Niliitembelea hiyo Blog ya huyo muandaaji wa Tunzo sijui Tuzo na kuacha comments za kutaka kueleweshwa zaidi, soma nilichoandika na jibu lililotolewa.
Mcharia on May 13, 2011 2:26 PM said...
Ni mara yangu ya kwanza kupita hapa, na ni kutokana na blog hii http://changamotoyetu.blogspot.com/ ambayo nilikuta imeandika habari kuhusu BLOG AWARDS.
Hata hivyo sina hakika kuwa mnazifahamu blog zote kama lengo ni kwa zile zinazoandika kwa kiswahili.
Anyway, hongera kwa kufikiria jambo hili ila naamini mtanisaidia maana niliwahi ona machapisho yanayohusu umoja wa bloger na nikaona pia walitunga na katiba.
SWALI:
Huo umoja upo au...
Unafanyaje kazi na unapatikanaje.
Ni nani wanaopaswa kujiunga.
Nipo hapa; www.mtayarishaji.blospot.com
Ahsante.
MAJIBU YA HUYO MUANDAAJI WA TUZO SIJUI TUNZO. HAPA NANUKUU:
Admin on May 13, 2011 7:52 PM said...
Asante na karibu sana. Blog zinazowekwa hapa tunaletewa na watu na zingine tunatafuta wenyewe. Hili shindano ndio limeanza na tuna kama week tatu tu. Hivyo bado tunajitahidi kutafuta blog ambazo hatujaweza kuzipata basi tuziweke humu. Na blog hizo sio lazima ziandikwe kwa kiswahili bali ziwe zimeandikwa na Mtanzania yeyote pale alipo ulimwenguni. Mtanzania huyo awe ni raia wa nchi nyingine sasa hivi au la sisi tunazipokea tunachojali hapa ni Tanzanian Nationality na mapenzi ya nchi..
Halafu hapa hatuko affiliate na mtu yeyote au kundi lolote. Umoja wa vitu vyovyote unaweza kuanzishwa mahali popote na watu wowote kwa dhamira yeyote waliyonayo kwenye kundi lao. E.g a) Wanaweza watu wanaoishi nchi fulani kama UK wakaamua kuanzisha umoja wa bloggers wa Kitanzania waishio UK etc etc b) Watu wenye umri fulani labda (12-18) wakaamua kuanzisha umoja wa bloggers wa kikitanzania wenye umri huo. c) Group fulani (wanawake) bloggers wa kitanzania wanaweza wakaa pamoja na kuamua kuunda umoja wao. d) Watanzania waishio Tanzania wanaoblog wanaweza wakakaa na kuamua kuunda umoja wao. Yaani hapa nina maana kuwa kila umoja unavyoanzishwa una madhumuni na malengo yake. Na hayo malengo yanaweza yakawa tofauti kutoka umoja wa jumuiya moja na nyingine.
Sisi hatupo katika umoja wowote na wala hatujapata mwaliko wa umoja wowote. Hivyo kujibu maswali yako sitaweza kwa vile hatupo kwenye umoja wowote wa bloggers wa kitanzania wowote ule.
MWISHO WA KUNUKUU…
Kaka nashukuru kwa kuliona hilo. Nashukuru kwa jitihada za kuelimisha na kuweka bayana.
JibuFutaNinalowaza zaidi ni kuwa KWANINI MTOA TUZO HAJULIKANI NI NANI NA ANAKAA WAPI?
Kwanini wanaotoa maoni wawe Anonys pekee? (nahisi ni yeye mwenyewe anayekuja na maoni ya sifa)
Kwanini TUZO ZITEULIWE NA WATU WASIOJULIKANA? Katika majibu yake kwangu amesema "Na unavyosema sijui tuwaandikie watu watueleze blog zao zinahusu nini. Kwa taaarifa yako kuna watu wengi wanablog lakini hawajui hata blog zao zinaelekea wapi. Kuna maswali tumetuna na kuna wengi wamesharudisha lakini nakwambia ni kama 50% ya waliorudisha mpaka sasa hivi hawajui blog zao zinahusu nini au wasomaji wa blog zao ni nani."
HAPA NDIPO NINAPOWAZA kuwa KAMA MTU HAJUI ANAANDIKA KUHUSU NINI, NA ANAMUANDIKIA NANI, NI KWANINI AWE NA TUZO?
Kwa majibu yake waweza kuona kuwa AMESHALENGA MAHALA.
Tuwenii macho na vitu kama hivi, sidhani kuwa tulianzisha blog zetu ili tupate hizo zawadi.
JibuFutaOk, labda ni tuzo, na kama ni tuzo, hawo waandaji wapo wapi, na ni akina nani, na masharti au vigezoo vya hizoo tuzo ni vipi
Tuelewe kuwa nyanja hii ya mawasiliano imegubikwa na sintofahamu nyingi, wapo ambao kila kukicha wanabuni mbinu za kupata kwa kutumia migongo ya watu.
Hatuna uhakika na hili, kama lipo na watu wana nia njema, waweke wazi, sio mbaya mkawajali wanablog...cha msingi mjue kuwa wengi wa wanablog ni wapiganaji kwa ajili ya manufaa ya jamii, sio kwa ajili ya biashara au zawadi, kama zipo tutashukuru, sio mbaya.