Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Aprili 14, 2011

MGENI

Hili ni kanisa la Waadventista Wasabato Kinondoni Dar es SalaaM

Watu wamekuwa wakitatizwa na matatizo ya kimaisha kama vile (kijamii i.e mapenzi, kikazi, kifamilia, kiuchumi na kisiasa). Almost kila mmoja wetu ameshapitia dhahma moja au nyingi kutokana na mambo ya mapenzi. Kwa wengine imepelekea kukata tamaa ya kuishi na wengine kufikia hata kutaka kujiua na wengine kujiua kabisa. Kuutambua mwili na baiologia yake (hususan viungo, milango ya fahamu na hormones husika) kunaweza kusaidia katika kukabiliana na matatizo yanayohusiana na maisha kwa ujumla (matatizo ya matatizo binafsi kama vile ugonjwa, kijamii, kisiasa na kiuchumi). Ingawa kila mwanadamu responded differently kwenye matatizo, nini kinasababisha kupata hisia husika i.e kulia, kucheka, kuumia tu moyoni, kupata msongo wa mawazo, kujiua, kudharau na kuendelea na maisha etc. Je, kwa ujumla, ni nini kinatokea mwilini pale unapokumbana na moja au zaidi ya matatizo yaliyotajwa hapo juu. Tusaidiane kujitambua ili kuweza kuchagua njia muafaka ya kutatua matatizo/ au jinsi ya kubeba hisia zhusika pale matatizo yanapojitokeza.


Hii ni kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kinondoni Dar es SalaaM

Napenda kuwakaribisha Watanzania na Waafrika wote mlioko CANADA na USA na maeneo mengine yote DUNIANI. Tarehe 16th, April kwenye Sabato ya “WAGENI " itakayo fanyikia Tanzania jijini Dar es salaam katika kanisa la Waadventista Wasabato Kinondoni. Siku hiyo, kutakuwa na kwaya mbali mbali pamoja na vikundi vya uimbaji, kuna wanaoimba Acappella, kuna wanaotumia magitaa na namna nyingi nyingine za kumtukuza MUNGU. Kila mmoja anakaribishwa maana ni siku maalum ya MGENI. Haichagui dhehebu, rangi, taifa, kabila wala jinsia n.k.

Twaomba kwa mola muweza juu ya kila kitu atupe uwezo na moyo wa kusimama kwa ajili ya haki, atupe yaliyo yenye rehma tuzijuazo na tusozijua, atusamehe makosa yetu tuyajuayo na tusiyoyajua, na atujaaliye mema duniani na hata MBINGUNI, na awafungulie kila aliye changia katika kulifanisha wazo hili la mtandao kama huu iwe rahisisho kwao la kuipata Neema pamoja na sote wana ndugu kwa neno la MWENYEZI MUNGU.

Ngoja Kwanza Kinondoni SDA Choir watujulishe jambo kwa kutukumbisha kuwa

"YESU ALISONONEKA".


KARIBUNI SANA


Maoni 1 :

  1. Asante kaka Mcharia kwa maneno mazuri yenye Unyenyekevu,Upendo,Kujenga,Kujali,Ukarimu,Umoja na Usharika mwema,Mungu akubariki kwa kutenda kazi yake na kukumbusha wengine!
    Asante tutakaribia ndugu yangu!
    Ubarikiwe kaka Mcharia!.

    JibuFuta