Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Agosti 20, 2011

NABII

Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.

Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).

Watu wa namna hiyo wanapatikana katika dini nyingi, hususan katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.Ellen G.White

Katika Uyahudi

Katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) tunakuta vitabu vingi vinavyojumlishwa katika jina "manabii", kuanzia Yoshua hadi Malaki. Katika Ukristo baadhi ya vitabu hivyo vinahesabiwa kuwa "vitabu vya historia", kumbe kile cha Danieli kinapangwa kati ya "manabii wakuu" pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli, wakati Wayahudi wanacho kati ya "maandiko (mengine)".

Katika Ukristo

Ukristo unakubali manabii wote wa Agano la Kale, lakini upande wa Agano Jipya ni wachache wanaoitwa hivyo, kwa mfano Agabo anayetajwa katika Matendo ya Mitume.

Kwa jumla ni kwamba Wakristo wote wanahesabiwa kuwa manabii kutokana na wajibu wa kutangaza Neno la Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.Muhammad
www.unreasonablefaith.com

Katika Uislamu

Katika Islam mtume Muhammad anapewa nafasi ya pekee kati ya manabii wengi waliotumwa na Mungu kwa binadamu wa nyakati na mahali tofauti. Ndiye anayesadikiwa na Waislamu wengi kuwa nabii wa mwisho na wa kudumu ("mhuri wa manabii" - khātim al-nabiyyīn (Kurani, XXXIII:40).

Uislamu unakubali manabii wa Biblia pamoja na wengine wasiotajwa katika kitabu hicho, kama vile Mwarabu Salih.


Katika dini nyingine

Dini nyingine zinatokana na mafundisho ya mtu anayehesabiwa nabii:

*************************************************

Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe.

Maoni 1 :