Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Machi 23, 2011

KUPENDA SANA UTAJIRI HUSABABISHA UKICHAA

Itizame picha iliyopo hapo juu kwa makini kabla hujaendelea kusoma hapo chini. Hii ni kazi iliyofanywa na mmoja wa marafiki zangu anayeitwa CELESTINE KIMARO. Kwa ufupi ana mambo mengi ya kuijulisha jamii. Unaweza mpata pia na katika facebook.


----------------------------------------------------------------------------
 • Sasa imekubalika fedha haileti furaha...,
 • Wenye kuweka mali mbele wanaumwa...,
 • Wanaoingia ndani mwao ndiyo matajiri.

---------------------------------------------------------------------------

Kwa sasa mitizamo inabadilika, tena haraka sana hasa kwenye nchi zilizoendelea. Labda kwao ni rahisi kwa sababu wana watu wengi walio matajiri ambao pamoja na utajiri wao wanaonekana kwamba wanasumbuka sana katika maisha.

Kwa huku kwetu, bado inaonekana kuwa mtu kumiliki hata nyumba tu na gari ni mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kumpa mtu huyo furaha ya kweli. Lakini, taarifa mbaya ni kwamba wale watu ambao wanaamini katika mali ili kuweza kupata furaha, hatmaye huingia kwenye kuwa vichaa.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, inawabidi watoke kwenye hali halisi na kuishi kwenye dunia yao ambayo haiwezekani. Wanajisahau wenyewe na kuweka nguvu zao kwenye vitu vya nje (mali), jambo ambalo huwaumiza.

Tulio wengi kwa sasa, tunajua kwamba fedha haziwezi kununua furaha; karibu kila mtu husema hivyo. Ni wachache wasiopenda kujiuliza maswali, ndio hawaamini hivyo.Na kwa kweli hata tafiti nyingii zinathibitisha hivyo. Lakini je, ulikuwa unajua kwamba kupenda sana mali kunaweza kuharibu akili na mwili?

Mnamo mwaka 2002, mwanasaikolojia Tim Kasser aliandika kitabu ambacho kinazungumzia kiundani kuhusu uhusiano wa kutokuwa na furaha na kupenda utajiri. Alichokigundua wakati wa tafiti zake kinaweza kukushangaza.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya kupenda maisha ya dunia na baadhi ya matatizo ya kiakili na kimwili. Kwa maelezo mengine ni kwamba, watu wanaopenda sana fedha, utajiri, na mali na kutothamini uhusiano na mambo mengineyo ya maana, wanauwezekano wa wana uwezekano wa kukutana na mambo kama, huzuni, wivu na chuki, msongo wa mawazo, wasiwasi wa kijamii, na hasira za ndani kwa ndani.

Wengine ni pamoja na, uzingativu mdogo, udhibiti mdogo wa hisia, kuona kama unadhibitiwa, kutokuwaamini wengine, tabia ya kuwafanya binadamu wengine kama vyombo vya kujinufaishia, uhusiano mfupi na wenye mvutano, kujiona kama unatengwa na jamii, kutojihusisha sana na mambo ya wema na kuwa na afya mbaya.

Ni rahisi kuona ni kwa jinsi gani kupenda mali kunavyoweza kudumisha kuliko kuponya matatizo yaliyotajwa hapo juu.

Utafiti wa Kasser unaonesha kwamba watu ambao wanaamini kwamba, fedha, muonekano, haiba na hadhi katika jamii, vitawafanya kuwa watu wenye furaha wanayakubatia mambo hayo na kugeuka 'mateja' wa tabia hizo kama vile walivyo watumiaji wa dawa za kulevya.

Kama alivyo teja yeyote, mponda raha za dunia, hugundua hatmaye kwamba furaha aliyoitegemea kwa kulewa ni ya kupita tu na ya muda mfupi na haikidhi haja. Zaidi ya hapo anagundua kwamba kutafuta furaha toka ktk vitu vya kupita na vya anasa kumemfanya asiweze kuyatatua matatizo yake ya kweli yanayomkabili.

Utafiti unaonesha mara kwa mara kwamba, unapokuwa na fedha za kutosha za kuweza kununulia mahitaji muhimu, ongezeko la mali na havileti ongezeko la furaha.

Kwa maneno mengine ni kwamba, ukiwa na mali haikuhakikishii kumaliza matatizo yote. Pia kwa kuendelea kuufukuzia utajiri ni kama kujisumbua, kwani furaha yenyewe unayoisaka unaweza usiipate.

Kwa mujibu wa Kasser, mpenda mambo ya dunia ni yule ambaye anapenda mambo ya nje (muonekano mbele za watu, heshima, uzuri, na umaarufu) kuliko mambo ya ndani mwake kama kuwa mwema, kujiheshimu na kuamini katika yeye mtu kama alivyo.

Usilinielewe vibaya-sijawa mpumbavu kiasi cha kudharau moja kwa moja sifa za nje za binadamu, kwa kuwa haiwezekani kukamilika bila hizo. Lakini mambo ya nje yanapokuwa yanapewa kipaumbele kuliko ya ndani mwa binadamu, litakuwa ni tatizo.

Nataka kila mmoja anielewe vizuri. Simlaumu mtu yeyote wala simhukumu mtu. Hakuna ubaya wowote kuhusu kutangaza bidhaa, vyombo vya habari, ulaji na muonekano mzuri mbele za watu. Kuna maisha bora zaidi nje ya maisha ya kuangalia runinga.

Hakuna ubaya tununuapo vitu tusivyovihitaji. Hata mimi nafanya hivyo mara kwa mara na hata ningependa na wewe ufanye hivyo. Tatizo linakuja pale watu wanaendana na dhana ya 'mpenda mali' kwa mujibu wa Kasser, wanapovithamini vitu mno kuliko watu; hadithi kuliko kutimiza wajibu; na uzuri kuliko afya.

Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba tabia yetu ya kula zaidi ya tunavyohitaji ina historia yake: tangu enzi za mawe pale mababu zetu walipokuwa wanakusanya matunda watokapo porini mawindoni.

Lakini yatupasa kujua kuwa tutakapolijua tatizo hili la kununua hata vitu ambavyo hatukuvipangilia tunaweza kujifunza namna ya kudhibiti tabia yetu hii. Na katika mchakato huo, hatuna budi kujifunza kwamba inawezekana kupata maana na furaha ya maisha tunayotaka kutokana na kazi hizi hizi tuzifanyazo na watu tuwapendao.


....Tukirudi katika picha hapo juu, najiuliza hivi designer pale aliwaza nini. Na labda msomaji nihakikishie hadi kufikia hapo mara baada ya kusoma haya maelezo na kuitafakari ile picha pale juu mpaka hapo una waza nini.

Maoni 1 :

 1. No life yani!

  Yani no PARENTS
  No Love
  No hope

  No food
  No shelter,...
  ...sasa kimebakia nini?:-(

  JibuFuta