Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Januari 21, 2012

Tumsifu Leo (Zaburi 145:1-21)...Majibu Yafanyayo Kazi.


 
01. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
0
2. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
0
3. BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
0
4. Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
0
5. Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
0
6. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
0
7. Wataadhimisha wema wako mwingi na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.
0
8. BWANA ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo.
0
9. BWANA ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
10. Ee BWANA, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.
11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako,
12. ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
13. Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. BWANA ni mwaminifu kwa ahadi zake zote
na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
14. BWANA huwategemeza wote waangukao na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
15. Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16. Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.
17. BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
18. BWANA yu karibu na wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu.
19. Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.
20. BWANA huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza.
21. Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu
milele na milele.
**************************************
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Ted Wilson and David Gates

Anapo: Talk in Sabbath Celebration.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni