Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatano, Machi 16, 2011

Dunia Isiyo na Njaa...KILIMO KWANZA!?.

Mtizamo wetu:
Niii kuwepo kwa dunia isiyokuwa na njaa na ukosefu wa lishe bora – Dunia ambayo kila mtu ana hakikisho la chakula kistahilicho na kinachofaa ili kuwa na afya bora. Mwono huu uwe ni wa dunia inayotoa na kulinda heshima ya kila binadamu wake wote. Hii ni dunia ambamo watoto wote wanaweza kukua, kusoma, na kusitawi, na kuendelea hadi kuwa watu wenye afya na watu wenye kujali maslahi ya wengine katika jamii na wenye maadili mema hasa ya kiroho.

Kumekuwepo na mafanikio: kwamba, katika kupunguza njaa na ukosefu wa lishe bora duniani, hata hivyo haijafanikiwa kuwa na ulimwengu ambao watu wote hawasumbuliwi na njaa. Tunapewa elimu na habari kwenye masuala yanayohusu njaa ya ulimwengu, kuwepo kwa chakula, na lishe bora kuwa mambo yatakayofanikisha ukweli huu. Kwa hivyo tunakita nguvu zetu kimawazo tu kwa vijana, waalimu na viongozi wao na dini katika nchi zao.

------------------------------------------------------------

Ikiwa kila mwaka watoto kote duniani watatangulizwa kwa pamoja kwa makala tofauti yanayofundisha kuhusu njaa na ukosefu wa lishe na kinachohitajika kufanywa wakati wa siku ya chakula duniani (16 Oktoba) wanaweza kukua wakielewa utegemeano wa dunia na uwepo wa MUNGU ikiwa watafundishwa masomo kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kwenye vitabu vya maarifa na hekima hasa kutoka tamaduni mbalimbali na hali, yumkini watakuwa tayari kushirikiana katika kutatua matatizo ya njaa na ukosefu wa vyakula. Kuna njia yoyote ambayo kwayo kikundi cha vijana kinaweza kufundishwa ili kujenga uraia wa kidunia lakini hasa MBINGUNI wenye dhima???.

Tunaamini:

Kuwa...majibu kwa maswali haya yote ni “NDIYO”. Kama walimu na viongozi hata na wa dini mko katika nafasi nzuri na bora kuwaeleza vijana jinsi ya kujali na kuingia katika mapambano dhidi ya njaa. Makisio, mawazo na nguvu za vijana vinawakilisha hazina muhimu ya kuendeleza jamii na mataifa yao. Ninyi waalimu na viongozi lakini pia wazazi na wananchi kwa ujumla tunaweza kusaidia katika kuleta mabadiliko kupitia utoaji wa habari, kushirikiana katika habari, kuhimiza kushiriki na kuonesha vijana kuwa wana jukumu muhimu la kutekeleza katika kupata dunia isiyo na njaa.

UNAITIZAMAJE KILIMO KWANZA...!!?

Maoni 4 :

  1. Kaka nilishawahi kuwa nawe hapo Morning Star ila sikukaa sana nikahamia media nyingine hapa Dar. Katika dunia kaka kunamatatizo mengi sana, watu wanapata shida kila siku, siku hizi dunia imekuwa uwanja wa fujo cha msingi ni kumgeukia Mungu

    JibuFuta
  2. Njaa ni hatari sana inauwa maendeleo yote!! matumaini,amani,upendo na kujiamini.

    Asante kaka kwa mada njema!
    Basi tuungane pamoja kwa kusaidiana iwe kwa mali au maarifa!.

    JibuFuta
  3. Nanukuu "Ninyi waalimu na viongozi lakini pia wazazi na wananchi kwa ujumla tunaweza kusaidia katika kuleta mabadiliko kupitia utoaji wa habari, kushirikiana katika habari, kuhimiza kushiriki na kuonesha vijana kuwa wana jukumu muhimu la kutekeleza katika kupata dunia isiyo na njaa"mwisho wa kunukuu:- Ni kweli kabisa sisi wazazi/walezi ni walalimu wa kwanza au niseme inabidi tuwa njia moja na waalimu ili wapate nguvu.

    JibuFuta