Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Novemba 30, 2011

JERRY MURO HATMAYE

…hatimaye Mwandish wa habari Jeri Muro ameachiwa huru, mwandishi huyo aliyekuwa anafanya kazi TBC alikuwa anakabiliwa na kesi ya kudai rushwa...


Jerry Muro alipewa Tuzo na Wamarekani,.pia akapewa nafasi miezi sita kwenda Kwa mluo Obama, kituko;' wakambania pale Itv' nafasi yake'yake Dongo akamaindi akapiga mzigo'chini. Mtaalam Mhando Tido akaona wenzake Itv wamechezea Lulu akamkaribisha Tbc, habari ndio hiyo MEEN. Duh People wana data za watu hadi inatisha!!!



Hebu tujikumbushe jambo kuhusu namna alivyo PASUA JIPU - Part I



KUNA MISEMO TOKA KWA WATU MBALIMBALI KTK MITANDAO, NA NI YA KUITAFAKARI:

Kijana, litumikie Taifa lako kwa moyo wako woote, akili zako zoote na nguvu zako zoote. We are what we think. With our thoughts we make the world. Mwenye njaa hana masikioKunawa uso ni kufukuza usingizi kwa mda... " Masikini haishiwi NDOTO !!! "'' Mtu ni Utu sio Kitu''A Little Impatience can spoil great plan! Watcha gonna do when they come for you?






Jumatatu, Novemba 28, 2011

LARVENIE MASS...MWALIMU WA UIMBAJI NA EDITOR KTK MEDIA

Harusi ni sherehe kwa ajili ya kufunga ndoa. Ndoa ni muungano wa maisha yote kati ya watu wawili unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii yaani mwanamke na mwanamme.

*******************************************

Mwanaume ni binadamu wa kiume. Kwa kawaida ni mtu mzima anayeitwa hivi kwani wanaume wadogo huitwa watoto wa kiume tu au wavulana.

Wanaume ni takriban nusu ya binadamu, wengine huwa wanawake. Wanaume na wanawake ni jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.


*******************************************

Mwanamke ni mwanadamu wa jinsia ya kike. Kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau amebalehe. Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kike.

*******************************************

Mitara (au Upoli au Upali) ni hali ya watu zaidi ya wawili kuishi katika uhusiano wa kindoa.

Hali hiyo ilikuwa ya kawaida barani Afrika, ambapo mwanamume mmoja aliweza kuwa na wanawake zaidi ya mmoja, lakini kwa sasa inazidi kupungua.

Ya nadra zaidi ni hali ya wanaume kadhaa kuchanga mwanamke mmoja. Baadhi ya nchi zinakubali hali hiyo, lakini nyingi zinaikataza.

Vilevile baadhi ya dini zinakubali mitara, hususan Uislamu, lakini nyingine zinaikataza, hususan Ukristo. Katika Biblia tunakuta maendeleo ya ufunuo kuhusu hali hiyo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.

*******************************************

Katika utamaduni wa nchi nyingi uhusiano huo yaa ni wa NDOA ni kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu na unalenga ustawi wao na uzazi wa watoto katika familia.

Katika nchi nyingine inakubalika ndoa kati ya watu wawili ambao mmojawao ana au anaweza kuwa na mwenzi au wenzi wengine pia (mitara), hususan ndoa ya mwanamume mmoja na wanawake zaidi ya mmoja. Kumbe kwingine hilo ni kosa la jinai.

Mara nyingi harusi inafanyika kwa ibada maalumu kadiri ya dini ya wahusika.

PAMOJA NA MAELEZO YOOTE HAPO JUU, LENGO LIILIKUWA NI HILI.

MTANGAZAJI NA MTAYARISHAJI WA VIPINDI VYA RADIO LARVEN DAVID MASIKA WA MORNING STAR RADIO 105.3 FM AMBAYE PIA NI EDITOR KATIKA TANZANIA ADVENTIST MEDIA CENTRE NA NI FOUNDER WA ACACIA SING’ERS TAREHE 27, NOVEMBER, 2011 ALIAGA UKAPERA NA KUJITWALIA MKE AITWAYE PENDO.

BLOG YA MTAYARISHAJI INAMTAKIA MAISHA MAREFU NA YA FURAHA SIKU ZOTE HADI MUNGU ATAKAPOKUJA KUTUCHUKUA, HII NI CHANGAMOTO LAKINI NINAAMINI ATAWEZA KUKABILIANA NA KILA HALI ATAKAYOKUTANA NAYO. MUNGU NI MWEMA.



Jumamosi, Novemba 26, 2011

MAJIBU YAFANYAYO KAZI

Ukweli ni lengo la akili katika kujua mambo yote kwa dhati iwezekanayo.


Unaweza kujulikana kuanzia hisi kwa kufikiria, lakini pia kwa kushika imani ya dini fulani inayosadikiwa imefunuliwa na Mungu.


Wazo hilo ni la msingi hasa katika Ukristo, na kwa namna ya pekee katika Injili ya Yohane.


Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo tutatizama:

2011 General Conference Spring Council at Oakwood University (Full Sabbath Service)





MAJIBU YAFANYAYO KAZI NI KIPENGELE KINACHOONGELEA MASUALA YA KIROHO.

Jumatano, Novemba 23, 2011

TUJIKUMBUSHE UJASIRI WA DEMOKRASIA TARIME

UJASIRI WA KIDEMOKRASIA TARIME -Part 1




UJASIRI WA KIDEMOKRASIA TARIME -Part 2




UJASIRI WA KIDEMOKRASIA TARIME -Part 3





SOURCE:
http://phillipmogendi.com/documentary

Jumatatu, Novemba 21, 2011

…Bongoland YA Tanzania

Tanzania ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi, Rwanda na Uganda upande wa magharibi.

Nchini Tanzania kuna lugha za kikabila zaidi ya mia moja. Hakuna lugha rasmi ya sheria. Lakini Kiswahili ni lugha ya kitaifa ya Tanzania. Kiswahili kinatumika kama lugha baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo ya rasmi; kwa hiyo Kiswahili ni lugha rasmi ya dhati. Baada ya uhuru, Kiingereza (iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi, na kwa hiyo ilichukuliwa lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi wa rasmi wa Kiingereza imepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchugulia Kiswahili kama lugha rasmi ya dhati ya pekee.

Tanzania ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Mji mkuu: Dodoma, Makao makuu ya serikali: Dar es Salaam, miji mikubwa mingine: Mbeya, Arusha

Historia

Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)

Jina "Tanzania" limeundwa kutokana na majina ya TANganyika na ZANzibar (pamoja na athira ya jina la kale la "Azania").

Nchi hizo mbili zilikuwa zote chini ya utawala wa Uingereza hadi kupata uhuru lakini hazikuwa makoloni ya kawaida. Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Uingereza. Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa iliyoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.

Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti hadi 1964, zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza.

Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa.

Tarehe 21 Desemba 2005 Kikwete, Jakaya Kikwete ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa.

Tanzania ni moja kati ya nchi maskini duniani ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni katika mpango wa kusamehe madeni wa Kundi la Nchi Nane.


Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar:

Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata miundo ifuatayo:

  • Nchi inatawaliwa na serikali ya muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.
  • Tanganyika au Tanzania bara haina serikali au bunge la pekee
  • Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake zinazoratibu mambo yasiyo ya muungano.

Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa shughuli za muungano:

  • Mambo ya nje
  • Jeshi
  • Polisi
  • Mamlaka ya dharura
  • Uraia
  • Uhamiaji
  • Biashara ya nje
  • Utumishi wa umma
  • Kodi ya mapato, orodha
  • Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu

Demografia

Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kunaishi mtu mmoja tu kwenye kilomita moja ya mraba (1/km²) lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba. Zaidi ya asilimia themanini huishi vijijini. Dar es Salaam ni mji mkubwa kabisa wenye watu karibu milioni tatu.

Kuna makabila zaidi ya 120. Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya na Wamakonde.

Idadi kubwa sana ya Watanzania ni Wabantu. Nje ya hao, kuna Waniloti, kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome na Wasi. Kuna vikundi viwili vya Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; majina yao ni Wasandawe na Waburunge. Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika ya Kati.

Ingawa kila kabila lina lugha yake, lugha ya taifa ya Tanzania ni Kiswahili ambacho ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu. Hali hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu.


Dini

Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi halina msingi halisi bali ni zaidi azimio la kisiasa.

Waislamu hudai mara nyingi ya kwamba wenyewe ni sehemu kubwa ya Watanzania, angalau zaidi ya nusu. Kamusi ya "World Christian Encyclopedia" (2002) yataja Wakristo kuwa 52%, Waislamu kuwa 32% na wafuasi wa dini za jadi kuwa 14%.

Kwenye visiwa vya Zanzibar idadi ya Waislamu huaminiwa kuwa takriban 95%.

Usafiri

Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Mengine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani la Bahari Hindi kuna pia usafiri kwa meli.

Hadi sasa idadi ya barabara za lami si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es Salaam, Mbeya katika kusini-madharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina barabara nzuri na mawasiliano ni magumu.

Shirika mbili za reli zahudumia Tanzania ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali.

Huduma kwa ndege zatumia hasa nyanja za ndege 11 penye barabara ya lami kwa ajili ya ndege hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro /Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni.

Utamaduni

Sanaa

Kati ya wasanii wa Tanzania ni hasa wajume wa ubao na wachoraji waliojulikana kimataifa.

Mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii pia soko la nje.

Tangu miaka ya 1970 uchoraji wa "tingatinga" umejulikana uliopata jina kutoka kwa Edward Tingatinga naye mtu wa Umakonde.

Urithi wa Dunia

Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokelewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".

(mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali)

NIWIE RADHI, SABABU YA MAJUKUMU NDIO MAANA NIMEKUWA SIWEKI PACHIKO LA MARA KWA MARA. TATIZO HILO NIMELIMALIZA NA SASA KILA SIKU NITAKUWA NAKUWEKEA KITU KIPYA.