Katika Blog ya Simon-Kitururu Nimekuta jambo hili:
Kuna maisha ya NENO yaishiyo kwenye MANENO!
Nikwambie Jambo rafiki;
Neno ni sehemu fupi ya lugha yenye maana. Ni sauti inayotamkwa au kuandikwa pamoja na kutaja jambo fulani.
Neno linaweza kuwa fupi lenye mofimu (yaani sauti inayowakilisha maana fulani) moja tu au kuwa ndefu lenye mofimu mbalimbali.
Wataalamu wanaona neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa maandishi jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafasi nyuma na mbele.
Katika mazungumzo wakati mwingine si rahisi kutofautisha maneno kama ni maneno marefu au maneno mawili. Kwa mfano kuna maneno yaliyobuniwa juzi tu kwa kutaja mambo ya teknolojia na sayansi ambayo yanaunganisha maneno mawili kuwa moja:
- garimoshi (gari + moshi) kama kifupi cha "gari la moshi" iliyokuwa kawaida zamanimawasilianoanga (mawasiliano + anga - "telecommunication")