Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Agosti 23, 2011

UMASKINI...SURA HALISI.

Umaskini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya binadamu ya msingi kama vile chakula, maji masafi, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara. Umaskini wa kadri ni wa kuwa na raslimali chache zaidi au mapato madogo zaidi ikilinganishwa na watu wengine katika jamii au nchi au ikilinganishwa na hali ya kadiri duniani. Hali hii pia hujulikana kama umaskini halisi au unyonge.

Umaskini linganishi ni hali ya kuwa na rasilimali chache au kipato cha chini kuliko wengine kwenye jamii au nchini, au ikilinganishwa na wastani duniani kote. Asili ya umaskini unajihusisha hasa na sababu zinazosababisha kiwango cha chini cha utajiri na uzalishaji cha watu maskini au, ikisemwa vingine, uhaba na mfumuko wa bei ya bidhaa ambazo wanazitumia.

Picha hii imebuniwa na kusanifiwa na: Celestin Kimaro. Mtembelee katika FaceBook.


Vikwazo kwa uzalishaji

Ukosefu wa hiari wa serikali na watu wa tabaka la juu kuwapa wapangaji wao haki kamili ya kumiliki ardhi imetajwa kama kikwazo kikuu kwa maendeleo. Ukosefu wa uhuru wa kiuchumi ni kizingiti kikubwa kwa ujasiriamali kwa watu maskini [3] Biashara mpya na wawekezaji kutoka nchi za nje wanaweza kufukuzwa kutokana na kuwepo kwa taasisi zinazoongozwa vibaya, hasa kutokana na ufisadi, udhaifu wa sheria na vikwazo vingi vya kiurasimu.

Nchini Kanada, itamchukua mwanabiashara siku mbili, hatua mbili za kiurasimu na Dola 280 kufungua biashara ilhali mfanyibiashara nchini Bolivia analazimishwa kulipa Dola 2,696 kama ada, angojee siku 82 za kazi, na apitie hatua 20 ili kufanya jambo lile lile Vikwazo vikuu kama hivi hufaidi zaidi biashara kubwa na kuzidhoofisha biashara ndogo, ambako idadi kubwa ya nafasi za kazi huundwa Nchini India kabla ya mabadiliko ya kiuchumi, wenye biashara walipaswa kuwahonga wafanyikazi wa serikali ili wafanye kazi zao za kila siku, na ilikuwa kama ushuru kwenye biashara yao.

Ufisadi, nchini Nigeria, kwa mfano mapato yanayotokana na uuzaji wa mafuta yanayokadiriwa kuwa Dola Bilioni 400 yameibiwa na viongozi wa Nigeria kati ya 1960 na 1999 Ukosefu wa nafasi pia unaweza kusababishwa na serikali kutojenga miundomisingi bora. Nafasi bora zaidi za kazi katika mataifa tajiri zaidi husababisha watu wenye vipawa maalum kuhama, na hivyo kuwapoteza wataalamu.



Kupotea huku kunaligharimu bara la Afrika zaidi ya Dola bilioni 4 zinazotumika kuajiri kazi zaidi ya wataalamu 150,000 kutoka nchi za ng’ambo kila mwaka. Wanafunzi wa India wanaoenda ng’ambo kuendelea na masomo yao huigharimu nchi yao mapato yanayotokana na fedha za kigeni yanayofika Dola bilioni 10 kila mwaka

Afya duni na ukosefu wa elimu nafuu huathiri vibaya uzalishaji. Ukosefu wa chakula cha kutosha utotoni huathiri uwezo kamili wa mtu wa kukua na kutumia vipawa vyake. Ukosefu wa madini muhimu kama vile aidini na chuma unaweza kuzuia kukua kwa ubongo. Watu bilioni mbili (theluthi moja ya watu wote duniani) wameathiriwa na ukosefu waiadinimwilini.

Katika mataifa yanayoendelea, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya watoto wenye umri wa miaka minne na chini wana ugonjwa wa anemia kutokana na ukosefu wa madini ya chuma katika chakula chao Tazama pia Afya na werevu. Vile vile matumizi mabaya ya madawa kwa mfano ulevi wa pombe wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya yanaweza kuwaweka watu katika hali ya umaskini unaoendelea




Upungufu wa mahitaji ya kimsingi

Kupanda kwa gharama ya maisha kunawafanya maskini wawe maskini zaidi. Kiwango kikubwa cha bajeti za watu maskini hutumika kununua chakula ikilinganishwa na matajiri. Kutokana na jambo hili, jamii za watu maskini na wale wanaopakana na umaskini huathiriwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la bei ya vyakula Kwa mfano, mwishoni mwa mwaka 2007 kupanda kwabei ya nafaka kulizua rabsha s katika mataifa kadhaa.

Benki ya Dunia ilionya ya kuwa watu milioni 100 walikuwa na hatari ya kuwa maskini zaidi. Ukame na uhaba wa maji pia vinaweza kuwa tishio kwa usambazaji wa chakula. Kulima mashamba majira baada ya majira humaliza rotuba ya udongo na mwishowe hupunguza mazao ya kilimo. Inakadiriwa ya kuwa asilimia 40 ya mashamba duniani yameharibika vibaya.

Barani Afrika, ikiwa mwenendo huu wa kuharibika kwa udongo utaendelea, bara hilo litaweza kulisha asilimia 25 pekee ya watu wanaoishi humo kufikia mwaka wa 2025. Hii ni kulingana na Chuo Kikuu cha Umoja wa MataifaInstitute for Natural Resources in Africa, chenye makao yake nchini Ghana.

Watu maskini hawapati Huduma za afya kwa urahisi. Uhamaji wa wafanyikazi wanaotoa huduma za afya kutoka nchi maskini kumeathiri vibaya nchi hizo. Kwa mfano, wauguzi 100,000 kutoka Ufilipino walihama kati ya 1994 na 2006. [31] Kuna madaktari Wahabeshi wengi zaidi mjini Chicago kuliko wale walio Uhabeshi. [mtajo wa maneno unahitajika][

Ongezeko la idadi ya watu na ukosefu wa huduma za kupanga uzazi.[ufafanuzi unahitajika] Kigezo:Clarify Ni vyema kutambua ya kuwa watu huongezeka kwa upole au hata idadi yao inaweza kupunguka. Hii inatokana na mabadiliko kama vile kiwango cha vifo na kiwango ya waliozaiwa na jinsi zinavyoathiri idadi ya watu


Athari za umaskini

Athari za umaskini pia zinaweza kuwa vyanzo, kama ilivyoorodheshwa hapo juu, na hivyo kuunda “mzunguko wa umaskini” unaodhihirika katika ngazi mbalimbali: ya kibinafsi, ya kimtaa, kitaifa na kimataifa.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni