Mfumo wa jua na sayari zake ni utaratibu wa jua letu na sayari au sayari kibete zinazolizunguka pamoja na miezi yao, asteroidi, meteoridi, kometi na vumbi ya angani yote ikishikwa na mvutano wa jua.
Kwa kawaida huhesabiwa sayari 9 zinazozunguka jua. Lakini miaka ya nyuma magimba makubwa yamegunduliwa angani ambayo bado hayakukubaliwa kama yahesabiwe kuwa sayari au aina ya asteoridi.
Orodha inayofuata bado inahitaji kuangaliwa kwa sababu kuna tofauti kati ya kamusi na vitabu mbalimbali jinsi ya kutaja sayari fulani.
Sayari katika mfumo wa jua ni zifuatazo:
Namba zote zinazotaja sifa mbalimbali za sayari zinaonyesha kipimo kulingana na tabia za dunia yetu kuwa "1". Kuhusu majina ya sayari kadhaa kuna mchanganyiko katika kamusi na vitabu. Pale ambako jina au umbo tofauti la jina ni kawaida linaonyeshwa katika mabano kama (jina). Majina yanayotumiwa katika vitabu kadhaa bila kuwa na uhakika yanaonyeshwa katika mabano ya italiki pamoja na alama ya swali kama (? jina).
Jina la sayari | Masi | Nusukipenyo ya mzingo wa kuzunguka jua | Muda wa mzingo | Kuinama kwa mzingo wa kuzunguka jua | Muda wa siku ya sayari | ||
Utaridi (Zebaki)* | 0.382 | 0.06 | 0.387 | 0.241 | 7.00 | 58.6 | 0 |
Zuhura (Ng'andu)** | 0.949 | 0.82 | 0.72 | 0.615 | 3.39 | -243 | 0 |
Dunia (Ardhi)*** | 1.00 | 1.00 | 1.00 | 1.00 | 0.00 | 1.00 | 1 |
0.53 | 0.11 | 1.52 | 1.88 | 1.85 | 1.03 | 2 | |
Mshtarii (? Sumbula) | 11.2 | 318 | 5.20 | 11.86 | 1.31 | 0.414 | 63 |
Zohari (Zohali) (? Sarateni) | 9.41 | 95 | 9.54 | 29.46 | 2.48 | 0.426 | 49 |
Uranus (? Zohali) | 3.98 | 14.6 | 19.22 | 84.01 | 0.77 | -0.718 | 27 |
Neptun (? Kausi) | 3.81 | 17.2 | 30.06 | 164.8 | 1.77 | 0.671 | 13 |
Pluto (? Utaridi)**** | 0.18 | 0.002 | 39.5 | 248.5 | 17.1 | -6.5 | 3 |
Utaridi ni jina la sayari ya kwanza kutokana na lugha ya Kiarabu. Vitabu vingine hutumia neno "Zebaki" ni pia neno lenye asili ya Kiarabu linalomaanisha metali; inaonekana limepatikana kama tafsiri ya jina la Kiingereza la sayari ya kwanza "Mercury" bila kujua historia ya majina ya sayari sita ya kwanza yaliyoingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiarabu. |
- ↑ Linganisha ukuasa wa majadiliano:sayari
- ↑ kuhusu majina ya sayari zilizojulikana kwa Waswahili na hivyo kuwa na majina ya asilia linganisha Jan Knappert, Swahili Islamic poetry, Brill 1971, Vol 1 uk 96-97 - taz google booksearch
UPO…???
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni