Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumatatu, Januari 10, 2011

DIOKSIDI KABONIA

Dioksidi kabonia (pia: Dioxidi ya kaboni) ni kampaundi ya kikemia inayounganisha atomi mbili za oksijeni na atomi moja ya kaboni katika molekuli. Fomula yake ni CO2.

Katika mazingira ya kawaida hutokea kama gesi inayoganda kwenye halijoto chini ya -78.5°C. Katika hali ya gesi haina ladha wala harufu.


Dioksidi kabonia inatokea wakati viumbehai wanapumua na kutoa pumzi; inatokea zaidi wakati wa kuchoma mada ogania yaani mada yenye kaboni ndani yake. Mimea inahitaji gesi hii kwa mchakato wa usanisinuru ilimojenga chakula chao. Inabadilisha CO2 kuwa sukari aina za glukosi.

Kiasi cha kaboni dioksidi hewani imeongezeka katika miaka 150 iliyopita kutokana na kuchoma kwa fueli kisukuku kama makaa mawe na mafuta ya petroli. Uchumi wa viwanda, uzalishaji umeme na usafiri kwa magari yenye Injini mwako ndani kumeleta kuchomwa kwa kiasi kikubwa cha fueli hizi ambazo yote zina kaboni ndani inayomwagwa sasa kwenye angahewa kwa umbo la dioksidi kabonia.




Kuongezeka kwa gesi hii hewani kunasababisha kupanda kwa halijoto duniani2infraredi yaani joto. Maana yake nishati ya mwanga unaoonekana unaingia katika angahewa ya dunia lakini joto peke yake halitoki kirahisi. Tabia hii ni muhimu kwa uhai duniani kwa sababu kaboni dioksidi hewani inazuia kupoa kwa dunia wakati wa usiku; ila tu kuongezeka kwa gesi kutokana na shughuli za kibinadamu kunasababisha pia kupanda kwa halijoto duniani na matokeo yake yasiyotakiwa. kunakuonekana kama tatizo kubwa kwa wakati ujao. Muhimu ni tabia ya CO kupitisha nuru inayoonekana kama nuru ya jua lakini kuzuia mnururisho wa

Dioksidi kabonia ina matumizi mbalimbali kwa mfano kama gesi katika vinywaji aina za soda na bia, katika kizima moto za kupambana na moto penye umeme na mengi mengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni