Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Agosti 13, 2011

MAISHA NA UJUMBE WAKE HUSABABISHA MABADILIKO...MAJIBU YAFANYAYO KAZI (THE SPRING INTO PRAISE MASS CHOIR)

Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako hapa duniani na ya milele yanaguswa na jibu lako kwa swali hili?

  • Mtu wa ajabu kupita watu wote katika nyakati zote?

  • Nani aliyejitokeza kuwa mtu mashuhuri kwa vipindi vyote?

  • Kiongozi mkuu?

  • Mwalimu mkuu?

  • Mtu aliyefanya matendo mema kwa wanadamu kupita mwingine?
  • Mtu aliyeishi maisha matakatifu kuliko yeyote aliyewahi kuishi?BWANA ANAYEISHI:
Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, wanafuasi wake wa kweli hawafuati tu orodha za mwanzilishi aliyekufa, bali wanauhusiano wa karibu na wakibinafsi na bwana aliyehai. Yesu Kristo yuhai leo na anabariki na kuimarisha maisha ya wote wanaomwamini na kumtii. Katika enzi zote, wengi wamedhihirisha kufa kwake Yesu Kristo, kati yao wakiwa watu waliotenda makuu ulimwenguni.

Mwanafizikia na mwanafalsafa wa Kifaransa Blaise Pascal alisema jinsi mwanadamu anavyomhitaji Yesu aliposema, "Kuna pengo katika moyo wa kila mwanadamu linayoweza kuzibwa na Mungu peke yake kupitia Mwana wake Yesu Kristo."

Je, ungependa kumjua Yesu Kristo kama Mwokozi wako? Unaweza! Yesu anahamu ya kuanza uhusiano wa kibinafsi uliojaa upendo kwako. Ameshafanya matayarisho yote.Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia tabaka za dini zao, kama wanajua chochote kuhusu historia, watakubali kwamba hakujawahi kuwa na mtu kama Yesu wa Nazareti. Yeye ni mtu wa ajabu mno kuliko watu wote wa enzi zote.

Yesu alibadilisha mwenendo wa historia. Hata tarehe kwenye gazeti lako la leo inathibitisha kwamba Yesu wa Nazareti aliishi ulimwenguni karibu miaka 2,000 iliyopita. Maandishi kwa Kiingereza "B.C." yanasimamia nyakati kabla ya kuzaliwa kwa Kristo; vilevile maandishi "A.D." yanasimamia nyakati baada ya kuzaliwa kwa Kristo.KUJA KWAKE KULITABIRIWA

Mamia ya miaka hata kabla ya Yesu kuzaliwa, maandiko yaonyesha wanabii wa Israeli wakitabiri kuja kwake. Agano la kale, lililoandikwa na watu wengi katika muda wa miaka 1,500, lina unabii zaidi ya 300 kuhusu kuja kwa Yesu. Yote yaliyotabiriwa yalitendeka, pamoja na kuzaliwa kwake kimiujiza, maisha yake matakatifu, kufa na kufufuka kwake.

Maisha aliyoishi Yesu, miujiza aliyotenda, maneno aliyosema, kufa kwake msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake mbinguni - yote yathibitisha kwamba yeye hakuwa mwanadamu peke yake bali alikuwa zaidi ya mwanadamu. Yesu alisema, "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30), "Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:9) na, "Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana 14:6).

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:
MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.

Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...

(Namaanisha JumaMosi)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo

Bruce N. Seawood & Dr. Carlton P. Byrd

Anapotwambia:

THE SPRING INTO PRAISE MASS CHOIR


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni