Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumanne, Machi 01, 2011

NDANI YA NYUMBA

Picha kwa hisani ya: www.spotistarehe.wordpress.com

Watu walikuwa wanakimbia hovyo, hakuna alieng’amua kilichokuwa kinaendelea mda huo, hata hivyo isinge baki kuwa siri maana ni jambo lililokuwa linaendelea kwa mda huo mchana kweupe wakati eneoni.

Njoo!!! Sauti ya kike ilisikika ikiita kwa nguvu na kwa ukali. Kumbe mvua kubwa ilikuwa ikinyesha hivyo kufanya pilikapilika za kukimbia kushamiri. Haikukoma ile sauti safari hii tena ilisikika ikitamka matusi kwa mfululizo.

Mtu mmoja akasikika akisema, wanawake wa uswahilini bwana!!!

Tulitembea mwendo mrefu kwa miguu, kwangu hayo yalikuwa ni maisha mapya maana sikuwahi kufanya hivyo tangu ningali mdogo, kwetu kwa maana ya nyumbani tulikuwa na uwezo na kila mtu alikuwa na usafiri (gari) lake.

Hata hivyo nilipenda jinsi nilivyoisanifu mandhari ya mji japo nimechoka, miguu inauma kwa ajili ya mwendo mrefu lakini nimepata kitu kipya ambacho hata sielewi ni nini kinanisukuma.

Nahisi kama kuna nguvu flani inanisukuma, moyoni. Kisa chenyewe kilikuwa kama ifuatavyo;

Nakumbuka tulipokuwa wadogo, maisha yetu hayakufanana na watoto wa rika sawa na tulivyokuwa sisi, kila mzazi yaani baba na mama walishangazwa na aina ya tabia tuliyokuwa nayo na hata jitihada achilia mbali majirani waliokuwa wanatuzunguka, nyumbani kwenyewe.

Pengine unaweza jiuliza ninamaanishaje katika usemi huu…! Ngoja nikwambie mambo yalivyokuwa…ila fahamu hili ni jambo linalonihusu mimi ingawa wewe nimekupa upendeleo wa kufahamu katika simulizi hii.


Picha kwa niaba ya: www.kimarothesenior.blogspot.com

Ni hivi;

Kila siku iliyokuja na kupita ilitulazimu kuwa na swali jipya la kumuuliza baba, huu ni mtindo mpya wa tabia tuliyoianza, tukiwa watoto watatu katika familia yenye watu watano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni