Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Februari 14, 2008

Baraza jipya la mawaziri

Shauku ya watanzania imetimia baada ya kusubiri kwa hamu kubwa kujua rais Jakaya Kikwete amewateua mawaziri gani katika baraza jipya na mawaziri gani wameachwa.

Baraza hilo jipya lilitajwa Jumanne adhuhuri katika Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma.

Hatua hiyo imetokana na kuvunjwa baraza la mawaziri baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa huo kufuatia kuhusishwa kwenye kashfa ya Richmond Development, kampuni iliyoshinda zabuni ya kufua umeme wa dharura.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni