Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Januari 10, 2011

MUKESH AMBANI HOUSE



Mmoja wa matajiri wakubwa duniani, Mukesh Ambani, raia wa nchini India, aliemaliza ziara yake katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kutoa ahadi ya kuitangaza hifadhi hiyo ili iweze kupata watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali. Ambani anayedaiwa kuwa ni tajiri namba nne duniani, aliingia nchini tangu Septemba 30, mwaka jana kupitia katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na ndege nne binafsi pamoja na ujumbe wa watu 48.

Tajiri huyo mwenye kumiliki majengo makubwa ya kifari nchini India yenye huduma zote (mojawapo hili kushoto) alisema amefurahishwa na kuvutiwa na vivutio vilivyomo katika hifadhi hiyo. Aidha, tajiri huyo alisema ataisaidia Serikali ya Tanzania kutafuta wawekezaji wa kuwekeza katika hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga mahoteli makubwa ambayo yatavutia watalii wengi zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni