Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Januari 29, 2012

Uchambuzi







....ni uwezo, udhaifu, fursa na vitisho ni mbinu ya kimkakati ambayo hutumika kutathmini S uwezo, W udhaifu, O fursa, na T vitisho vinavyopatikana katika mradi au biashara husika. Inahusisha ubainishaji wa lengo la biashara au mradi na kutambua mambo ya ndani na ya nje ambayo yanafaa au hayafai katika kufikia lengo hilo. Sifa za mbinu hii ni zake Albert Humphrey, ambaye aliongoza makubaliano katika Chuo Kikuu cha Stanford mnamo miaka ya 1960 na 1970 kwa kutumia takwimu kutoka makampuni mia tano(500) ya Fortune.

Uchambuzi wa SWOT lazima uanze kwa kufafanua mwisho wa jambo linalotamaniwa au lengo lake. Uchambuzi wa uwezo, udhaifu, fursa na vitisho unaweza kujumuishwa katika kielelezo cha mipango ya kimkakati. Mfano wa mbinu ya kimkakati inayojumuisha lengo linaloendeshwa na uchambuzi wa SWOT ni Uchambuzi wa kimkakati bunifu. Mipango ya kimkakati, ikiwemo Uchambuzi wa SWOT na Uchambuzi wa kimkakati bunifu, imekuwa hoja kuu katika utafiti.

·   S Uwezo: sifa za mtu au kampuni ambazo zitamsaidia katika kufikia lengo.
·   W Udhaifu: sifa za mtu au kampuni ambazo zinazuia kufikia lengo.
·   O Nafasi: hali za nje ambazo zinasaidia katika kufikia lengo.
·   T Vitisho: hali za nje zinazoweza kusababisha uharibifu wa lengo.

Ubainishaji wa Uchambuzi wa SWOT ni muhimu kwa sababu hatua zinazofuata mchakato wa kupanga mafanikio ya lengo lililochaguliwa au kadiriwa, laweza kutoka kwa SWOT.

Kwanza, lazima waamuzi watambue kama lengo laweza kufikiwa kutokana na Uchambuzi wa uwezo,udhaifu,fursa na vitisho. Kama lengo haliwezi kufikiwa, lazima lengo tofauti lichaguliwe na mchakato kurejelewa.
Mara nyingi uchambuzi wa SWOT hutumika katika usomi kuonyesha na kutambua uwezo, udhaifu, fursa na vitisho. Ni wa munufaa hasa katika kutambua maeneo kwa ajili ya maendeleo.

Matumizi bunifu ya SWOT: kuzalisha Mikakati

Kama, kwa upande mwingine, lengo linaonekana kufikiwa, SWOT hutumiwa kama pembejeo kwa ubunifu wa kizazi cha mikakati iwezekanayo, kwa kuuliza na kujibu kila moja ya maswali manne yafuatayo, mara nyingi:

·   Tunawezaje kutumia na kufaidika katia kila nguvu au uwezo?
·   Tunawezaje kuboresha kila Udhaifu?
·   Tunawezaje Kutumia na kufaidika kutokana na kila Nafasi au fursa?
·   Tunawezaje kupunguza kila Tishio?

Kwa kawaida, kikundi kilicho na uamilifu mwingi au jopo kazi liwakilishalo mitazamo mingi ndilo lipasalo kutekeleza uchambuzi wa SWOT. Kwa mfano, timu ya SWOT inaweza kuhusisha mhasibu, muuzaji, meneja mtendaji, mhandisi, na mpokezi wa maswala ya utenda kazi kwa umma.

Kulinganisha na Kubadilisha

Njia nyingine ya kutumia SWOT ni kulinganisha na kubadilisha.
Ulinganishaji hutumiwa kupata faida za ushindani kwa kulinganisha uwezo na nafasi. Kubadilisha ni kutumia mikakati ya kugeuza vitisho au udhaifu kuwa uwezo au fursa. Mfano wa mkakati wa Kugeuza ni kutafuta masoko mapya.
Kama vitisho au udhaifu hauwezi kubadilishwa basi yafaa kampuni ijaribukuupunguza au kuuepuka.

Ushahidi katika Matumizi ya SWOT

Uchambuzi wa SWOT huweza kupunguza mikakati inayofikiriwa katika tathmini. "Aidha, watu ambao wanatumia SWOT wanaweza kufikiri kuwa wamefanya kazi nzuri ya kupanga na wapuuze mambo yanayostahili kama kufafanua malengo ya kampuni au kuhesabu ROI kwa mikakati mbadala." Matokeo kutoka Menon na wenzake (1999)[5] na Hill na Westbrook (1997) yameonyesha kwamba SWOT huweza kudhuru utendaji. Kama mbadala wa SWOT, J. Scott Armstrong anaelezea mbinu mbadala ya hatua tano (5) ambayo hupelekea utendaji bora wa shirika. 

Ukosoaji huu unaelekezwa kwa toleo la zamani la SWOT linalotangulia uchanganuzi wa Uchambuzi wa uwezo,udhaifu,fursa na vitisho ulioelezewa hapo juu, kwa mada "Mkakati na Matumizi bunifu ya uchanganuzi SWOT." Toleo hili la zamani halikuhitaji SWOT zitolewe kutoka kwa lengo lililokubaliwa. Mifano ya uchanganuzi wa SWOT isiyotaja lengo imetolewa hapa chini katika "Rasilimali za kibinadamu" na "elimu ya soko."

Vipengele vya ndani na njeLengo la uchanganuzi wowote wa Uchambuzi wa SWOT ni kutambua vipengele vya ndani na nje ambavyo ni muhimu katika kufikia lengo. Havi huja kutoka ndani ya mkusanyiko wa thamani ya kipekee ya kampuni. Uchanganuzi wa Uchambuzi wa SWOT unajumuisha vipande muhimu kwa makundi mawili makuu:

·   Vipengele vya ndani - uwezo na udhaifu wa ndani ya shirika.
·   Vipengele vya nje - nafasi na vitisho vilivyowakilishwa na mazingira ya nje kwa shirika. - Tumia hali ya kisiasa,kiuchumi,kijamii,technologia au uchambuzi wahali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, teknolojia,mazingira na ya uhalali kusaidia kutambua vipengele

Mambo ya ndani yanaweza kutazamwa kama uwezo au udhaifu kulingana na athari zake kwenye malengo ya shirika. Kile kinachoweza kuwakilisha uwezo na heshima katika lengo moja kinaweza kuwa na udhaifu kwa lengo lingine. Sababu zinaweza kujumuisha 4P's;zote, na vile vile wafanyakazi, fedha, uwezo wa viwanda, na kadhalika. Mambo ya nje yanaweza kujumuisha masuala makubwa ya uchumi, mabadiliko ya teknolojia, sheria, na mabadiliko ya kiutamaduni, na vilevile mabadiliko sokoni au katika nafasi ya ushindani. Mara nyingi matokeo hutolewa kwa namna ya matriki.

Uchambuzi wa SWOT ni njia moja tu ya uainishaji na ina udhaifu wake. Kwa mfano, inaweza kushawishi makampuni kuandika orodha badala ya kufikiri kuhusu kilicho muhimu hasa katika kufikia malengo. Pia inatoa orodha bila uchunguzi muhimu na bila mpangilio maalum hivi kwamba, kwa mfano, nafasi dhaifu huweza kuonekana kusawazisha vitisho kviuu.

Ni jambo la busara kutoondoa kwa haraka mgombea yeyote anayeingizwa na SWOT. Umuhimu wa kila SWOT utafanuliwa au kuabainika kwa thamani ya mikakati inayozalisha. Bidhaa ya SWOT inayozalisha mikakati ya thamani ni muhimu. Bidhaa ya SWOT isiyozalisha mikakati si muhimu.

 

Matumizi ya Uchambuzi wa SWOT

Umuhimu wa uchambuzi wa SWOT haukomi tu kwa mashirika ya kutafuta faidaWa viti You may not post si mdogo kwa faida ya kutafuta mashirika. Uchambuzi wa SWOT unaweza kutumika katika maamuzi yoyote wakati lengo la mwisho linalonuiwa limefafanuliwa. Mifano ni kama: mashirika yasiyo ya faida, vitengo vya kiserikali, na watu binafsi. Uchambuzi wa SWOT pia waweza kutumika katika kupanga mikakati ya kabla ya mgogoro na usimamizi wa kuzuia tatizo. Uchambuzi wa SWOT unaweza pia kutumika katika kujenga mapendekezo wakati wautafiti wa uwezekano wa kitu.

Uchanganuzi wa kimandhari wa SWOT

Mandhari ya SWOT huchukua usimamizi wa aina mbalimbali kwa maono mapana ya kutazamia utendaji wa kulinganishwa vitu kulingana na matokeo yake Brendan Kitts, Leif Edvinsson na Tord Beding (2000).
Mabadiliko katika utendaji wa kadiri huendelea kutambuliwa. Miradi (au vitengo vingine vya vipimo ) ambavyo vingeweza kuwa hatari vinazungumziwa.
Mandhari ya SWOT pia huonyesha sababu gande za nguvu / udhaifu ambazo zilikuwa au zitakuwa na ushawishi mkubwa katika muktadha wa thamani katika matumizi (kwa mfano:kuyumbayumba kwa thamani ya Mtaji. )

Mipango ya shirika

Kama sehemu ya maendeleo ya mikakati na mipango ya kuwezesha shirika kufikia malengo yake, basi, hilo shirika litatumia mchakato wenye utaratibu / mkali unaojulikana kamamipango ya shirika. SWOT pamoja na hali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiteknolojia / hali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiteknolojia, kimazingira na ya uhalali huweza kutumika kama kigezo cha uchambuzi wa biashara na mambo ya mazingira. 

·   Kuweka malengo - kufafanua yakayofanywa na shirika
·   Ubainishaji wa Mazingira
o  Tathmini ya ndani ya SWOT ya shirika, hii inafaa kujumuisha tathmini ya hali ya sasa pamoja na mpangilio wa bidhaa / huduma na uchambuzi wa muda wa kutumika kwa bidhaa /mzunguko huo.

