Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Aprili 26, 2011

SIKU YA KWANZA ....M a J i/WATER

Maji huwa ni kiini cha uhai duniani na pia kiini cha utamaduni wa kibinadamu. Hakuna mtu anayeweza kuishi bila maji kwa sababu asilimia 50 - 65 za mwili wa mwandamu huwa ni maji. Hata miili ya mimea na wanyama kwa kiasi kikubwa ni maji.Kikemia ni kampaundi ya elementi za oksijeni na hidrojeni zikiunganisha atomi mbili za hidrojeni na atomi moja ya oksijeni kuwa molekuli ya H2O au maji.

Jina la maji hutumika hasa kwa hali ya kiowevu ya H2O. Hali mango huitwa barafu na hali ya gesi huitwa mvuke. Yenyewe haina rangi wala ladha au herufu.

Maji huwa ni kiowevu kinachopatikana kwa wingi duniani. Yajaza mito, maziwa na bahari. Theluthi mbili za uso wa dunia hufunikwa na maji.

Upatikanaji wa maji ulikuwa jambo muhimu katika historia ya utamaduni wa kibinadamu tangu mwanzo. Njia za maji zilikuwa kati ya njia za kwanza za mawasiliano kwa watu; mabonde ya mito inakata milima na kurahisisha usafiri.

Hata kwa watu kwenye ngazi ya wavindaji kando la mto au la ziwa lilikuwa mahali muhimu walipopata wanyama waliokuja kunywa. Watu wenyewe walipanga makazi yao penye maji. Binadamu walipoanza kulima maji kwa mashamba yalikuwa muhimu zaidi hasa katika maeneo pasipo na mvua wa mara kwa mara.

Wataalamu wengi huona ya kwamba ugawaji wa maji ulikuwa chanzo cha hisabati, sayansi na serikali. Madola makubwa ya kwanza yametambuliwa katika mabonde ya mito kwenye nchi yabisi kama mto Naili, Frati na Hidekeli au Indus. Haja ya kugawa maji, kujenga mifereji, kuitunza na kusimamia shughuli hizi zilileta haja ya kujenga uwezo wa kuhesabu, kutunza kumbukumbu, kuanzisha mwandiko na kuwa na vyombo vya utawala.

**************************************************************

SIKU YA KWANZA NI SIMULIZI INAYOGUSA MAISHA HALISI YA BINADAMU, NI KIPENGELE KITAKACHOKUWA KINAKUIJIA KILA JUMANNE.

**************************************************************

Issue Hii ni Kwa Msaada wa WiKiPeDia

Maoni 2 :

  1. Kweli nakubali MAji muhimu aisee yani .....umegusa gololi kabisa kwenye belingi Mkuu!

    JibuFuta
  2. Na ndio hapo ninapojikuta kuwa nina KIU ya kunywa maji wakati kumbe pia sijaoga siku 3 ajili ya baridi.

    JibuFuta