Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Oktoba 12, 2011

BUSARA




Busara ni mojawapo kati ya maadili bawaba yaliyotambulikana na wanafalsafa wa Ugiriki. Ndiyo adili linalofanya akili izingatie kwa makini hali halisi ili kutambua yaliyo mema na kuchagua njia ya kufaa kuyafikia.

Aristotle alifuatwa na Thoma wa Akwino akisema busara ndiyo kanuni nyofu ya utendaji. Adili hilo halichanganyikani na woga unaomzuia mtu asitende inavyotakiwa, wala na ujanja unaotumia undumakuwili na ulaghai.

Kwa Kilatini inaitwa «auriga virtutum – dreva wa maadili», kwa kuwa inatakiwa kuongoza utekelezaji wa maadili mengine yote ikiyaonyesha kanuni na kiasi. Busara ndiyo inayoongoza uamuzi wa dhamiri. Mwenye busara anatenda kufuatana na uamuzi huo.

Kwa njia ya busara tunatumia kwa hakika misimamo ya kiadili katika nafasi mbalimbali na kuondoa wasiwasi kuhusu la kutenda. Muone huyu http://simon-kitururu.blogspot.com/ anavyofafanulia zaidi.

Hakuna maoni: