Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Agosti 15, 2011

KOLONI

Koloni zilikuwa njia ya kueneza utawala wa nchi au taifa tangu enzi ya Wagiriki na Waroma wa kale. Asili ya neno koloni ni kilatini "colonia" inayotokana na kitenzi "colere" (kulima, pia kuabudu). Colonia ilikuwa makazi ya Waroma wa Kale nje ya eneo lao la awali. Chanzo chake kilikuwa mji mpya uliokaliwa na wanajeshi wastaafu waliopewa ardhi ya shamba kama pensheni yao. Koloni za aina hii zilianzishwa hasa mpakani wa maeneo mapya yaliyotwaliwa karibuni na kuingizwa katika Dola la Roma. Walowezi walipewa mashamba yao kwa masharti ya kuwa tayari kutetea mipaka kama vita ikitokeaHata kama neno "koloni" lilitokana na lugha ya Kilatini Waroma wa Kale hawakuwa watu wa kwanza waliounda koloni walifuata nyayo za mataifa yaliyotangulia kama Wagiriki wa Kale au Wafinisia.

Miji ya Wagiriki au Wafinisia ilikuwa miji ya biashara kando la bahari. Walianzisha koloni-miji mpya hasa wakati idadi ya watu katika mji mama iliongezeka mno kulingana na eneo la mji huu. Badala ya kutwaa maeneo majirani barani walitafuta mahali mapya ufukoni kwa bahari pasipo na wakazi wengi nje ya eneo lao kwa sababu usafiri kwa jahazi ulikuwa rahisi kuliko kujenga barabara barani.

Hivyo Wagiriki waliunda miji mipya katika Italia ya kusini au kwenye pwani za Bahari Nyeusi. Miji mingi ya Italia ya kusini inaonyesha hadi leo jina lenye asili ya Kigiriki kwa mfano Napoli iliyokuwa "Νεάπολις" (nea polis = mji mpya)


Wafinisia waliunda miji mipya katika Afrika ya Kaskazini na Hispania. Koloni-mji mashuhuri ya Wafinisia ilikuwa Karthago.

"Colonia" za aina hii zilianzishwa na Waroma wa kale katika maeneo yaliyotwaliwa nao karibuni kwa shabaha ya kurahisisha usimamizi wa maeneo mapya. Wanajeshi wastaafu walipewa ardhi kama shukrani kwa huduma yao pamoja na masharti ya kwamba watakuwa tayari kutetea eneo kama vita ikitokea tena.

Koloni za aina ziliundwa awali ndani ya Italia wakati wa upanuzi wa utawala wa mji wa Roma juu ya rasi yote. Baadaye koloni zilianzishwa pia nje ya Italia kwa mfano Gallia, Germania, Britania, Uyahudi au Afrika ya Kaskazini.

Miji kadhaa ya kisasa iliyoundwa na Waroma inatunza neno la kilatini "colonia" hadi leo ndani ya umbo la majina yao:

  • Köln nchini Ujerumani ilianzishwa kama "Colonia Ara Agrippensis" na jina lake la leo ni badiliko la neno "colonia".
  • Colchester katika Uingereza ulikuwa na jina la Kiroma la "Colonia Claudia Victricensis". Silabi ya kwanza ni mabaki ya neno la Kiroma.
  • Lincoln katika Uingereza iliitwa "Lindum Colonia" na jina la leo ni namna ya kufupisha jina la kale.


Maoni 1 :