Mtayarishaji

Morning Star Radio

Alhamisi, Februari 14, 2008

Kenya wajadili uwezekano wa serikali ya mseto

Aliyekuwa katibu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewaelezea wabunge wa Kenya kwa ufupi kuhusu maendeleo ya mazungumzo nchini humo yenye nia ya kutuliza mgogoro kufuatia uchaguzi wa rais.

Bw Annan aliwaeleza hayo kabla hawajahamia eneo la siri kuendeleza mazungumzo hayo.

Hakutoa taarifa zozote kwa waandishi wa habari lakini mwandishi kutoka BBC amesema kuwa huenda kukawa na mpango wa serikali ya mseto na uchaguzi mwengine kuitishwa mwakani.

Bw Annan amefutilia mbali wazo la kurudia kuhesabu kura na kuongeza kuwa nchi ya Kenya haiko tayari kwa uchaguzi mpya kwa sasa angalau baada ya muda wa mwaka mmoja kupita.

Watu wasiopungua 1000 wamefariki baada ya chama cha upinzani kutangaza kuwa kulifanyika hila katika uchaguzi huo.

Zaidi ya watu 600,000 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mapigano ya kikabila yanayoonekana kama wengine wanawaunga mkono upinzani na wengine serikali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni