Alianza katika hilo chapisho hivi:
Sabato njema kaka mcharia. Yaani kaka Mcharia ninaposikiliza kipindi chako (ACAPPELLA) huwa napata picha nyingi sana. Mojawapo kati ya picha hizo ni kwamba kama hawa wasanii wanaoimba muziki wa dunia laiti kama wangekuwa wanaimba muziki wa injili hasa wa kisabato hebu vuta picha tungekuwa na kwaya ya aina gani.
Halafu picha nyingine ni kwamba huwa naona hii acapella (christian) ina nguvu mno ya kumshawi mtu atake kuiimba hebu angalia siku hizi katika makanisa yetu karibu kila kanisa lazima kutakuwa na kikundi cha vijana wanoimba acapella, ukizingatia mtu yeyote hakuwalazimisha wala kuwaambia waimbe, ni ile tu nguvu ya ushawishi iliyopo katika muziki huu.
Na vijana hao unakuta wana umri kati ya miaka 13-19 na kuendelea, na ukija huku katika dunia vijana wenye umri kama hou hou huwa wanajishughulisha na muziki wa dunia, wengine jinsi ya kucheza muziki huo n.k. Hivyo basi vijana kati ya umri huu kutokana na mawazo yangu ni rahisi kushawishika, na picha nyingine nyingi kama hizi. Sasa kaka Yusuph huu umoja wa acapella tuliouanzisha tumuombe mungu atuwezeshe tuutumie kwa kasi zaidi kama njia mojawapo ya uinjilisti na zaidi kuliko Lusifa anavyoutumia muziki wa dunia muziki wa dunia kama moja ya njia yake ya uinjilisti.
Mi naamini umoja wa acappella utafanya kitu katika siku hizi za usoni. Tukiachana na hilo na mimi pia ni kijana ambaye huu huu muziki wa acappella ulinishawishi kuachana na muziki wa dunia. Na pia sasa najifunza kuimba acappella katika kundi la AZANIA BROTHERS pale shule ya sekondari azania. Siku moja ukipata muda njoo pale jangwani siku ya ijumaa katika jumuiya ya ASSA utatuona tukiimba. Mungu akubariki sana na sabato njema.
Ngoja nikwambie msomaji wangu jambo hili, kwamba:MAJIBU YAFANYAYO KAZI ni kipengele kinachoongelea masuala ya kiroho zaidi.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...(Namaanisha JumaMosi)
Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe ambapo
Dr. Carlton P. Byrd
anapotwambia "Don't Box Me In".
Naaam!!
Sijaondoka.., bado nipo nikiendelea kumtizama na kumuangalia Dr. Carlton P. Byrd.
Au kwa lugha nyingine Mchungaji wetu Fesibuuku na wakati mwingine hutumia jina la Mchungaji Carlton Byrd. Mcheki katika Facebook kama nilivyoorodhesha majina yake haya.
Inapendeza,inavutia kaka Mcharia!Familiya kwanza,Ubarikiwe sana!!!!!!!
JibuFuta