Teknolojia ya kwanza: Zana za Mawe
Kati ya mifano ya kwanza ya teknolojia ya kibinadamu ni matumizi ya mawe kama vifaa pamoja na matumizi ya moto. Tangu kupatikana kwa vifaa vya mawe wanahistoria wanahesabu kipindi hiki kama Zama za Mawe
Mifano ya vifaa vya kwanza ilivyopatikana pia Olduvai
Jinsi gani kutumia kifaa cha mawe
Kisu cha mawe iliyoboreshwa kiasi
Chaguo la visu vilivyoendelea (Marekani)
Mahali mbalimbali duniani penye mawe ya kufaa
wataalamu walitambua mabaki ya karahana ambako visu vya mawe vilitengenezwa kwa
vingi. Mfano mmojawapo ni bonde la Isimila karibu na Iringa, Tanzania ambako mabaki
mengi ya utengenezaji wa vifaa vimepatikana. Mafundi wa kale walipasua mawe na
kuyapigapiga hadi kupata visu vikali. Vipande vidogo vilivyokatwa pamoja na
visu visivyoridhika vilitupwa mahali pa kazi na hivyo wataalamu wamepata picha
ya kazi zilizotekelezwa. Kwa kutazama mabaki kama
yale ya Isimila katika pande zote za dunia inawezekana kupata picha ya
maendeleo ya teknolojia ya kutengeneza vifaa vya mawe kwa kupata visu vyembamba
na vikali zaidi. Karahana kama Isimila zinaonyesha uzalishaji kwa wingi kwa
hiyo ni dalili ya biashara maana wataalamu wanahisi visu hivi vilibadilishwa
kwa chakula au chumvi na watu walioishi katika sehemu pasipokuwa na mawe ya
kufaa.
Zama za Mawe hupangwa katika vipindi mbalimbali
kufuatana na maendeleo ya kuboreshwa kwa vifaa vya mawe ingawa mabadiliko haya
yalikuwa tofauti sana
kati ya maeneo mbalimbali. Kwa mfano tamaduni za Amerika zilitumia vifaa vya
mawe vyenye kiwango cha juu hadi kufika kwa Wazungu katika karne ya 16 ingawa menginevyo wenyeji hao
walikuwa na miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya na maendeleo mengine.
Maendeleo mengine wakati wa Zama za Mawe
Watu wa kwanza waliishi katika Afrika penye hali
ya hewa ya joto. Kadri walivyohama na kufika nchi baridi zaidi walihitaji mavazi ya kujikinga dhidi ya baridi. Inaaminiwa ya kwamba
mwanzoni ngozi za wanyama zilitumiwa kama
mavazi lakini rahisi kujua chanzo kamili kwa sababu tofauti na zana za mawe
ngozi au vitambaa vinaoza. Lakini kuna sindano za kushona zilizotengenezwa kwna
mifupa na ndovu zilizopatikana tangu miaka 30,000 KK.
Hakuna uhakika ufundi wa ufumaji
ulianza lini lakini kuna dalili katika makaburi ya kale zinazoonyesha uwezekano
ya kwamba ufumaji
ulianza kabla ya kilimo.
Hatua nyingine iliyotokea tangu milenia ya
mwisho wa Zama za Mawe ilikuwa ufinyanzi.
Mfano wa kale wa udongo uliofinyagwa na watu na kuchomwa motoni ni sanamu ndogo
za wanawake wanaoamiiwa kuwa ushahidi wa dini za kale. Mfano wa kale kanisa
limepatikana nchini Ucheki na kukadiriwa ulitengenezwa miaka 30,000 iliyopita
ingawa mifano ya vyombo vya ufinyanti kama
bakuli au chupa inapatikana tangu mwaka 1200 pekee.
Mapinduzi ya Kilimo
Tangu takriban mwaka 12,000 KK badiliko kubwa
lilitokea katika maisha ya watu walipogundua kilimo. Badiliko hili lilikuwa
harakati lililohitaji miaka mielfu likazidi kuenea polepole lakini
likabadilisha maisha na utamduni wa ubinadamu.
Hadi sasa kuna mahali pachache duniani palipogunduliwa
ya kwamba ni hapa watu walianza kulima. Kila mahali watu walianza kutambua
uwezekano wa kutunza mbegu za mimea na kuzipanda tena na kuvuna palepale
walipopanda; upande mwingine ulikuwa uwezo wa kufuga wanyama badala ya
kuwavinda tu.
Hasa ujuzi wa kupanda mbegu ulisababisha
badiliko kubwa la maisha. Tangu kugundua mbinu huu watu hawakuhitaji tena
kuhama wakifuata windo na hali ya hewa lakini walipokuta ardhi njema waliweza
kupanda na kuvuna na kukaa mahali pamoja. Hatua hii ilikuwa chanzo cha makazi
ya kudumu na vijiji na miji
ya kwanza.
Ukifika mkoani Iringa, kuna eneo
lenye mabaki ya mawe mfano wa sawa na ulioyaona hapo juu. Historia inasimuliwa
na wenyeji pamoja na watunzaji wa eneo hilo
kuwa:
Hayo mawe inaonesha ndio yaliyokuwa
yanatumiwa na watu wa kale.
Mimi nilienda huko mwaka huu
nikajionea, post ijayo nitakuwekea picha…
...baadae tena mdau.
Asante kwa shule hii Mkuu!
JibuFuta