Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Oktoba 09, 2011

UTAMADUNI

Utamaduni Neno hili lina fafanuzi nyingi. Kwa mfano, mnamo mwaka 1952, Alfred Kroeber na Clyde Kluckhohn walikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno "utamaduni" katika kazi yao: Culture:a Critical Review of Concepts and Definitions. Hata hivyo, neno "utamaduni" linatumika kimsingi katika njia tatu zifuatazo:

  • Maonjo ya hali ya juu katika sanaa, vilevile hujulikana kama utamaduni wa juu.
  • Mkusanyiko wa maarifa ya kibinadamu, itikadi na tabia ambao hutegemea sana uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kiishara.
  • Ni jumla ya mitazamo, kaida, malengo na maadili yanayotambulisha asasi, shirika au kikundi Fulani.
Dhana hii ilipoibuka kwanza katika karne ya kumi na nane na kumi na tisa barani Ulaya, ilimaanisha mchakato wa kulima au kuboresha kilimo au kilimo cha mboga. Katika karne ya kumi na tisa dhana hii ilimaanisha kuboreshwa kwa mja kupitia kwa elimu na hali kadhalika ilimaanisha kutekelezwa kwa maazimio ya kitaifa au maadili. Katikati mwa karne ya kumi na tisa, wanasayansi wengine walitumia dhana ya utamaduni kurejelea uwezo wa kiubia wa binadamu.

Katika karne ya ishirini, "utamaduni" ilijitokeza kama dhana ya kimsingi katika somo la Anthropolojia. "Utamaduni" ulihusisha mambo yote yaliyomhusu binadamu ambayo hayakufungamana na matokeo ya kimaumbile. Dhana ya utamaduni katika Anthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili:Maoni 1 :