Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Novemba 28, 2011

LARVENIE MASS...MWALIMU WA UIMBAJI NA EDITOR KTK MEDIA

Harusi ni sherehe kwa ajili ya kufunga ndoa. Ndoa ni muungano wa maisha yote kati ya watu wawili unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii yaani mwanamke na mwanamme.

*******************************************

Mwanaume ni binadamu wa kiume. Kwa kawaida ni mtu mzima anayeitwa hivi kwani wanaume wadogo huitwa watoto wa kiume tu au wavulana.

Wanaume ni takriban nusu ya binadamu, wengine huwa wanawake. Wanaume na wanawake ni jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.


*******************************************

Mwanamke ni mwanadamu wa jinsia ya kike. Kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau amebalehe. Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kike.

*******************************************

Mitara (au Upoli au Upali) ni hali ya watu zaidi ya wawili kuishi katika uhusiano wa kindoa.

Hali hiyo ilikuwa ya kawaida barani Afrika, ambapo mwanamume mmoja aliweza kuwa na wanawake zaidi ya mmoja, lakini kwa sasa inazidi kupungua.

Ya nadra zaidi ni hali ya wanaume kadhaa kuchanga mwanamke mmoja. Baadhi ya nchi zinakubali hali hiyo, lakini nyingi zinaikataza.

Vilevile baadhi ya dini zinakubali mitara, hususan Uislamu, lakini nyingine zinaikataza, hususan Ukristo. Katika Biblia tunakuta maendeleo ya ufunuo kuhusu hali hiyo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.

*******************************************

Katika utamaduni wa nchi nyingi uhusiano huo yaa ni wa NDOA ni kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu na unalenga ustawi wao na uzazi wa watoto katika familia.

Katika nchi nyingine inakubalika ndoa kati ya watu wawili ambao mmojawao ana au anaweza kuwa na mwenzi au wenzi wengine pia (mitara), hususan ndoa ya mwanamume mmoja na wanawake zaidi ya mmoja. Kumbe kwingine hilo ni kosa la jinai.

Mara nyingi harusi inafanyika kwa ibada maalumu kadiri ya dini ya wahusika.

PAMOJA NA MAELEZO YOOTE HAPO JUU, LENGO LIILIKUWA NI HILI.

MTANGAZAJI NA MTAYARISHAJI WA VIPINDI VYA RADIO LARVEN DAVID MASIKA WA MORNING STAR RADIO 105.3 FM AMBAYE PIA NI EDITOR KATIKA TANZANIA ADVENTIST MEDIA CENTRE NA NI FOUNDER WA ACACIA SING’ERS TAREHE 27, NOVEMBER, 2011 ALIAGA UKAPERA NA KUJITWALIA MKE AITWAYE PENDO.

BLOG YA MTAYARISHAJI INAMTAKIA MAISHA MAREFU NA YA FURAHA SIKU ZOTE HADI MUNGU ATAKAPOKUJA KUTUCHUKUA, HII NI CHANGAMOTO LAKINI NINAAMINI ATAWEZA KUKABILIANA NA KILA HALI ATAKAYOKUTANA NAYO. MUNGU NI MWEMA.Hakuna maoni:

Chapisha Maoni