Hivi leo tunapozungumzia sheria zetu au ugunduzi fulani, huwa tunaamnini kabisa kwamba, tunazungumzia mambo yasiyo na kasoro na ambayo yamefanywa baada ya matumizi makubwa ya akili.
Itizame picha iliyopo hapo chini kwa makini kabla hujaendelea kusoma hapo chini…POVERTY!!!!!. Hii ni kazi iliyofanywa na mmoja wa marafiki zangu anayeitwa CELESTINE KIMARO. Kwa ufupi ana mambo meeengi ya kuijulisha, kuikumbusha na kuelimisha Jamii Yetu. Rafiki yangu, au au nikuite “Ndugu” yangu maana pia wewe ni “Msomaji” wangu…(Mtayarishaji). Unaweza, ikiwa utamhitaji mpate na katika facebook.
KILA JAMII INA SHREIA 'KICHAA'.
Lakini, huenda hakuna ukweli wa kutosha kwenye masuala haya. Inawezekana sheria tunazozifuata hazina maana sana na hata baadhi ya ugunduzi unaoaminika sana, inawezekana ni upuuzi mtupu. Unaweza kuja kugundua upuuzi huo baadae, wakati ugunduzi mwingine bora zaidi utakapokuwa umefanywa. Nasema hivyo kwa sababu, kwenye karne ya 6, lilikuwa ni jambo la kawaida kule ulaya, kuwapongeza watu waliokuwa wanapiga chafya. Watu walikuwa wakiamini kabisa bila chembe ya wasiwasi kwamba, mtu akipiga chafya, ina maana kwmba, anamtoa ibilisi kutoka ndani ya mwili wake.
Wakati ulaya iliposhambuliwa na ndwele (maradhi ya hatari) iliyouwa sana watu. Papa wa wakati ule alitoa amri ikatungwa sheria kuhusiana na kupiga chafya. Sheria hiyo ilimtaka kila raia kusema, 'Mungu akubariki,' kila mtu mwingine anapopiga chafya. Kumbuka hapa tunazungumzia sheria, siyo kwamba, mtu anaombwa kama anataka ksema au hataki. Ni sheria na watu waliifuata bila shida. Lakini, sheria zia kimawenge haziko kwenye chafya peke yake au ulaya tu. Hadi leo kwenye jimbo la Washington kwa mfano, ni kinyume cha sheria kwa mtu kutamba kwamba, baba yake ni tajiri.
Yeye mwenyewe anaweza kutamba kwamba ni tajiri, lakini haruhusiwa kisheria kutamba kwamba, baba yake ni tajiri. Ingawa wanasema ni sheria za vitabuni tu, lakini kwa sababu hazijafutwa bado zina nguvu yake. Kule maryland, huko huko marekani, ni inyume cha sheria kwa radio kupiga muziki wa Randy Newman unaosema "short people" (watu wafupi). Hebu rudi nyuma hadi kwenye mwaka 1313. Hapa mfalme Edward II alipitisha sheria inayosema, 'Imekatazwa na kuzuiliwa kufia ndani ya bunge. Hebu fikiria kuhusu sheria kama hii!. Kwa miaka 100 hadi sasa, ni kinyume cha sheria huko kwenye mji wa Willowdale, Oregon, Marekani kwa mtu kujiapiza wakati akifanya mapenzi.
Lakini, kule Minnesota, nchini humohumo Marekani, ni kinyume cha sheria wanawake na wanaume kuanika nguo zao za ndani kwenye kamba moja. Kule urusi, sheria ilikuwa inaruhusu polisi kumpiga mtu anayekamatwa akipiga chabo. Kwa marekani, jimboni Texas, sheria inamruhsu mtu mwenye jicho moja yaani chongo, kupiga chabo. Lakini, hata ambaye umri wake umevuka 50. Kule uingereza kuna sheria ndogo au sheria ya mtaa kwenye mji wa london ambapo mwanamke mjamzito anaruhusiwa kukojoa popote hata kwenye zile kofia za bati (helmet) za polisi. Lakini nchini humohumo kwenye mji wa Vermot, mwnwmke anahitaji kwanza ruhusa ya mumewe kbla hajaweka jino bandia.
DAaaah…!! nimelikumbuka gazeti la JITAMBUE
La Jumatano February 6-12, 2008.
TAHADHARI:
…HaBaRi Hii BaDo UnArUhUsA KuIpInGa.
*******
Kwa kweli napata faraja kuona kazi nzuuri na yakuvutia hasa kwa elimu unayotoa..Kanzi sana tena sana..Mungu akubariki na usikate tamaa kwa lolote..Hongera..
JibuFuta@Chalii Yangu:
JibuFutaNashukuru sana kwa nyongeza ya ukarimu katika maneno hayo.
Pamoja Mkuu.