Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Oktoba 22, 2011

Neema Imani na Tumaini

Imani

Ingawa kwa Kiswahili neno imani lina maana mbalimbali (k.mf. "huruma"), ile kuu inahusiana na kitenzi kuamini, kinachofanana na kusadiki. Hapo ni kukubali ukweli wa jambo lisiloweza kuthibitishwa. Katika dini msingi wake ni mamlaka ya Mungu aliyeshirikishwa ukweli huo kwa njia ya ufunuo maalumu ili kumsaidia binadamu amjue yeye, ajifahamu pamoja na maisha yake duniani na ahera. Kwa msingi huo, au wa namna hiyo, mtu anaweza kushikilia jambo bila ya uthibitisho mwingine, ingawa pengine Ukristo unatia maanani pia akili katika ujuzi wa ukweli. Kadiri ya Mtume Paulo imani ikifuatana na tumaini na upendo ni adili kuu mojawapo, msingi, mzizi na chanzo cha wokovu.



Tumaini

Tumaini ni hali ya nafsi yenye matarajio mema kuhusu mambo yajayo. Katika dini linatokana hasa na imani. Ukristo, ukimfuata Mtume Paulo, unaliorodhesha pamoja na imani na upendo kati ya maadili yanayodumu.


Neema

Neema ni neno lenye maana mbalimbali, kama vile za kiroho na za kiuchumi, lakini zote zinaelekeza kumfikiria Mungu kama asili yake kuu. Teolojia katika dini mbalimbali inatumia neno hilo kadiri ya imani yake. Kwa namna ya pekee neno linatiwa mkazo katika Ukristo unaosisitiza kwamba yote ni neema. Hata hivyo madhehebu yake yanatofautiana sana katika kutafsiri tamko hilo.



Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Ninamaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Acappella wataimba wimbo uitwao Roll Jordan




Na George Frideric Handel, amallizie kwa - Messiah - The Trumpet shall sound




Ama The Cathedrals (ACAPELLA) ktk wimbo wao wa "Wonderful Grace Of Jesus"


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni