Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Aprili 02, 2011

MAJIBU YAFANYAYO KAZI...SIKU YA KWANZA.


Uboreshaji wa njia za mawasiliano hususani simu na mtandao ni hatua nzuri katika kujiletea maendeleo hasa kama zitatumiwa vizuri na kwenye mambo yanayohusu maendeleo.


Kiukweli kabisa BINADAMU huwa tunatofautiana sana katika utendaji wetu. Mafanikio yetu katika utendaji hutegemea sana uzoefu katika jambo hilo tunalolitenda.

Napenda kutoa shukrani zangu nyingi kwako, kwa kazi nzuri uliyoifanya. P ia natoa shukrani kwa namna ya pekee kwa wale wote ambao kwa maombi (sala) zao uliweza kuifanya kwa kuikamilisha kazi hiyo.

Siku tutakapokuwa tumezungumzia maana, namna, mahitaji na hatari zinazotusonga katika kudumisha urafiki wa kweli, tutaendelea na hasa katika kuangalia matokeo ya mahusiano ya kirafiki na kwa namna ya pekee mwelekeo rasmi unaowezakujitokeza mara nyingi kama tunda la urafiki na mahusiano. Si kosa, tena ni sehemu ya asili ya binadamu kuwa na mvuto huo hasa iwapo mvuto huo utatokana na uhuru na utashi wa kila mhusika.

Mlangoni Pa Moyo Amesimama Mgeni...mfungulie!!!

Ni simulizi ya kweli, iliyotokea halisi. Tangu mwanzo hata sasa tunapoendelea. SIKU YA KWANZA mara baada ya kuanza jambo, hebu kumbuka siku ya kwanza wewe kupanda ndege. Au hivi, ile siku ya kwanza uliyokutana na ambaye kwa sasa!!, sasa hivi namaanisha ndie mama mkwe wako wakati ule ulipoenda kutoa posa.

Mimi siku ya kwanza kula wali hata siikumbuki! Lakini nakumbuka siku ya kwanza kupanda gari!!... ni kisa cha kuchekesha sana kwa namna flani hivi ingawa ndani yake kuna fundisho. Hivyo ndivyo binadamu anavyokabiliana na mazingira.

********************************************************
SIKU YA KWANZA NI SIMULIZI INAYOGUSA MAISHA HALISI YA BINADAMU, HEBU ANGALIA JAMBO HILI.

********************************************************
Maisha yanaendelea kuwa na maana kutokana na mapitio, changamoto tunazokutana nazo na jinsi tunavyokabiliana nazo. Nitakupatia mfano mmoja, jinsi kipimo cha upendo kilivyo baina ya mwanamke na mwanamme. Angalia mapitio na changamoto walizokutana nazo vijana, kila mmoja kwa muda wake na mazingira aliyokuwemo. Kwa kuwa bado tupo pamoja tunaamini kwamba
"SINNERS SAVED BY GRACE
"...!!!Hata hivyo bado kuna mambo ya kuzingatia katika kuamua kujenga mahusiano rasmi ambayo kwa kweli huwa ni mwanzo wa safari mpya kabisa ya kimaisha yenye malengo na mwisho tafauti na yale tuliyokuwa nayo katika mahusiano ya awali. Kwa sasa mwelekeo wetu unaonesha We Are GOING HOME.


KUBALI TATIZO LAKO ULITATUE.

Maoni 2 :

 1. Bwana Mtayarishaji,

  Siku ya kwanza ni siku ambayo kwa ukweli imekuwa na changamoto kubwa. Hutufanya tuwe na maisha ya kihistoria, hasa baada ya kufikiria tulivyohisi katika siku ile ya kwanza. Hivi fikiria siku ya kwanza kukanyaga ardhi ya Mbinguni; tutajisikiaje? Tena hasa baada ya kukubali ukweli kwamba tutaishi kwa furaha hiyohiyo milele! Siku ya kwanza!

  JibuFuta
 2. SIKU YA KWANZA
  Ni neno tu japo linamaana na uzito wake kulingana na mazingira halikadhalika nyakati.
  Wewe siku ya kwanza kuingia shule unaikumbuka?
  Je siku ya kwanza kutongoza!!

  Huwa wakati mwingine najiuliza hivi siku ya kwanza mimi kucheka ilikuwaje!! sijapata jibu bado na hata nilipomuuliza mama hakunipa jibu la kuridhisha kulingana na mtizamo niliokuwa nao.

  Bado na itazidi kuwa bado siku ya kwanza kuingia mbinguni itafanana na siku ya kwanza ya mtu anayefika Marekani au ulaya kwa ujumla?

  JibuFuta