Mtayarishaji

Morning Star Radio

Ijumaa, Oktoba 14, 2011

Makala Kuhusu Mapendo au Mapenzi.



...Leo nimeingilia fani za watu AISEE.

Neno "kupenda" linaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ("Napenda chakula hicho"), hadi mvuto mkali kati ya watu ( "Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi wa dhana hii, hata ikilinganishwa na hali zingine za kihisia.

Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba na ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usiohusisha ngono hadi umoja wa kina au ibada ya upendo] wa kidini.

Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamu na, kutokana na umuhimu wake mkuu wa kisaikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika sanaa.

Ufafanuzi

Neno la Kiingereza "love" linaweza kuwa na maana tofauti, lakini zinazohusiana, katika miktadha tofauti. Mara nyingi, lugha nyingine hutumia maneno mbalimbali kueleza baadhi ya dhana tofauti ambazo lugha ya Kiingereza hutumia neno "love" kurejelea; mfano mmoja ni wingi wa maneno ya Kigiriki yanayorejelea "mapendo". Tofauti za utamaduni katika kufafanua mapenzi hivyo, hufanya liwe jambo gumu kuanzisha ufafanuzi bia wowote.

Ingawa desturi au chanzo cha mapenzi ni suala ambalo hujadiliwa mara kwa mara, sura tofauti ya neno hili zinaweza kuwekwa wazi kwa kuamua ni nini ambacho sio mapenzi. Kama njia ya kawaida ya kuonyesha hisia chanya (aina kubwa ya kupenda), mapenzi kwa kawaida hulinganuliwa na chuki (au kutojali); kama upendo ambao umegemea zaidi kwenye uhusiano wa kirafiki kuliko wa kingono, mapenzi kwa kawaida hulinganuliwa na tamaa, na kama uhusiano kati ya watu, unaohusisha mahaba, mapenzi hulinganuliwa na urafiki, ingawa fdesturi zingine za neno mapenzi zinaweza kutumika kwa urafiki wa karibu katika miktadha fulani.

Wakati yanapojadiliwa katika hali dhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea upendo kati ya watu, hisia alizo nazo mtu kuhusu mtu mwingine. Mapenzi mara nyingi yanahusisha kutunza au kujiainisha na mtu au kitu, ikiwa ni pamoja na nafsi ya mtu.


Aidha, katika tofauti za-kiutamaduni katika kuelewa mapenzi, mawazo kuhusu mapenzi pia yamebadilika sana na mpito wa wakati. Baadhi ya wanahistoria wanahusisha dhana za kisasa za mapenzi ya kimahaba na Ulaya wakati au baada ya enzi ya kati, ingawa kuwepo kwa mahusiano ya kimahaba kabla ya wakati huo kunaonyeshwa na ushairi wa kimapenzi wa kale.

Kutokana na utata na udhahania wa mapenzi, mjadala juu ya mapenzi kwa kawaida hupunguzwa hadi maneno yaliyopitwa na wakati, na kuna mithali kadhaa kuhusu mapenzi, mojawapo ikiwa ile ya Vergilio ya kuwa "Pendo hushinda yote" na ile ya Beatles "All you need is love" (Unachohitaji ni mapenzi tu). Bertrand Russell anaelezea mapenzi kama hali ya "thamani kamili", kinyume na thamani inayobadilika. Mwanafalsafa Gottfried Leibniz alisema kwamba mapenzi ni "kuwa na furaha tele kutokana na furaha ya mwingine."



Mapenzi yasiyohusishwa na mtu maalum

Mtu anaweza kusemekana kuwa anapenda nchi, kanuni, au lengo ikiwa anaithamini sana na kuizingatia kwa makini. Vilevile, mapenzi ya huduma za huruma na wafanyakazi wa kujitolea ' "upendo" ya kazi yao yanaweza kutokana na mapenzi yasiyohusishwa na kitu pamoja na utu na imani za kisiasa badada ya mapenzi kati ya watu. Watu pia wanaweza "kupenda" vitu, wanyama, au shughuli ikiwa wao wenyewe watajitolea kutagusana au kwa vinginevyo kujihusisha na vitu vile. Ikiwa tamaa ya kingono pia inashirikishwa, hali hii inaitwa 'paraphilia'.

Mapenzi kati ya watu

Mapenzi kati ya watu wawili ni hisia za nguvu kuliko kumpenda mtu mwingine kwa jumla.
Mapenzi yasiyotuzwa ni hisia za mapenzi ambazo haziwezi kulipizwa au kurudishwa. Mapenzi kama haya yanaweza kuwepo kati ya wanafamilia, marafiki, na wanandoa. Pia kuna matatizo kadhaa ya kisaikolojia yanayohusiana na mapenzi.


Katika historia, falsafa na dini ndizo taaluma ambazo zimewaza sana kuhusu suala la mapenzi. Katika karne iliyopita, sayansi ya saikolojia imeandika mambo mengi juu ya suala hili. Katika miaka ya karibuni, sayansi za saikolojia ya mabadiliko, biolojia ya mabadiliko, anthoropolojia, sayansi ya nyuro na biolojia zimezidisha ufahamu juu ya mapenzi.

Msingi wa kikemikali

Maumbo ya kibiolojia ya jinsia huona mapenzi kama hisia za mamalia, kama vile njaa au kiu. Helen Fisher, mtaalamu mashuhuri katika mada ya mapenzi, amegawanya mapenzi katika sehemu tatu zinazolingana: tamaa, mvuto na upendo. Tamaa huwafunua watu kwa wengine; mvuto wa kimahaba huwahamasisha watu kuzingatia nishati yao kwa kuhusiana kingono; na upendo unahusisha kustahimili mwenzako (au mtoto) kwa muda wa kutosha wa kumlea hadi uchanga.

Tamaa ni hamu ya mwanzo ya ngono ambayo hukuza uhusiano kingono, na inahusisha kutolewa kwa wingi kwa kemikali kama vile 'Testosterone' na 'estrogen'. Athari hizi huwa hazikai kwa muda uliopita wiki chache au miezi michache. Upendo ni hamu ya kibinafsi na kimahaba zaidi inayoelekezwa kwa mgombea maalum wa kuhusiana kingono, ambayo hutokana na tamaa wakati wajibu kwa mgombea huyo mmoja unakua.


Utafiti uliofanywa hivi karibuni katika Sayansi ya nyuro umeonyesha kuwa jinsi watu wanavyoendelea kupendana, ubongo huwa unatoa aina fulani za kemikali, ikiwa ni pamoja na 'pheromones', 'dopamine', 'norepinephrine', na 'serotonin', ambayo hufanya kazi sawa na 'amphetamines', kuchochea kiini cha furaha kwenye ubongo na kusababisha madhara kama vile kuongezeka kwa mpigo wa moyo, kupoteza hamu ya kula na kulala, na hisia kali za msisimko. Utafiti umeonyesha kwamba hatua hii kwa jumla hudumu kwa muda wa mwaka moja na nusu hadi miaka mitatu.

Kwa kuwa hatua za tamaa na mvuto huendelea kwa muda tu, hatua ya tatu inahitajika ili kuelezea mahusiano ya muda mrefu. Upendo ni maingiliano ambayo hukuza mahusiano ya kudumu kwa miaka mingi na hata miongo. Upendo kwa jumla umejengwa kwenye wajibu kama vile ndoa na watoto, au kuheshimiana kirafiki kulikojengwa kwenye mambo kama vitu mnavyovipenda. Upendo umehusishwa na kuwepo kwa viwango vya juu vya kemikali 'oxytocin' na 'vasopressin' ikilinganishwa na mahusiano ya muda mfupi.

Enzo Emanuele na wenzake walieleza kuhusu kuripotiwa kwa molekuli ya protini inayojulikana kama kipengele cha ukuaji wa neva (nerve growth factor) (NGF) ina viwango vya juu wakati watu wanaanza kupendana, lakini viwango hivi kurudi kwenye vipimo vya awali baada ya mwaka mmoja.



Msingi wa kisaikolojia

Saikolojia inaonyesha mapenzi kama jambo tambuzi na la kijamii. Mwanasaikolojia Robert Sternberg alibuni nadharia ya miraba mitatu ya mapenzi na akasema kuwa mapenzi yana vipengele tatu tofauti: urafiki, kujitoa, na uchu. Urafiki ni aina ambayo watu wawili huambiana siri na mambo kadhaa kuhusu maisha yao binafsi, na kwa kawaida hudhihirika katika urafiki na mahusiano ya kimahaba. Kuwajibika, kwa upande mwingine, ni matumaini kuwa uhusiano huo ni wa kudumu.


