Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Aprili 04, 2011

…Ilikuwa ni Monday, March 10, 2008 nilipoandika habari kuhusu: SIKUKUU YA KUVUTA MARIJUANA MAREKANI.

www.deathandtaxexmag.com:

Ilikuwa saa kumi na dakika ishirini tarehe ishirini mwezi wa nne. wanafunzi wa chuo kikuu cha Brown walifurika uwanjani kwa madai eti wanasherehekea majilio ya msimu wa joto. Uwanja mzima ulifurika vimwana na maghulamu weupe wengi na weusi wachache. Kama kawaida kwota sketi zilikuwa nyingi huku baadhi ya mibabe wakiwa kifua wazi kuonyesha malaika zao. Busu zilikuwa si haba. za waume kwa waume, wake kwa wake na zingine za waume kwa wake. Kila mtu alionekana mwenye furaha iliyovuka mipaka. Vicheko havikuwa vya kawaida. Ungefika pale ndugu ungedhani wanafunzi jamani wameanza kupagawa. Wachuuzi wa vyakula walikuwa chonjo kuokota dola. Walijua hii ni siku ambayo wanafunzi hula pasipo kuweka breki.

Hali hii isiyo ya kawaida ilinipelekea kuuliza maswali mbona leo wanafunzi wa chuo kikuu wana furaha isokuwa na kifani? Wanafunzi wangu hawakuachwa nyuma pia bali waliniomba rukhsa ya kujumuika na wenzao. Waliita sikukuu ile 4:20 at 4:20 maanake tarehe ishirini Aprili, saa kumi na dakika ishirini. Kwa kawaida niliwajua Wamarekani kama watu wasokuwa na furaha; watu wanaovalia tabasamu kwa muda unapokutana nao; watu waliojawa na upweke kiasi cha kulala vitandani na mbwa wao; watu wasiojumuika na wenzao kwa urahisi labda kuwe ile waiitayo 'appointment'.


http://www.umsl.edu/~keelr/180/pot.html

Kulikuwepo harufu aina yake katika uwanja mzima. Kila mmoja alionekana kuvuta kitu fulani chenye muundo wa sigara. Moshi wa kile walichovuta ulipeperushwa na upepo mwororo hadi nilipokuwa. Hapo nikajua kuna jambo linaendelea uwanjani. Harufu hii haikuwa ya kawaida. Nilianza basi kuchanganua matukio na kuyaoanisha. Kicheko na vitendo visivyo vya kawaida uwanjani nilivioanishwa na walichokuwa wakivuta wana wa watu. Nilipokuwa mchanga niliambiwa kwamba mtu anapovuta Marijuana huwa na tabia zisizo za kawaida. Mojawepo ya ngano nilizopashwa ni za mvutaji fulani, aliyepika ugali mkubwa kisha akapika 'kijiugali' kingine kidogo eti kiwe kitoweo cha ugali ule mkubwa.

Lakini iwapo hawa wanavuta marijuana mbona basi polisi wamejaa uwanjani? Sikuamini hadi nilpopata habari kutoka kwa Wamarekani zaidi ya watano. Kwamba siku hii inasherekewa takribani katika shule zote nchini Marekani zikiwepo shule za upili pia. Siku hii haiitwi sikukuu hadi wanaoisherehekea wavute Marijuana kupindukia. Eti kusherehekea mwanzo wa joto ni kisingizio tu; swala kuu ni kusokota Marijuana.


(Image above: Marijuana money from the Bank of Ganja.
From (
http://deathby1000papercuts.blogspot.com).

Iwapo utajiuliza maswali ndugu basi hivi ndivyo Marekani inawasaidia wafanyibiashara wa Marijuana. Kumekuwepo fununu pia baadhi ya madaktari Marekani wanawashauri wateja wao kutumia Marijuana. Piga hesabu huku ukitilia maanani mamilioni ya wanafunzi wanaovuta marijuana siku hii 'tukufu'. Siku hii pekee imewazalishia walanguzi wa marijuana mabilioni ya dola. Baada ya kufanya hesabu, jiulize sheria za U.N. zasemaje kuhusu madawa ya kulevya? Juzi Marekani wamevunja sheria ya U.N. na kushambulia Iraq. Hivi jana wamevunja ya madawa za kulevya kwa kuwaruhusu walanguzi kuuza na wanafunzi kununua.

MAREKANI INAOZA KWA KASI NDUGU.

Maoni 4 :

  1. Ee bwana wewe ni mkali katika kuandika kitu na kikawa na mvuto. Vipi, tuitengenezee riwaya hii habari fupi?

    JibuFuta
  2. Duh, hii kali mkuu! Marijuana, au bangi...mwisho wa siku tutaishia kuwa na vichaa kibao...oh, tuombe hiyo dini isiwateke vijana wetu hapa nchini

    JibuFuta
  3. DUH HII HABARI IMENIFANYA NICHEKE MBAVU SINA. KAKA HIVI HIZI HABARI UNAZITOAGA WAPI?. KWELI WEWE MKALI, NASIKIA KWAMBA WATU WANAO VUTA BANGI NI WAPOLE NA WAUNGWANA SANA. PIA INASEMEKANA KWAMBA WATU WANAO VUTA BANGI WANAKUA NA AKILI NYINGI SANA. ETI NDOMANA IKAPIGWA VITA, SASA SIJUI NI KWELI.

    JibuFuta
  4. @Filipo: si vibaya kwa wazo hilo la huo mradi Neema itakuwepo?.

    @Emu 3: naam ndugu.

    @Prince: Ninavyozipata habari hizi ni kwa sababu ya kusoma zaidi machapisho mbali mbali. Suala la kuwa wavuta marijuana wanakuwa na akili sana sina hakika ila nimeshaanza kulifanyia kazi (uchunguzi)

    Jamani, ninawashukuru wote mliosema jambo katika post hii, much respect.

    JibuFuta