Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumapili, Aprili 17, 2011

SEMA NA JAMII

Ktk pekua pekua yangu ya kutafuta ni nini nikiongeze kichwani kwa upande wa MAHUSIANO ili kipindi ninachoendesha kila jumanne kiitwacho SEMA NA JAMII ambacho huruka kuanzia saa 2:30-4:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki Morning Star Radio 105.3 fm.

Nilipopita hapa http://richmanyota.blogspot.com nilikutana na mada inayosema AINA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA WANAUME.

Mwandishi wa Blog hiyo alieleza kwa kuorodhesha baadhi ya aina za wanawake wanaopendwa na wanaume; mimi nitazitaja kwa ufupi tu japo kila moja ilifafanuliwa vizuri.

 1. WENYE MSIMAMO
 2. WAPENDA USAWA
 3. WANAOJUA MAPENZI
 4. MARAFIKI
 5. WA WAZI
 6. WANAOJITEGEMEA
 7. WASIO NA PRESHA
 8. MARIDADI
 9. WANAORIDHIKA
 10. WA MMOJA
Baada ya kuwa nimesoma na kutafakari ikaonekana japo sina hakika kuwa hii orodha ni kwa mujibu wa watafiti. Nilijiuliza maswali mengi lakini mwishowe nikaona wacha nimuulize msikilizaji yeye anafahamu nini kuhusu hili jambo, kipindi kiliruka tarehe 5th, April, 2011.
Ni mada ambayo iliwagusa watu wengi mno kwa mujibu wa simu zilizopigwa na msg nilizopokea. Hata hivyo mtizamo nilioupata ni tofauti na nilivyoelewa mara baada ya kuwa nimesoma habari hiyo katika Blog ya kaka
RICHARD MANYOTA iitwayo:
http://richmanyota.blogspot.com/2011/04/aina-10-ya-wanawake-wanaopendwa-na.html

Kiukweli tulijadiliana kwa kina na huku msikilizaji akiwa ndio muongeaji mkuu kwa jinsi ambavyo niliamua kukiendesha kipindi. Na sasa haya ndio matokeo ya kile kilichotajwa, badala ya aina 10 za wanawake wanaopendwa idadi ilikuwa ya kushangaza…nayo ni hapa kama ilivyosemwa:

1. Awe Mkarimu

2. Awe Mkweli

3. Awe Mtiifu

4. Awe Mchapa kazi

5. Awe Mwaminifu

6. Awe Mnyenyekevu

7. Asiye na makundi

8. Awe Msiri

9. Awe Mvumilivu

10. Awe na Umbo zuri

11. Awe Upendo

12. Awe Huruma

13. Awe ni mtu wa Kujitoa

14. Awe Huduma

15. Awe ni mtu wa Maombi

16. Awe Mpole

17. Asiwe na roho mbaya

18. Awe Mcheshi

19. Awe Rangi halisi/alisi (sio mkorogo)

20. Asiye na nywele bandia

21. Awe ni wa kuvaa Mavazi ya heshima

22. Asiwe Muoga

23. Wanaume wengi tunataka kuishi na wanawake kwa udikteta,tunataka wao wawajibike kwetu bila ya wanaume nao kuwajibika kwao. Dhana ya mwanaume ni kichwa cha nyumba inatutia kiburi,lakini kichwa bila kiwiliwili kitasimama? Ukiwa mwanaume mwema utapewa mke mwenye sifa njema.YONA JOHN.CHALINZE

24. Usafi, unyekevu uvumilivu, ukalimu, usiri, upole, heshima, upendo, hayo yanamata sana ila kuna wengine wanachukulia utii kama ni uoga la hasha! Mwanamke ukimchukulia mme kama rafiki hayo yanawezekana hautaona kama utumwani ni mourine wa machimbo

25. Sifa za mwanamke apendwaye.Awe mtii,awe mkweli,awe na sauti ya kawaida na awe tayari kuomba msa maha kama kosa liko wazi.Hata hivyo sisi waume tukitaka kupendwa inatupasa sisi kupenda kwanza,kwani upendo huzaa UPENDO.Mathayo 7. 12 Fredrick R, Tungilo.From Mbagara.

26. Pia mwanamke mcheshi anayejua kuongea vizuri na watu hana mapozi mwenye comfidence akizungumza na watu pia ni kivutio kizuri kwa mwanaume sio mwanamke hata kuongea naye inakuwa tabu kwani hana hobie ya kuongea gidion toka kitunda

27. Pia mwanamke awe ni mwenye kujiheshimu kwa mavazi ya kusitiri mwili, mwenendo uwe safi, na asiwe wa kupokea ushauri mbaya kwa rafiki zake, awe na hofu ya "MUNGU" Christina sinza.

28. NAITWA MASAI MJANJA KUTUWA MARO NIKIWA RUGOBA SALENI MCHANGO WANGU WOTE WAWE MAPENZI YAKWELY

29. Mwanamke Muwazi,awe huru kutenda au kunena isiwetu kwa sababu mim ni mumewake'iwe ni tabia yake,isiwe utii na unyenyekevu wa woga'ADONI-KIMARA

30. MWANAMKE MSAFI YEYE MWENYEWE NA MAZINGIRA KWA UJUMLA NI SIFA YA MUHIMU UCHAFU UMEVUNJA NDOA NYINGI.Yona John.chalinze

31. MWANAMKE AWE MSAADA KWA MASIKINI ,WAJANE NA YATIMA. BY MRS MAINGU JANDWA

32. MWANAMKE ANAEFAA NI HUYU ,ANAE MWOGOPA MUNGU KWANZA YAAN ANAMJUA MUNGU VIZUR NAKUMTII,MENGNE ITAKUWA LAHSI KWA MUME WAKE KUMTII MI MAMA MUS SNZA

33. WANAMKE ANAE WAHESHIMU NDUGU WA PANDE ZOTE MBILI NI SAMAKI GODFREY ISOMBA SAMAKI WA IKIZU SHOP VINGUNGUTI

34. MTANGAZAJI SASA HIVI WATU WAMEFANYA NDOA KAMA FASHENITU UPENDO WA KWELI NI KuJUA MWENZAKO ANA MAWAZO AU MATATIZO GANI UKAWA KARIBU NAE NA UTANDAWAZI UMEONDOA HESHIMA YA NDOA KWA WAKINA MAMA HASA WAKIWA NA KIPATO KULIKO WANAUME NI SABA GODFREY MASAWA ISOMBA WA NYAMANG'UTA BUSENGETE

35. Mama aliyeanza kuchangia.Kanigusa sana.Hata mimi naona kwanza mwanamke awe mkweli kila anapofanya jambo kinyume.Maon yako nihayo.Patrick sinza mapambano.

36. MADA YA LEO INANICHOMA TUPO PAMOJA NAITWA SALEHE ILUNDE WA KIWALANI DAR

37. MADA NI NZURI SANA ILA ILITAKIWA WEWE KUELEZEA HIYO ORODHA NDIPO NASI TUONGEZEE TOKEA HAPO UKISEMA AINA INA MAANA TOFAUTI NA DHANI KICHWA CHA MADA YENYEWE HAIEL

38. Kwakweli upendo hauchagui unaweza ukamuona mwanamke mbaya kaolewa na mwanaume mzuri, tabia ndiyo inadumisha upendo hata akikupenda kwa umbo ipo cku umbo litachuja, kwahiyo mtaachana? ila tabia haichuji, mwanaume ukimpenda wanamke na mwanamke akimuheshimu mumewe lazima mtapendana tu, au sio kaka? MIMI LILIAN MASARE.

39. Kaka yusufu unajuwa kwamba ckila mke au mme mwema hutoka kwa Mungu na sio wote wanaojuwa maandiko kinachotakiwa ni kujishusha, kuaniniana, napia hata katija mazungumzo kuwa mwenye uamuzi mmoja sio upohuku mara upohuku MIMI LILIAN MASARE

Baada ya kuwa nimepata orodha hii, kumbuka hii ilikuwa ni kwa upande wa wanawake yaani aina za wanawake wanaopendwa na waunaume. Nikaona hapa bado haitoshi nikaamua kufanya mundelezo ambapo tarehe 12nd, Aprili kupitia kipindi hicho hicho cha SEMA NA JAMII tukaanza kujadiliana kuhusu AINA YA WANAUME WANAOPENDWA NA WANAWAKE ana mjadala huo ulizaa majibu ya fuatayo:

1. Mavazi/mwanamme apendeze

2. Aoge maji anayopelekewa na mke wake

3. Asichelewe kurudi nyumbani bila taarifa

4. Awe Mkweli

5. Amtumikie Mungu

6. Awe anasaidia kazi

7. Asiwe mtu wa kulala wakati mwanamke anaosha vyombo (kusaidiana)

8. Awe mwanaminifu (asiwe msaliti)

9. Mcha Mungu

10. Asiwe muongo

11. Awe msafi

12. Awe Mkarimu

13. Awe mcheshi

14. Awe mpole

15. Nidhamu

16. Asifanye kazi za ndani

17. Asipende mpira (ushabiki hasa)

18. Mwanaume muongo hupendwa sana na mwanamke

19. Asiye na majigambo

20. Awe mtanashati

21. Asiye anayetumikisha

22. Mwenye hela

23. Awe na Upendo

24. Mwenye hekima na busara

25. Muwazi

26. Mkweli

27. Mtetezi na mlinzi

28. Anayebembeleza

29. Asiwe mbinafsi

30. Asiye na dharau

31. Anayedekeza

32. Mcha Mungu

33. Anayeshirikisha familia katika mambo yote

34. Awe na hofu ya Mungu

35. Mchapa kazi

36. Anayeweza kusimamia familia

37. Awe mwema

38. Awe rafiki

39. Awe ni ambaye hawapendi wazazi ama kukaa na ndugu

40. Awe ni anayewahi kurudi nyumbani

41. Awe ni anayetoa ruhusa ya kwenda kwa kila harusi/sherehe

42. Ajue kumuandaa mke kwa mambo ya kitandani naitwa madebe wanawake wanapenda umridhishe chakula cha usiku usimbake muandae nae a lizike

43. Awe ni mtu wa kushukuru

44. Asimia kubwa kwa sasa wanawake wanapenda wanaume wenyepesa.Wasiseme maumbie yoyote.Mi najua mwanume mwenyepesa atapendwa.Patrick sinya mapambano

45. Habari kaka Yusuph, napenda kuwa himiza Kina mama, waondio wajitokeze iri sisi wanaume tujue wao wanapenda wanaume waweje. Jakobo Michael –

46. Hbr za leo mtangazaj! Mimi kwa uzoef wangu, nimeshuhudia wanawake weng wakipenda wanaume kwa kutazama maumbile na tabia ndo inafuata. Wanawake wanapenda mwanaume mrefu, mwenye kifua, mweusi kidogo, anayejua kupendeza, anayejua kuimba na kadhalika. Sasa weng wanapenda maumbile alaf tabia ndio kinafuata. Ahsante!

47. kaka yusufu kweli baadhi yetu sisi hawapendi waume zao kuelewana na wazazi na ndugu sasa mtu kama huyo tumfanyaje na anasema wazi

48. Kama mhagama anamke,basi anatabu.Mimi ninajua kuwa ndoa yenye furaha ya kweli,kwavyovyote wanamjua MUNGU.

49. KWANZA WOTE MKIWA WACHA MUNGU LAZIMA MTAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU MAANA NDOA ITAKUWA TAKATIFU,KAMA KTK KUTA2WA MIGOGORO MUNGU AWE KAMA HAKIM WENU LILIAN MASARE

50. migogo yote huletwa na kufungiwa nira na wasio amini mimi kama nikiwa mpenda starehe nikampata anaependa starehe kama mimi migogoro itatoka wapi?LILIAN MASARE

51. mimi ninaitwa mama lisa kweli hayo aliechangia huyu dada mimi pia ninamsapoti kwa asilimia mia na hayo ya kudhalauliwa mimi ndie muhanga wa kudhalauwa hapo ninapoandika ujumbe huu ninatoa machozi ya uchungu kwa jinsi nilivyo dhalauliwa sana pia sina lungu ila mungu anajuwa niko arusha asante

52. Mwanaume ambaye hana hofu ya Mungu, basi upendo wa dhati kwake haupo, pia hawezi kuhurumia familia yake na walio wahitaji, mimi nasisitiza kwamba, ukiwa na hofu ya Mungu, na kuzishika sheria zake, nakujua Neno la Mungu linasema nini juu yetu wanadamu, ukiwa umcha Mungu, basi sifa zote utakuwa nazo, maana hata mfuasi wa Yesu huwa wanatambulika kwa matendo, kikubwa Mungu kwanza, mengine yatafuata kwa kuongozwa na Roho wa Mungu. Christina sinza.

53. MWANAUME ANATAKIWA ASIWE MUONGO, AWE MSAFI, AWEZE KUKONTROL FAMILIA YAKE, ASIWE MCHOYO, ASIPENDE SIFA NI MSIKILIZAJI KUTOKA TEGETA

54. Mwanaume anayependwa Muazi,alie mkweli,mwenye kujiamini inapotokea shida,mcha mungu,asiyetumia pombe na madawa ya kulevya na sigara

55. Mwanaume kujiamin mi napenda mwanaume anayejiamini kwa maana kujiamin ni mambo yote.

56. Napenda mwanaume mwenye hofu ya mungu.awe sio mtu wa vijiweni awe mtu wakupenda maendeleo awe smati anayejipenda.awe anayependa ushauri.asiwe anayependa wanawake wengine.awe mrefu kiasi awe mnene kiasi awe na rangi ya maji ya kunde.

57. Ninapenda mwanaume anaempenda Mungu, anaenipenda kutoka ndani ya moyo, mwenye hekima na busara, mwenye msimamo, awemshauri mzuri kwangu, anaeniheshimu na kunijali, anaenithamini na kunisikiliza, asiwe muongo, asiependa vijiweni. mi Jesca Mandala wa kinondoni.

58. Sipendi tabia ya wanaume kukojoa bararani ovyo, usafi ni muhimu wapendwa. mama nyakoro

59. wanapenda wanaume waminif wasaf,wakarim,wachesh,wapole,wenye nidham wenye kumcha MUNGU.ANTON mabibo

60. Wanaume anaosema baba risasi wenye tabia hizo ni wale wanaojaribu ndoa ikishindikana anajaribu kutafuta mbinu ya kutoka.

61. Wanaume wanaopendwa ni wale wasafi wa mwili, watanashati, wacheshi,wakarimu, wenye huruma, wenye mapenzi ya dhati , warefu na wembamba wa wastani. Robert john wa sinza dsm

62. YUSUPH MADA HII NI NZURI SANA MM IMENIFURAHISHA SANA ILA NIWAOMBE MAMA ZETU WAITUMIE ILI SISI VIJANA TUJIFUNZE KUTOKA KWAO NI MM YUSTO KISOMA NIKO MAGOMENI

UmEoNaE...,

NA WEWE UNANYONGEZA?

...Upi niMtizamo wako.

Maoni 1 :

 1. Mie baada ya kusoma listi naanza kuhisimwanamke na mwanaume wenye sifa zote hizo labda bado hawajazaliwa! Kwa hiyo -ngojea niwaze zaidi!:-(

  JibuFuta