·   Uchambuzi wa mikakati iliyopo, hii itaamua umuhimu kutokana na tathmini ya matokeo ya ndani / nje . Huenda hii ikajumuisha uchambuzi pengo ambayo itaangalia maswala ya kimazingira

·   Masuala ya kimikakati yakiwa yameelezwa - vipengele muhimu katika kuendeleza mpango wa shirika unaohitaji kuangaliwa na shirika

·  Ibuwa mikakati mipya / iliyopigwa msasa' - mikakati iliyopigwa msasa yaweza kumaanisha kuwa kuna haja ya malengo kubadilishwa

·   Tambua vipengele muhimu vya mafanikio - kuafikia malengo na utekelezaji wa mikakati

·   Maandalizi ya uendeshaji, rasilimali, mipango ya miradi kwa utekelezaji mkakati

·   Ufuatiliaji matokeo - kwenda dhidi ya mipango, kuchukua hatua ya kurekebisha ambayo inaweza kumaanisha marekebisho kiasi kwa malengo / mikakati.

Elimu ya soko

Katika uchanganuzi wa washindani wengi, wauzaji huweka maelezo ya kina kuhusu kila mshindani katika soko, wakilenga hasa nguvu na udhaifu wa ushindani huo wakitumia uchambuzi wa SWOT. Mameneja masoko wataangazia muundo gharama wa kila mshindani , vyanzo vya faida, rasilimali na uwezo, kujiekeza kwa ushindani na kutofautiana kwa bidhaa , kiwango cha mahusiano kati ya walio juu na walio chini, majibu ya kihistoria kwa maendeleo ya kiwanda, na mambo mengine.

Usimamizi wa masoko mara nyingi hupata kuwa ni muhimu kuwekeza katika utafiti wa kukusanya takwimu sahihi zinazohitajika ili kuendeleza uchanganuzi wa masoko ulio hakika. Kwa hivyo, mara nyingi usimamizi hufanya utafiti wa soko (au masoko ya utafiti) ili kupata habari hii. Wauzaji hutumia mbinu mbalimbali kufanya utafiti wa soko, lakini baadhi ya zile ambazo ni za kawaida ni kama:

·   Utafiti wa uzuri wa masoko, kama vile vikundi vinavyoangaziwa
·   Utafiti wa wingi wa masoko, kama vile takwimu tafiti
·   Mbinu za majaribio kama vile mtihani wa masoko
·   Mbinu za kuangalia kama vile uchunguzi wa kiethnografia (za papo hapo)
·  Mameneja wa masoko wanaweza pia kubuni na kusimamia michakato mbalimbali ya ubainishaji mazingira na ushindani wenye werevu ili kusaidia kubaini mielekeo na kurekebisha uchambuzi wa masoko ya kampuni.

Kutumia SWOT kuchanganua msimamo wa soko wa usimamizi mdogo unaozingatia usimamizi wa rasilimali za binadamu.

Ahsante sana WikiPedia.

Ijumaa, Januari 27, 2012

MATENDO YA SHETANI

Neno hili hutumika mara 35 katika Agano Jipya. Iblisi kwa Kigiriki diabolos ni jina linalomaanisha "Mtapitapi" "Mpinzani"; "Mshtaki" - sawa na Shetani.




Kadiri ya imani ya dini mbalimbali, hasa zile zinazokubali ufunuo waliopewa Waisraeli, shetani ni malaika, roho, au mungu mdogo anayewakilisha uovu unaopingana na Mungu. 

Shetani aajulikana pia kwa jina la Ibilisi (kutoka Kigiriki Diabolos, -ou, "Anayetenganisha"), Mtawala wa giza, Mkuu wa ulimwengu huu, Belzebub (jina la dhihaka kwa mungu Baal linalotafsiriwa "Bwana wa nzi"), Belial, Lusiferi (kutoka Kilatini Lucifer, "Mleta mwanga"). 

Baadhi ya watu, kwa mfano Wakristadelfiani, hufundisha kwamba Shetani ni mfano tu wa uovu na dhambi.
Shetani kwa Kiebrania  Satan, kwa Kigiriki Satanâs, kwa Kilatini Sátanas ni jina linalomaanisha "Mpinzani"; "Mshtaki".

******************************* 

RAFIKI, UMEISOMA HII...!!!!????????????

*******************************
KATIKA PEKUA PEKUA KWENYE FACEBOOK NIMEKUTANA NA HII HABARI HaPa. TAFADHALI SOMA KWA MAKINI NA UTAFAKARI UKWELI WAKE.....

Lucifer, Mkuu wa mashetani aliitisha semina elekezi kwa mashetani wote Duniani na katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano
huo alisema:-

"Tumeshindwa kuwazuia WANADAMU wasiende kwenye nyumba za IBADA" Tumeshindwa
...kuwazuia wasisome VITABU vyao vitakatifu na kufahamu ukweli"
Tumeshindwa hata kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kweli kwa MITUME yao " "Mara wapatapo muungano wa kweli kwenye MAHUBIRI ya DINI zao, mamlaka yetu yatakuwa yamefika mwisho." Kwa hiyo kuanzia sasa waacheni waende kwenye nyumba zao za IBADA, waacheni waendelee na karamu zao za upendo,

LAKINI waibieni muda, ili wasipate nafasi ya kudumisha IBADA za kweli kweli kwa MOLA WAO MUUMBA...." "Hiki ndicho ninachotaka mfanye." Alisema Lucifer:
"wataabisheni WANADAMU WOOTE wasipate kamwe kushikamana na DINI zao na wasifungamane katika KUMCHA MUNGU"



"Tutafanyaje jambo hilo?" mashetani yalimwuuliza

kwa jazba.

LUCIFER aliwajibu:
"hakikisheni wanakuwa 'BUSY' (BUSY= Being Under Satan's York ) katika mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao na muwaanzishie mipango mingi sana isiyohesabika ili kujaza akili na ufahamu wao. "Washughulisheni na kutumia, na kutumia, na kutumia; na kukopa, nakukopa, na kukopa."

"Washawishini wake zao waende kufanya kazi kwa siku na kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa siku na Waume zao wafanye kazi kwa siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa 10 hadi 12 kwa siku, ili wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote kulingana na mfumo huo wa maisha." "Wazuieni wasiwe na nafasi ya kukaa na watoto wao" "Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao ili kuhakikisha kwamba hawaiskii ile sauti ndogo tulivu ya Mungu wao."

"Washawishini walize radio au kaseti au muziki kwenye simu, popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu. Waache TV,VCR, CD na KOMPYUTER zikiwa zimewashwa kama kawaida majumbani mwao na mhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki usiokuwa wa KIDINI tena mfululizo bila kukoma." "Hii itasonga akili na fahamu zao na kuvunja ule muungano kwa MOLA WAO."

"Jazeni magazeti na vijarida mbalimbali vya upuuzi kwenye meza zao za kahawa na chai Duniani kote." "Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani yafahamu zao kwa muda wa masaa 24." "Ingilieni kwenye muda wao wa kuendesha barabarani kwa kuwaonyesha mabango na matangazo.' "Kwenye masanduku ya posta na barua pepe jazeni vipeperushi
na majarida na kila aina ya matangazo ya habari za vitu na hudumu yanayowapa matumaini ya uongo."




 


"Wekeni wanawake warembo sana mitaani, club, maofisini na kwenye Televisheni na majarida ili kwamba Wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba urembo wa nje ndio muhimu, na wasiridhike na wake zao."

"Wafanyeni wake zao wachoke sana wasiweze kuonyesha upendo kwa waume zao nyakati za usiku.Wapeni maumivu ya kichwa ili wasiwape waume zao upendo wanaouhitaji sana,ili waanze kutazama kwingine. Wafanyeni Wanawake wawadharau Waume zao na kuwapuuza.

"Hiyo itaparaganyisha familia zao haraka sana !
"Wapeni WANADAMU Waalimu wa uongo ili wawapotoshe wasifundishe maneno ya MUNGU ya kweli kwa watoto wao na waumini wao."

"Hakikisheni wanakuwa 'BUSY' na kusongwa na mambo kiasi kwamba hawapati muda wa kutafakari wema wa Mungu. Badala yake wapeni kutalii kwenye maeneo ya ajabu, matukio ya michezo, matamasha, kumbi za sinema na video."Wafanye wawe 'BUSY,' 'BUSY,' 'BUSY,! Yaani wasongwe na kusongwa na kusongwa na kazi kwelikweli!"
"Na wanapokutanika kwenye ibada zao za kiroho wafanye waingie katika umbea na fitina na kuzungumzia mambo madogo madogo ya umbea na fitina ili waondoke wakiwa na dhamira mbaya zilizochafuliwa."

"Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha yao ili wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za MUNGU. Muda si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe, badala ya maelekezo ya MUNGU, huku wakihatarisha afya zao na za familia zao kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe."

"Itafanya kazi" "Itafanya kazi!
"Huu ni mkakati kweli kweli. Mashetani yaliondoka kwenye mkutano yakiwa na hamu kubwa sana ya kutekeleza majuku hayo waliyopewa na kuanza kuwafanya WANADAMU wawe wa kukimbia na mambo huku na huko. Watakuwa na muda
mdogo sana kwa ajili ya Mungu wao na familia zao. Wakakosa muda wa kuwaeleza wengine kuhusu MAMBO YA IBADA na kubadili maisha ya wanadamu.
*******************************
SWALI:- JE SHETANI AMEFANIKIWA

KATIKA MIPANGO YAKE HIYO? WEWE NDIYE HAKIMU !!!!!!!! TAFAKARI KUANZIA SASA KUTATHMINI UMETOKA WAPI, UKO WAPI NA UNAKWENDA WAPI. PIA UNA MKAKATI GANI WA KUPAMBANA NA MIKAKATI YA SHETANI.
'UBIZE' au kutingwa na kazi kunamaanisha : kuwa chini ya mkataba au utumwa wa shetani?

PLEASE PASS THIS ON, IF YOU ARE NOT TOO BUSY !!
VERY INTERESTING TO LEARN SEMINA ELEKEZI YA MASHETANI.
.
 
 

Jumatano, Januari 25, 2012

Mifano kutoka Methali za Tanzania

UKIMWI umeendelea kuleta changamoto katika maisha ya binadamu. Ni janga ambalo
linagusa maisha ya kila siku ya binadamu katika nchi nyingi na hasa zilizo fukara.
Kutokana na kugusa sehemu mbalimbali za maisha, janga hili limejadiliwa katika nyanja
mbalimbali za kitaaluma ikiwa ni pamoja na tabia na mahusiano ya watu (Nelkin na
wenzie 1991). Katika Tanzania, UKIMWI umejadiliwa kihistoria (Kaijage, 1993) na hata
katika sanaa mbalimbali ikiwamo lugha na fasihi (Mutembei 2001,
2002)

 na wenzie) wanavyosema katika
Wala sio kifua kikuu, lile gonjwa, kigaga cha magonjwa ya mlipuko, ambalo kwa
kulinganisha na magonjwa mengine lenyewe linaweza kutoa maandishi mengi ya kifasihi
kwa muda mfupi.

Mbali na kulinganishwa na kifua kikuu, UKIMWI nchini Marekani, unajitokeza zaidi
katika maandishi kuliko homa ya manjano, kipindupindu na magonjwa mengine mengi.
Kwa muda mfupi tu, UKIMWI umejitokeza katika maandishi ya kifasihi sawa na gonjwa
la tauni lilivyojitokeza katika maandishi ya namna hiyo huko Ulaya. Kwa sababu ya hali
hii, janga hili linavuta hamu ya kitaaluma ya kutaka kutafiti ni kwa vipi na kwa kiasi gani
limejipenyeza katika sanaa za jamii, na hususani limejipenyeza katika tanzu zipi za fasihi
ya jamii.

Kwa mfano, ni kwa kiasi gani UKIMWI umejipenyeza katika fasihi ya
Kiswahili? Ni kwa namna gani athari za UKIMWI zinaweza kuonekana kama kipengele
cha ujumi katika maisha ya Watanzania? Katika fasihi, ni tanzu zipi zimeitikia mguso wa
janga hili na kulielezea kisanii? Na maelezo hayo yanamaanisha nini katika maendeleo ya
utanzu husika na kwa fasihi kwa ujumla? Katika mantiki hii, makala haya yanajadili jinsi
utanzu wa methali unavyoguswa na janga hili.

Lengo la makala haya kwanza, ni kuelezea ni kwa kiasi gani UKIMWI umejipenyeza
katika fasihi na athari yake ni nini. Katika kufanya hivyo, mifano itatolewa kutoka katika
utanzu mdogo kuliko tanzu zote za fasihi yaani methali. Hoja ni kwamba, kama
UKIMWI umeweza kujipenyeza hadi katika utanzu wa fasihi ulio mdogo kabisa, basi
inawezekana katika tanzu nyingine, janga hili likaonekana waziwazi kifasihi.
Lengo la pili ni kuonesha ni kwa kiasi gani UKIMWI, ama umebadili methali
zilizokuwapo kabla ili ziweze kuakisi kuwepo kwa UKIMWI, au umeleta methali mpya.

Katika makala haya nimetumia zaidi methali kutoka katika kabila la Wahaya kwa kuwa
UKIMWI ulijitokeza mkoani Kagera mapema zaidi kuliko ulivyojitokeza katika mikoa
mingine yote ya Tanzania; na kutokana na hali hiyo athari za ugonjwa huu mkoani humo
ni za zamani, na pengine, kubwa zaidi kuliko katika mikoa mingine. Malengo haya
mawili ndiyo yaliyonisukuma niizungumzie dhana ninayoiita
kama nitakavyoielezea katika sehemu zinazofuata.

  ukimwishaji katika methali

Maana ya methali imeelezwa na kufafanuliwa na wanataaluma wengi wa fasihi. Baadhikeshatajwa: 8)). Wataalamu hawa wawili kama walivyoukweli na kuenea
Vipengele viwili zaidi vinapatikana katika kuiona methali kuwa ni "usemi mfupi
wa mapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na
tajriba" (Mulokozi 1996:36). Vipengele hivyo ni
inamaanisha uzoefu au "ujuzi" (Senkoro,
uzima (Madumulla,
ujuzi huu unaosemwa, au tajriba katika methali sio sifa miongoni mwa watoto au vijana.
Wazalishaji wakuu wa methali ni wazee, huku watoto na vijana wakiwa watumiaji tu.

Kwa hakika wengi walioandika kuhusu maana ya methali, hawakukimakinikia
kipengele cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia na uwezo wa mabadiliko hayo katika
kuathiri utamaduni wa mawasiliano katika jamii. Kwa sababu, kama tutakavyoona
baadaye, zamani usemi (methali) mmoja ulichukua muda mrefu sana kuweza kuenea
mahali pengi na katika jamii nyingi. Utamaduni huo sivyo ulivyo leo.

Dhana ya utamaduni na uhusiano wake na methali inajadiliwa na Knappert (1986)
ninayemuona hapa kuwa anahitimisha makabala huu unaoiona methali kimapokeo. Hata
hivyo, Knappert anapingana na Mulokozi na Madumulla ambao wanaelekea kutoa hoja
kuwa methali ni utanzu wa wazee na sio wa vijana; kwa kuwa wazee, kutokana na
maisha yao marefu, basi wameona mengi na wana busara ionekanayo kupitia katika
methali.

Akielezea kwa nini methali inahusishwa na wazee, Knappert anasema:
umapokeo na tajriba. Sifa ya tajribakeshatajwa) unaokwenda sambamba na utukeshatajwa). Ukiangalia kwa makini mawazo haya utagundua kuwa
Na hii inafafanua ni kwa nini methali zihusishwe na wahenga, na wale wenye umri
mkubwa katika jamii, sio ati kwa sababu wana uzoefu mkubwa zaidi, na kwa hiyo
wanakumbuka zaidi maneno ya busara, lakini ni kwa kuwa ni shauku yao kushikilia
muundo wa jamii yao uliopo...

methali. Hizi ni pamoja na ufupi wa usemi, ukweli wa yale yasemwayo, muda wake
katika jamii, kusambaa au kuenea kwake na mawazo yake mazito au ya busara. Makala
haya yanalenga kuziangalia tena sifa hizi na kutoa maoni kuwa baadhi yake hazina budi
kuangaliwa upya kwani zimepitwa na wakati.


Tuanze na sifa ya ukweli wa usemi. Hoja kwamba methali husema ukweli,
imejadiliwa kwa kina na Mineke Schipper (2004) katika andiko lake lililokusanya
methali elfu kumi na tano kutoka mataifa mbalimbali duniani. Akiangalia jinsi mataifa
mbalimbali yanavyomzungumzia mwanamke kupitia methali Schipper anadai kuwa
"ukweli" unaosemwa katika methali ni "ukweli" wa kundi fulani la jamii, na sio
wanajamii wote kwa pamoja.

Kwa mfano, Schipper anaonesha jinsi ambavyo wanawake
wanavyotazamwa na wanaume kutoka mataifa mbalimbali –kupitia methali. Anaonesha
pia jinsi ambavyo wanaume hutofautiana kijamii na kiuchumi kutokana na nafasi zao.
Kwa hiyo "ukweli" unaosemwa kupitia katika methali ni ukweli wa watu fulani tu na
kwa sababu fulani tu; na wahenga wanaosemwa huwakilisha mawazo ya kundi
linalohusika , siyo yale ya jamii yote kwa ujumla.

Mkabala huu wa kimapokeo wa wataalamu wachache tuliowaona unatoa sifa tano za
Mara nyingi wazungumzaji wa methali za Kiswahili huanza kwa kusema ‘wahenga
walisema....’ au ‘kama wahenga walivyosema....’
huwa zinaitwa methali kutokana na umri wake katika jamii ina "ukweli" kiasi gani? Je,
vijana hawawezi kuwa na methali zao? Je methali hutokeaje? Na je, ili usemi uweze
kuitwa methali hauna budi uwe na umri gani katika jamii? Maswali haya nilijiuliza baada
ya mjadala kwamba UKIMWI haujakaa katika jamii kwa muda mrefu wa kutosha
kuweza kuzua methali.

Suala la methali hutokeaje, na umri gani uwe wa kutosha limeangaliwa na akina
Omari, Kezilahabi na Kamera (1975). Wao wanasema kwamba misemo ikikaa kwa muda
wa kutosha katika jamii, hata kuwa na kufanana toka jamii moja hadi nyingine, ikisema
kwa kifupi "busara" za wahenga, basi hubadilika kuwa methali. Je umri wa kutosha ni
upi? Tunaikubali fikra kwamba ili usemi uitwe methali hauna budi kuwa umeenea katika
jamii mbalimbali.

Jambo muhimu la kujadiliana ni kuhusu misemo na methali. Je ni wakati gani
msemo hukoma kuwa msemo na kuanza kuwa methali? Bila shaka mojawapo ya sifa
zitakikanazo ni msemo kuwa umeenea mahali pengi. Uwe unafanana katika jamii nyingi.
Hiki ni kigezo cha msingi. Hata hivyo, ikumbukwe kuwa namna za kueneza usemi kama
huo leo ni tofauti kabisa na jinsi ilivyokuwa miaka ishirini na mitano iliyopita. Ni tofauti
na jinsi ilivyokuwa miaka hamsini iliyopita. Leo hii kutokana na mapinduzi katika
mifumo ya mawasiliano, jambo linaweza kusemwa sehemu moja na likasikika sehemu
nyingi kwa wakati mmoja na kwa upesi sana. Leo hii, radio na televisheni zinarusha
matangazo dunia nzima katika jamii nyingi na kwa lugha mbalimbali kwa kasi ya hali ya
juu.

Uwezo huu wa teknolojia unalazimisha mabadiliko katika nadharia mbalimbali
zilizokuwapo hapo awali. Hii leo usemi mmoja unaweza kuenezwa kwa njia mbalimbali
kwa haraka na kwa mvuto tofauti. Kwa mfano matangazo ya biashara katika televisheni
yanavutia zaidi leo na yanaweza kuenezwa kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa hapo
mwanzo. Uanzishwaji wa matumizi ya simu za mikononi umeleta mapinduzi makubwa
katika mawasiliano. Leo hii usemi mfupi uliobeba muhtasari wa mawazo fulani ya jamii,
unaweza kuenezwa kwa siku moja na ukaanza kutumika haraka miongoni mwa vijana,
watu wazima au watoto kwa kadri utakavyokuwa umewekwa. Kwa mtindo huu huu, leo
hii matangazo kuhusu UKIMWI yanarushwa kwa haraka, yanawafikia watu wengi zaidi
na kwa njia mbalimbali.

Tukiangalia hali ya teknolojia Tanzania na wakati wa UKIMWI, tunaona kuwa janga
hili "limezushwa" duniani si zaidi ya miaka thelathini iliyopita. Huu ni wakati ambapo
nchini Tanzania kulikuwa na mabadiliko makubwa katika teknolojia ya habari na
mawasiliano. Zilianzishwa redio kadhaa, na nchi ikapata televisheni zaidi ya moja.
Mabango ya matangazo yalianza kujaa barabarani na simu za mikononi zilianza kuenea
nchini. Njia hizi zote ziliwezesha kuanzishwa kwa misemo na semi mpya na kuzieneza
kwa haraka katika jamii za Waswahili, Afrika ya Mashariki. Aidha, baadhi ya semi na
misemo mingine iliyokuwapo ilibadilishwa na kuenea kwa haraka hasa miongoni mwa
vijana.

Katika mtazamo huo basi tunaweza kusema makala haya yanatoa changamoto
kubwa katika kuangaliwa upya kwa utanzu wa fasihi na uhusiano uliopo kati ya utanzu
huo na mabadiliko katika teknolojia ya habari na mawasiliano. Ni jambo la kuzingatia
kwamba yafaa maana za tanzu mbalimbali za fasihi ziendane na jamii iliyopo, na wakati
huo huo ziwe na sifa za kukivuka kizingiti cha wakati.

Umuhimu mwingine wa makala haya ni kuchochea udadisi mpana zaidi katika
tanzu za fasihi. Ni matarajio yangu kuwa msomaji atataka kujua hasa maana ya leo ya
methali ni nini. Mwingine baada ya kusoma makala haya anaweza kusema, 'utanzu
mmoja wa methali hautoshi kuonesha athari za UKIMWI katika tanzu za fasihi', hivyo
akatafiti na kuandika kuhusu athari za UKIMWI katika tanzu nyingine mbili au tatu.
Ikitokea hivyo, makala haya yatakuwa yamefanikiwa kuchochea udadisi sio tu wa ni nini
maana ya methali, bali pia athari ya UKIMWI katika tanzu nyinginezo za fasihi.

Labda nihitimishe sehemu hii kwa kusema kuwa kuendelea kutumiwa kwa misemo
hiyo na wanajamii, hasa misemo inayohusu UKIMWI, kunanifanya nijiulize swali moja
ambalo ndilo linalonishughulisha katika makala haya. Ninataka kujua athari za UKIMWI
katika tanzu za fasihi. Nitafanya hivyo kwa kuitazama athari hiyo katika utanzu wa
methali kwa kutumia dhana ya ambayo nimeamua kuiita
Je, hoja kwamba methali ni za wazee naukimwishaji.
yao ni Roger (1981); Roger (1982); Senkoro (1982); Schipper (1991); Madumulla
(1995); na Abrams (1999). Methali imefafanuliwa kuwa ni usemi mfupi wenye maana na
ambao unaelezea ukweli fulani ulioenea mahali pengi ukizungumzia maisha ya kila siku
(Cuddon 1991:752; Abrams (
waliowatangulia, wanaongelea vipengele viwili vilivyo muhimu:
mahali pengi.


Kuhusu lugha na fasihi kwa ujumla, UKIMWI ndio ugonjwa ambao kwa muda
mfupi umejitokeza katika maandishi zaidi kuliko magonjwa mengine yoyote yale. Hata
katika nchi za ki-Magharibi kwa mfano, kifasihi UKIMWI umejitokeza katika maandishi
zaidi kuliko saratani. Nchini Marekani, UKIMWI umejadiliwa zaidi katika maandishi
kuliko kifua kikuu katika miaka ya 1990 kama Goldstein (
nukuu hii:

Jumatatu, Januari 23, 2012

MALEZI

...ni kazi maalumu ya muda mrefu ambayo binadamu anamsaidia mwingine kukabili maisha kwa jumla au sehemu yake mojawapo.


Ni kazi inayowapasa kwanza wazazi, ambao wanahitaji msaada wa ukoo, kabila, taifa, dini n.k.
Ni kazi inayahitaji moyo mkuu na ustahimilivu mkubwa.
Nchi za Afrika zilipojikomboa zilikazania elimu ili kupata mapema wataalamu kwa kazi na huduma za jamii.
Hasa siku hizi wengi wameona umuhimu wa kusoma ili kukabili maisha. Ila mara nyingi juhudi hizo hazilengi kujua ukweli, bali kufanikiwa katika kazi na uchumi, na zinaweka pembeni maadili yaliyokuwa muhimu katika malezi ya kimila.
Hayo yalikusudiwa kuwaandaa watoto na vijana kwa maisha, wawe washiriki wa ukoo na kabila ambao wamekomaa kiasi cha kuweza kuchukua majukumu yao.
Hata leo bila ya hayo ujuzi na ufundi vinaweza kuongezeka, lakini ukomavu haufikiwi.
Hivyo vijana wanachelewa kushika nafasi yao katika ujenzi wa jamii, k.mf. kwa njia ya ndoa.
Badala yake unaenea uhuni (uasherati, bangi, wizi n.k.).
Kwa kuwa ujana ni kipindi cha mabadiliko ya haraka pande zote, ni vigumu kuumudu sawasawa na kuwa na msimamo.
Hasa mijini kuna mchanganyiko wa watu (makabila, dini n.k.) pamoja na njia hasi za kuishi zinazotokana na ushindani mkubwa, utepetevu katika maadili na upotovu.


Katika hali hiyo dini ya ukoo si kinga tena: kijana mwenyewe anajichagulia aamini nini na aishi vipi badala ya kufuata tu mazoea ya nyumbani kama alivyofanya utotoni.
Anahitaji kusaidiwa ajibu maswali makuu ya maisha: “Mimi ni nani? Nimetoka wapi? Ninakwenda wapi? Nafikiriwa kuwa wa namna gani?”
Kumbe watu wazima wengi wanamsema badala ya kujihusisha naye katika matatizo yasiyoepukika ya umri wake.
Anahitaji kueleweka na kuthaminiwa, lakini akitafuta hayo anaitwa jeuri, mwenye kiburi n.k.
Hasa siku hizi kati ya wazee na vijana umbali ni mkubwa kutokana na mabadiliko ya nyakati (upande wa elimu, afya, uchumi,mawasiliano, tunu za maisha n.k.).
Vijana wanaonelea miundo asili ni mambo ya zamani, hata wakadharau utamaduni wa mababu kama kwamba mambo yake yote yamepitwa na wakati.
Kinyume chake wanapokea kwa urahisi mkubwa mawazo mengi ya kigeni kupitia vyombo vya upashanaji habari na mitindo mipya inayozuka mijini.
Halafu wanatumia muda mwingi kijiweni au katika burudani, kumbe ule wa kukaa na wazee ni mfupi mno: hilo ni pengo lisilozibika, kwa kuwa linawafanya wasifaidi mang’amuzi ya vizazi vilivyotangulia, kutegemezwa na mashauri wanayoyahitaji, kuungana na ndugu zao katika kukabili maisha.
Wanakuwa jamii tofauti, wageni kati ya watu wao!
Wazee wengi wanaona vijana wakiungana ni nafasi tu ya kujenga urafiki mbaya, si haja halisi ya nafsi na ya maisha.
Hivyo badala ya kuwasaidia kuchambua mambo wanazidisha hali ya kutoelewana nao.
Basi, hatuna budi kulea kwa kuoanisha ujuzi na ukomavu ili tupate watu tunaowahitaji: watu ambao ni huru kwa ndani na wanaweza kuwajibika kwa uadilifu.
Ili kijana anazidi kukomaa kiutu anahitaji kusaidiwa ajifahamu ili kustawisha vipawa vyake na kupunguza kasoro zake.
Utu ndio msingi ambao juu yake yanajengwa maisha yote.
Mwenye matatizo nafsini mwake anasumbuka na kusumbua watu anaofungamana nao.
Basi, ni muhimu awahi kujirekebisha kama inavyobidi kuwahi ili kunyosha mti ukiwa bado mbichi.
Ni lazima aifanyie kazi nafsi yake kwa ustadi na bidii nyingi kuliko mkulima anavyoshughulikia shamba lake ili lizae sana.

Jumamosi, Januari 21, 2012

Tumsifu Leo (Zaburi 145:1-21)...Majibu Yafanyayo Kazi.


 
01. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
0
2. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
0
3. BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
0
4. Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
0
5. Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
0
6. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
0
7. Wataadhimisha wema wako mwingi na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.
0
8. BWANA ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo.
0
9. BWANA ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
10. Ee BWANA, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.
11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako,
12. ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
13. Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. BWANA ni mwaminifu kwa ahadi zake zote
na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
14. BWANA huwategemeza wote waangukao na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
15. Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.
17. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
18. BWANA yu karibu na wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu.
19. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.
20. BWANA huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza.
21. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu
milele na milele.
**************************************
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Ted Wilson and David Gates

Anapo: Talk in Sabbath Celebration.


Alhamisi, Januari 19, 2012

Yaani...Upepo Ni Mwendo Wa Hewa.


Husababishwa na joto la jua. Hewa ikipashwa joto na jua hupanuka huwa nyepesi na kupanda juu. Hivyo inaacha nafasi ambako hewa baridi zaidi inaingia kuchukua nafasi yake.


Kwa lugha ya metorolojia kuna mwendo kutoka eneo la shindikizo juu la hewa kwa eneo eneo lenye shindikizo duni ya hewa.


Kuna aina nyingi za upepo. Upepo mkali huitwa dhoruba. Ikizunguka ndani yake ni tufani, na tufani ikianza baharini ni Nguvu ya upepo ilitumiwa na binadamu tangu karne nyingi kwa njia ya teknolojia mbalimbali kama vile

  • jahazi na usafiri wa maji
  • kuendesha mashine za kusaga nafaka
  • kuendesha pampu za maji kwa umwagiliaji

Tangu karne ya 20 nguvu ya upepo imetumiwa pia kutengeneza umeme. Katika karne ya 21 umeme wa upepo umeanza kuwa chanzo muhimu wa nishati.

Jumatano, Januari 18, 2012

UTAPIAMLO

utapiamlo umekuwa kwa muda mrefu umejulikana kupunguzu maendeleo ya uchumi na kuendeleza umasikini, na bado kipindi cha miaka kumi jumuia ya kimataifa na serikali nyingi katika nchi zinazoendelea wameshindwa kushughulika utapiamlo, ijapokuwa kuna mtazamo unayo tahiri kabisa kama reporti inauyosema 

sasa chaguo la muhimu ni baina ya kuendelea kushindwa, kama jumuia ya ulimwengu ilivyofanya na ukimwi kwa kupita miaka kumi au kwa mwisho wa wiki lishe katika ya maendeleo ili safu kubwa ya uchumi na maendeleo ya jumuia yanayotegemea na lishe inaweza kutambua.”