Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Machi 26, 2011

MAJIBU YAFANYAYO KAZI...Mawasiliano Bora.

Yusuph Mcharia akijaribu kile awezacho na kupenda.

Mawasiliano bora ni muhimu kwa mafanikio yetu katika nyanja mbalimbali.
Ikiwa hatuna mawasiliano bora, yaani kwamba; ikiwa hatuwezi kuwasiliana inavyotakiwa, itakuwa vigumu kwa watu wengine kutusaidia katika kile tunachokihitaji.
Kushindwa kuwasiliana vyema kunadumaza na mara nyingine kuua kabisa uhusiano baina yetu na wengine.

Yusuph Mcharia ndude ikiwa imekolea.

Ni vigumu sana kumsaidia mtu ambaye analaumu usiku na mchana.
Hapendi hiki, hapendi kile, hataki hiki na wala hataki kile na bado hawezi kusema anapenda au kuhitaji nini. Kwa hali hii watu wa namna hii huwa wanabaki kuwa ni wakulaumu mara dufu
.
Yusuph Mcharia akihakiki alichokuwa anaingiza.

Usisubiri itokee siku ambayo utalala halafu ukiamka asubuhi ukute yale uliyokuwa unayataka yametokea. Malengo yako lazima yakutese usiku na mchana.
Watu wote waliofanikiwa hawakufika hapo kwa bahati, walipanga malengo na wakayafanyia kazi.


MAMBO YA KUZINGATIA KUELEKEA MAFANIKIO.

Kwa kuwa maisha ni kama safari na malengo ndiyo dira, ukianza kuyafanyia kazi malengo yako utagundua unatakiwa kufanya nini ili safari yako ya maisha iwe rahisi. Lazima ufahamu mambo muhimu yatakayokusaidia kurahisisha safari yako kuelekea mafanikio.

....Kwa sababu ya upekee na unyeti wa siku, Sio vibaya tukibadilishana mawazo na kuambizana yaliyomuhimu katika maisha hasa ya kiroho.
Na huu utakuwa ni mfululizo kwa kila siku kama hii ya leo...
(NAMAANISHA JUMAMOSI)

Pamoja na kwamba weeengi wanaamini hii ni kweli, lakini kweli halisi jionee mwenyewe kuhusu

Satanic Conspiracy In The Music Industry

HALAFU UTAFAKARI.

...Wakati ukiendelea kutafakari.

JENGA PICHA AKILINI MWAKO
Jenga taswira ya kitu unachokitaka akilini mwako.
Picha unayoijenga lazima iwe kubwa.
Fikiria jinsi utakavyokuwa na mafanikio makubwa maishani katika kile ulichochagua kukifanya. Jione tayari ukiwa katika mafanikio ambayo ulikuwa ukiyatamani kwa siku nyingi
.

NAKUTAKIA SABATO NJEMA....Wakati unaendelea kutafakari.

Tabia za watu wasioweza kufanikiwa huwa ni za kukwepa kuwajibika. Kuna mtu ambaye amekuwa akisoma makala mbalimbali na amekuwa akipenda kufanikiwa kimaisha namuomba, asiwe miongoni mwa watu ambao watakuwa na tabia zifuatzo kwani haweza kufanikiwa kimaisha.


Kufikiri, kusema na kufanya yasiwezekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni