kwenye nyumba za IBADA" Tumeshindwa
...kuwazuia wasisome VITABU vyao vitakatifu na kufahamu ukweli"
Tumeshindwa hata kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kweli kwa MITUME yao " "Mara wapatapo muungano wa kweli kwenye MAHUBIRI ya DINI zao, mamlaka yetu yatakuwa yamefika mwisho." Kwa hiyo kuanzia sasa waacheni waende kwenye nyumba zao za IBADA, waacheni waendelee na karamu zao za upendo,

LAKINI waibieni muda, ili wasipate nafasi ya kudumisha IBADA za kweli kweli kwa MOLA WAO MUUMBA...." "Hiki ndicho ninachotaka mfanye." Alisema Lucifer:
"wataabisheni WANADAMU WOOTE wasipate kamwe kushikamana na DINI zao na wasifungamane katika KUMCHA MUNGU""Tutafanyaje jambo hilo?" mashetani yalimwuuliza

kwa jazba.

LUCIFER aliwajibu:
"hakikisheni wanakuwa 'BUSY' (BUSY= Being Under Satan's York ) katika mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao na muwaanzishie mipango mingi sana isiyohesabika ili kujaza akili na ufahamu wao. "Washughulisheni na kutumia, na kutumia, na kutumia; na kukopa, nakukopa, na kukopa."

"Washawishini wake zao waende kufanya kazi kwa siku na kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa siku na Waume zao wafanye kazi kwa siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa 10 hadi 12 kwa siku, ili wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote kulingana na mfumo huo wa maisha." "Wazuieni wasiwe na nafasi ya kukaa na watoto wao" "Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha kwamba hawaiskii ile sauti ndogo tulivu ya Mungu wao."

"Washawishini walize radio au kaseti au muziki kwenye simu, popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu. Waache TV,VCR, CD na KOMPYUTER zikiwa zimewashwa kama kawaida majumbani mwao na mhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki usiokuwa wa KIDINI tena mfululizo bila kukoma." "Hii itasonga akili na fahamu zao na kuvunja ule muungano kwa MOLA WAO."

"Jazeni magazeti na vijarida mbalimbali vya upuuzi kwenye meza zao za kahawa na chai Duniani kote." "Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani yafahamu zao kwa muda wa masaa 24." "Ingilieni kwenye muda wao wa kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo.' "Kwenye masanduku ya posta na barua pepe jazeni vipeperushi
na majarida na kila aina ya matangazo ya habari za vitu na hudumu yanayowapa matumaini ya uongo."
 


"Wekeni wanawake warembo sana mitaani, club, maofisini na kwenye Televisheni na majarida ili kwamba Wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba urembo wa nje ndio muhimu, na wasiridhike na wake zao."

"Wafanyeni wake zao wachoke sana wasiweze kuonyesha upendo kwa waume zao nyakati za usiku.Wapeni maumivu ya kichwa ili wasiwape waume zao upendo wanaouhitaji sana,ili waanze kutazama kwingine. Wafanyeni Wanawake wawadharau Waume zao na kuwapuuza.

"Hiyo itaparaganyisha familia zao haraka sana !
"Wapeni WANADAMU Waalimu wa uongo ili wawapotoshe wasifundishe maneno ya MUNGU ya kweli kwa watoto wao na waumini wao."

"Hakikisheni wanakuwa 'BUSY' na kusongwa na mambo kiasi kwamba hawapati muda wa kutafakari wema wa Mungu. Badala yake wapeni kutalii kwenye maeneo ya ajabu, matukio ya michezo, matamasha, kumbi za sinema na video."Wafanye wawe 'BUSY,' 'BUSY,' 'BUSY,! Yaani wasongwe na kusongwa na kusongwa na kazi kwelikweli!"
"Na wanapokutanika kwenye ibada zao za kiroho wafanye waingie katika umbea na fitina na kuzungumzia mambo madogo madogo ya umbea na fitina ili waondoke wakiwa na dhamira mbaya zilizochafuliwa."

"Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha yao ili wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za MUNGU. Muda si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe, badala ya maelekezo ya MUNGU, huku wakihatarisha afya zao na za familia zao kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe."

"Itafanya kazi" "Itafanya kazi!
"Huu ni mkakati kweli kweli. Mashetani yaliondoka kwenye mkutano yakiwa na hamu kubwa sana ya kutekeleza majuku hayo waliyopewa na kuanza kuwafanya WANADAMU wawe wa kukimbia na mambo huku na huko. Watakuwa na muda
mdogo sana kwa ajili ya Mungu wao na familia zao. Wakakosa muda wa kuwaeleza wengine kuhusu MAMBO YA IBADA na kubadili maisha ya wanadamu.
*******************************
SWALI:- JE SHETANI AMEFANIKIWA

KATIKA MIPANGO YAKE HIYO? WEWE NDIYE HAKIMU !!!!!!!! TAFAKARI KUANZIA SASA KUTATHMINI UMETOKA WAPI, UKO WAPI NA UNAKWENDA WAPI. PIA UNA MKAKATI GANI WA KUPAMBANA NA MIKAKATI YA SHETANI.
'UBIZE' au kutingwa na kazi kunamaanisha : kuwa chini ya mkataba au utumwa wa shetani?

PLEASE PASS THIS ON, IF YOU ARE NOT TOO BUSY !!
VERY INTERESTING TO LEARN SEMINA ELEKEZI YA MASHETANI.
.
 
 

Maoni 2 :

  1. so interesting to hear that, ni kwamba hayo yote ni ya ukweli kabisaa na hayapingiki na yanaendelea sana tuu huku duniani, ukiangalia dini imekuwa kama desturi tuu za watuu,kanisani kwenda ni kutimiza wajibu huko nyumbani hilo lipo, ukija hapa ulaya hata kwenda kanisani ni kazi hakuna anayeenda kanisani, mfano mmoja tuu kanisa ninalosali tupo watu tusiozidi ishirini vijana tupo watatu wanaobaki ni wazee, angalia kwenye matamasha ya mziki vijana wanavyojaa mpaka wanakosa nafasi ya kukanyaga, huo ni mpango mzima wa ibilisi, kwani Biblia inasema vijana ndo wana nguvu ndo watakao toka na kutangaza neno la Mungu angalia nguvu zao wanatumia kwenye nini???, tuje kwenye habari zilizojaa kwenye vyombo vya habari asilimia tisini ni za kuharibu akili zetu na kuzipumbaza nothing more. Barabarani ukipita hayo matangazo yaliyojaa ni ya kishetani tuu, mfano hapa Norway nikiwa safarini naenda Sweeden u cant believe unakutana na tangazo linasema wanauza na kununua ngono kweli jamani??? kilichobakki hapo ni nini?? Mwisho sasa shetani amefanikiwa katika kila idara kuwarubuni wanadamu na ndo mana kila kitu tunaona ni sawa tuu, Mungu atusaidie kwa nguvu na uwezo wetu hatuwezi

    JibuFuta