Aina ya mwisho na inayopatikana sana ya mapenzi ni mvuto kingono na uchu. Mapenzi ya uchu ni kama yanavyoonyeshwa katika kupumbazwa kimapenzi pamoja na mapenzi ya kimahaba. Aina zote za mapenzi hutazamwa kama mchanganyiko tofauti wa vipengele hizi vitatu. Mwanasaikolojia kutoka Marekani, Zick Rubin anajaribu kufdesturi mapenzi kwa saikrometiki. Kazi yake inasema kuwa mapenzi yamejengwa na vipengele vitatu: upendo, kujali na urafiki.

Kufuatia maendeleo katika nadharia za umeme kama vile sheria ya Coulomb, ambayo ilionyesha kuwa nguvu chanya na hasi huvutiana, milinganisho katika maisha ya binadamu ilifanywa, kama vile "vinyume kuvutiana." Katika karne iliyopita, utafiti juu ya desturi ya mahusiano ya kingono miongoni mwa binadamu umepata kwa jumla kuwa jambo hili si kweli kukija ni tabia na utu-watu kwa kawaida kuwapenda wale walio na sifa zinazofanana na zao.


Hata hivyo, katika miliki chache zisizo za kawaida na maalum, kama vile mifumo ya kinga, inaonekana kwamba binadamu hupendelea binadamu wengine ambao ni tofauti wao (mfano, walio na mfumo wa orthojoni), kwa kuwa jambo hili litasabbaisha kupata mtoto ambaye ana sifa bora za pande zote mbili. Katika miaka iliyopita hivi karibuni, nadharia mbalimbali za maingiliano ya binadamu zimebuniwa, na kuelezewa kwa kuzingatia upendo, mahusiano, maingiliano, na mivuto.

Baadhi ya mamlaka ya Magharibi hugawanywa katika vipengele viwili vikuu, chenye utu na chenye kujipenda. Mtazamo huu umewakilishwa katika kazi ya Scott Peck, ambaye kazi yake katika uwanja wa saikolojia ya matumizi ilitafiti fafanuzi za mapenzi na maovu. Peck anasema kuwa mapenzi ni mchanganyiko wa "wasiwasi kuhusu ukuaji kiroho wa mwingine," na kujipenda sahili. Kwa pamoja, mapenzi ni shughuli, si hisia tu.

Ulinganifu wa mifumo ya kisayansi

Mifumo ya kibIolojia ya mapenzi huyatazama kama msukumo wa kimamalia, sawa na njaa au kiu. Saikolojia hutazama mapenzi kama jambo linaloegemea zaidi kwa jamii na utamaduni. Pengine kuna dalili za kweli katika mitazamo yote miwili. Hakika mapenzi huathiriwa na homoni (kama 'oxytocin', 'neurotrophins', NGF na 'pheromones'), na jinsi watu hufikiri na kutenda katika mapenzi huathiriwa na mawazo yao kuyahusu.

Mtazamo wa kawaida katika biolojia ni kwamba kuna misukumo miwili makuu katika mapenzi: mvuto wa kingono na upendo. Upendo kati ya watu wazima huchukuliwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni sawa na zile zinazomfanya mtoto mchanga kumpenda mama yake. Mtazamo wa jadi wa kisaikolojia huangalia mapenzi kama anaona kuwa muungano wa mapenzi ya kimwenzi na mapenzi ya kiuchu. Mapenzi ya kiuchu ni hamu kubwa, na mara nyingi huandamana na mwamsho wa kimwili (kupumua kwa nguvu, mpigo wa moyo wa kasi); mapenzi ya kimwenzi ni mapenzi na hisia za kirafiki zisizoandamana na mwamsho wa kimwili.

Uchunguzi umeonyesha kuwa ubongo wa waliopumbazwa na mapenzi unafanana na ule wa wale wenye ugonjwa wa akili. Mapenzi huanzisha shughuli katika eneo la ubongo sawa na njaa, kiu, na hamu ya madawa. Mapenzi mpya, kwa hiyo, yanaweza kuegemea kwenye upande wa kimwili kuliko kihisia. Kadri wakati unavyopita, athari hizi zinazotokana na mapenzi hukomaa, na maeneo mbalimbali ya ubongo ni yanaamshwa, hasa yale yanayohusiana na ahadi za muda mrefu.
.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni