Mtayarishaji

Morning Star Radio

Jumamosi, Mei 22, 2010

UTARATIBU NA CODE NAMBA YA HUKU NA KULE 105.3 fm

CHANZO CHA KUFELI

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUHUSU MATOKEO YANGU YA KIDATO CHA NNE 2008

(Nimeiandika 8th, February 2009)
Kumbukumbu ya matokeo yalivyotoka na kunihusu mimi mdogo wako.

Hayo yote yalitokana na msichana mmoja ambaye niliwahi mpenda na kujikuta na zama katika kufeli mtihani na maisha yangu kupinda. Kisa hiki kina husu yale yote yaliyonikuta shuleni na hatimaye kushindwa kutimiza ahadi yangu, ilikuwa hivi:

Nilikuwa nasoma shule moja iliyopo Arusha, kwa ujumla afya yangu haikuwa njema kwa kipindi chote cha masomo yangu. Niliugua sana muda wote wa maisha ya pale shuleni. Ndipo siku moja nikaaamua kwenda nyumbani kutibiwa.

Nilitumia mda mrefu kutibiwa baada ya hosipitali kushindwa kunitibu ndipo nikaacha shule ili niwe nyumbani kwa ajili ya matibabu, nilitibiwa kwa muda wa miezi sita hatimaye nikapata nafuu ya kuweza kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha pili na nilifaulu mtihani wangu wa kidato hicho.

Baada ya hapo, ndipo nilipokutana na msichana mmoja aliyenipenda yeye mwenyewe nami nikajikuta nampenda kulingana na jinsi tulivyokuwa tumezoeana kwa muda mrefu, ni kweli tulipendana sana tena sana, tuliheshumiana na kila mmoja alimjali mwenzake.
Hapo ilikuwa mwezi wa kumi na mbili baada ya kumaliza mtihani wa kidato cha pili.

Matokeo yalipotoka, wote tulifaulu kuendelea na kidato cha tatu. Sasa huo ndio mda matatizo yalipoanzia hasa kwa upande wangu mimi. Ugonjwa ulianza tena kwa kasi ya ajabu ambayo muda wote ulinifanya mimi kuwa mgonjwa sana

Wakati huo huyo msichana kumbe yeye alikuwa na msela mwingine ambaye ni rafiki yangu sana, kadri nilipokuwa nikimuuliza na kumwambia kwamba yeye ana mtu mwingine alikuwa anakataaa kata kata kwamba hana. Tuliendelea na uhusiano wetu kwa muda, siku moja mimi mwenyewe nikamkuta akitoka kwao na huyo jamaa.

Kumbe alikuwa akienda mara kwa mara kwao, nikaamua kuachana nae kabisa. Kuna wakati aliniomba msamaha, alinisihi sana nami niliaamua kumsamehe kutokana na jinsi nilivyokuwa nikimpenda. Lakini kadri nilivyozidi kuwa nae ndivyo nilivyokuwa na ugua sana.

Mara kifua kuuma sana, mara malaria kali ambayo haikuwa inaisha katika mwili wangu nilivumilia sana mpaka tukamaliza kidato hicho cha tatu lakini kwangu ilikuwa shida sana. Baadae alianza dharau, chuki na kuniona mimi simfai, niliachana nae hapo sasa niliugua nusura kufa!!

Nakumbuka baada ya kuachana naye siku hiyo niliugua usiku huku akinitokea mimi akiniambia kwamba kwa nini nimemwacha huku akiniambia nitakiona. Kesho yake nilienda hospitali kupimwa nikakutwa nina malaria kali sana. Daktari aliamua kunichoma sindano za malaria nikaanguka chini nakupoteza fahamu.

Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza mimi kuzimia, baada ya hapo nilipozinduka na kupata nguvu niliamua kumfuata, nilienda nikamueleza yote, yeye alijibu kwamba aliomba kwa Mungu wake anifunulie mimi na kunionesha kwamba yeye alikuwa hana huyo ninaye hisi kwamba alikuwa naye.

Kwanza alicheka sana baada ya mimi kumwambia hayo yote yaliyonisibu, nikaamua kumuomba msamaha. Cha ajabu ni kwamba ugonjwa uliisha baada ya maongezi kwa muda na kesho yake nilikuwa mzima sana nikarudi shule.

Baada ya kurudi shule, niliendelea vyema na masomo yangu huku nikiendelea kumpenda na kumjali sana yeye kama mpenzi wangu, haukupita mda mrefu tukiwa kidato cha nne ndipo alipoamua kubadilika kabisa alinitenda alivyotaka. Baada ya kuona hayo mimi nikaamua kuachana nae tena kabisa mpaka mda wa wa kipindi cha mitihani kufika nilipatwa na tatizo la kufukuzwa shule na mwalimu wangu.

Kosa ni kufokeana na kiranja pale shuleni, huyo mwalimu hakujali hili wala lile akanifukuza shule. Kumbe huyo mwalimu alikuwa akitembea nae kwa maana ya mahusiano, ndipo alipopata nafasi ya kunifukuza shule huku akisema kwamba;…nilikuwa nakutafuta kwa mda mrefu.

Nilihangaika sana kuweza kumshauri huyo mwalimu anisamehe lakini alikataa kabisa nami niliamua kurudi nyumbani huku yeye akisema kwa marafiki zake kwamba amenikomoa sana mimi na kwamba alikuwa akinichukia sana mimi.

Baadae nilifanikiwa kurudi shule alipoona nimerudi akataka tena turudiane! mimi nikakataa, akawa ananitusi lakini sikuwahi hata kidogo kuongea nae jambo lolote lile hata kumjibu mpaka ikafikia hatua yeye alianza kujenga urafiki lakini nilikataa

Kwamba simtaki kabisa na kujiwekea msimamo wa aina hiyo mpaka sasa, lakini huyo mwalimu aliekuwa nae alisema jambo moja; tataona kama utafaulu mtihani wako wa mwisho!! Sikumjibu jambo lolote lile hata moja na kweli matokeo yalipotoka ndipo nikaamini kwamba nimefeli mtihani wangu lakini sikukata tama hata moja shule nitakwenda.

HII NDIO STORY YA MAISHA YALIYONIKUTA SHULENI, NIMESHINDWA LAKINI MUNGU HATANIACHA KAMWE.

Kaka, naomba kama kuna uwezekano wa mtu yeyote kutumia stori hii ili aweze kutoa mkanda ama kitabu sio jambo la uongo ni TRUE STORY. Sitasahau kamwe, jina la filamu iwe SELINA kuashiria matatizo yaliyonipata.

Mpaka sasa Yule msichana anataka turudiane lakini mimi nimeshaamua kuwa mwenyewe kabisa sitaki kupenda tena hata kidogo. Faida ya kupenda ndio hiyo iliyonikuta mimi na hasara ndio hiyo. Je, kama ni wewe ungefanyeje kuhusu yote hayo? Toa maoni yako kaka kwa kadri utavyoweza.

Hakika imeniuma sana na bado yeye anatuma salaam kwangu lakini mimi nilimjibu kwamba salaam zake ampe mpenzi wake ambaye alimuona anafaa kwake ndipo aliponitusi mimi mpaka na matusi ya mama yangu!! nilimuuliza mama yangu anamahusiano gani kati ya jambo hilo na yeye angepaswa anitusi mimi.

Kweli iliniuma sana mimi, lakini sitasahau kamwe mkasa huu ulionikuta mimi, ingawa mpaka sasa anatamani nimsamehe lakini mimi simtaki hata kidogo na wala jambo lolote kutoka kwake sihitaji kabisa.

Ahsante kunielewa.
Ni mimi mdogo wako,
E.D.M

Najaribu kufanya kile kitakachosaidia wazo lililoanza.
Wakati mwingine unaweza dhani kuwa hii siyo kawaida lakini ukweli unaonesha MAISHA ni sawa na mashindano ya aina yoyote yanayofanyika.
Kwa nini nasema hivi;
KILA SIKU INAHITAJI WAZO JIPYA, NAMNA JINSI UTAKAVYOJIKWAMUA KATIKA HALI UNAYOKABILIANA NAYO KATIKA MAZINGIRA ULIPO.
Kwa maana hiyo basi, naanza kuashiria mwanzo uliokwisha anza.
NINA MENGI YA KUONESHA

Fikiria Jambo Hili kwa KINA:

VIPI KAMA HALI HII INGEKUWA HIVYO SIKU ZOTE BILA KUBADILIKA
(No Jioni Wala Mchana na Hata Asubuhi)
**************
SIKU YA KWANZA

Ni simulizi ya kweli, iliyotokea halisi.
Tangu mwanzo hata sasa tunapoendelea.
SIKU YA KWANZA mara baada ya kuanza jambo.
Kumbuka siku ya kwanza wewe kupanda ndege.Au hivi, ile siku ya kwanza uliyokutana na ambaye kwa sasa!!, naamaanisha sasa hivi (kwa aliyeoa) ndie mama mkwe wako wakati ule ulipoenda kutoa posa.

**********

Mimi siku ya kwanza kula wali hata siikumbuki! Lakini nakumbuka siku ya kwanza kupanda gari!!... ni kisa cha kuchekesha sana kwa namna flani hivi ingawa ndani yake kuna fundisho. Hivyo ndivyo binadamu anavyokabiliana na mazingira.

************

Maisha yanaendelea kuwa na maana kutokana na mapitio, changamoto tunazokutana nazo na jinsi tunavyokabiliana nazo. Nitakupatia mfano mmoja, jinsi kipimo cha upendo kilivyo baina ya mwanamke na mwanamme. Angalia mapitio na changamoto walizokutana nazo vijana hawa wawili, kila mmoja kwa muda wake na mazingira aliyokuwemo.

****************

SIKU YA KWANZA NI SIMULIZI INAYOGUSA MAISHA HALISI YA BINADAMU.

Yusuph D. Mcharia.

Radio Presenter,

Story & Song wrighters, Producer and much more...!

Watoto Wanapenda Kucheza Kwenye Maji.


Jumamosi, Aprili 10, 2010

HII NI ISHARA TU, MOJA YA MAJUKUMU TUNAYOKABILIANA NAYO KILA MAWIO YANAPOFIKA NA HATA MACHWEO YANAPOJITOKEZA.

KAMA UNAWEZA JIULIZE JUU YA JUKUMU LINALOKUKABILI KILA SIKU INAYOPITA. DHAMIRA YANGU TANGU MDOGO NDIO HII NILIYOIFIKIA UKUBWANI, MTAYARISHAJI.

SASA, NAKULETEA MUHIMU YANAYOTUHUSU SOTE MAANA NATAMBUA WENGI TUNAPENDA BURUDANI.

NAYASEMA HAYA KWA SABABU NIMEMUDU KUFIKIA, ENDELEA BLOGINI...

Jumatatu, Machi 29, 2010

Hellow wote mtandanoni!!
Ni yangu imani kuwa haujambo msomaji wa blog hii.
Ni kwa siku nyingi nimekuwa kimya bila kuendeleza nia ya fikra zangu.
Namshukuru Mungu kwa jinsi anavyoendelea kuniweka katika namna ambayo kwa hakika sikuitaraji.
Kwa ufupi napenda kusema nimerejea tena.
MUZIKI WA ACAPPELLA NDIO JAMBO AMBALO LIMENICHUKULIA MDA WANGU MWINGI LENGO NIKUUFANIKISHA KWA KUUFIKISHA KATIKA NGAZI INAYOTAKIWA, WENGI WANAIITA YA KIMATAIFA.
Hellow wote mtandanoni!!

Ni yangu imani kuwa haujambo msomaji wa blog hii. Ni kwa siku nyingi nimekuwa kimya bila kuendeleza nia

Jumatano, Machi 12, 2008

UNAONAJE UKIWA HAPAAAAAAA?


MADE IN TANZANIA TU


Januari 23, 2008

JOHN Nolan, yule raia wa Ireland aliyejaribu kuighilibu Serikali ya Tanzania imruhusu aanzishe mashamba ya kamba (prawns) ambayo yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kuliambia gazeti moja la Uingereza kwamba kati ya nchi za "ajabu" alizopata kuishi ni Tanzania .

Nolan aliliambia gazeti hilo ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na akaondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea!

Alitoa mfano wa yeye mwenyewe kwamba aliingia Tanzania akiwa hana kitu, lakini 'akatengeneza pesa' akiwa katika chumba chake cha hoteli kutokana na dili walizochonga na viongozi ambao walimwamini kwa kuwa tu ni Mzungu!

Lakini Nolan si mgeni pekee aliyepata kuikejeli Tanzania . Mwaka jana gazeti la Mtanzania lilipata kumnukuu mwekezaji mmoja kutoka China , anayefanya biashara ya kuuza kamba na kambakochi Mashariki ya Mbali, akiikejeli Tanzania kwamba rushwa yake ni "poa".

Kwa mujibu wa Mchina huyo, ni katika Tanzania tu ambapo unaweza kumwita hakimu nyumbani kwako na kumpa rushwa ya Sh. 100,000 tu, na kisha kumpa maelekezo ya namna ya kutoa hukumu ya kesi ya mamilioni ya pesa inayokuhusu!

Lakini kama utashangaa na kutoziamini kauli hizo za Nolan na za Mchina huyo, utasemaje kuhusu hii ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanzisha kampuni yake ya biashara (ANBEM) yeye na mkewe, mwaka 1999, akiwa bado Ikulu?. Kwa kufanya hivyo, Mkapa akawa Rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kufanya biashara akiwa Ikulu. Historia bwana, nani hapendi kuweka historia ya ujasiriamali?

Lakini hakuishia hapo. Mwaka mmoja kabla ya kuondoka madarakani; yaani Desemba 29, 2004, Mkapa huyo huyo akashirikiana na aliyekuwa Waziri wake wa Fedha na baadaye Nishati na Madini, Daniel Yona, kusajili kampuni nyingine binafsi iitwayo Tanpower Resources Company, na akaisimamia kununua asilimia 85 ya uliokuwa mradi wa umma wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

Lakini pia hakuishia hapo. Akautumia wadhifa wake wa urais kuhakikisha kampuni yake hiyo mpya – wakurugenzi wakiwa ni pamoja na mkewe na mtoto wake, kuingia mkataba wa kuiuzia Tanesco megawati 200 za umeme katika gridi ya taifa.

Raia wema waliohoji iwapo hakuna mgongano wa maslahi kwa Rais kufanya biashara akiwa bado Ikulu; huku akinunua kampuni ya umma (Kiwira) na kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni nyingine ya umma (Tanesco), walinyamazishwa haraka kwa kuambiwa Mkapa ni "mjasiriamali", na kwamba anaonyesha "ujasiriamali" kwa vitendo akiwa Ikulu! Upo hapo?

Kama hiyo haitoshi kukuthibitishia vioja vya Tanzania , utaielezeaje hii ya Jeetu Patel kufanikiwa kughushi na kuchota Sh. bilioni 90 kutoka Benki Kuu kwa kutumia makampuni manane tofauti aliyoyasajili?

Ilikuja ya kwanza ikachota, ikaja ya pili ikachota, ikaja ya tatu ikachota, na vivyo hivyo mpaka kampuni ya nane! Na bado Watanzania tunatakiwa tuamini kwamba hakuna aliyejua kuwa hati zilizotumiwa na makampuni hayo ni za kughushi, hadi majuzi ripoti ya ukaguzi ya Ernest & Young ilipotua mezani kwa Rais Kikwete!

Lakini kama hilo halikushangazi au kukushtua, hebu tafakari na hili jingine: Watanzania masikini wanapandishiwa umeme kwa asilimia 21 kwa sababu Tanesco iko hoi kifedha. Kwa nini iko hoi? Kwa sababu vigogo serikalini wameiingiza katika mikataba mibovu ya Richmond , IPTL na Songas.

Kwa sababu ya mikataba hiyo mibovu, Tanesco inailipa IPTL Sh. bilioni 3.3 kila mwezi, Songas Sh. bilioni 5.8 na Richmond Sh. bilioni 4.7. Kwa viwango hivvyo vya malipo, unahitaji kuwa na kampuni yenye utajiri wa Microsoft ya Bill Gates, kutotetereka kifedha. Na hivyo Tanesco ilitetereka. Ili isife, ikaamua kuongeza umeme kwa asilimia 21!

Hiyo maana yake ni nini? Hiyo maana yake ni kwamba Watanzania masikini na walalahoi wa nchi hii ndiyo "wanaobebeshwa" zigo hilo la Tanesco la kufidia gharama zilizosababishwa na vigogo serikalini za mikataba ya IPTL, Richmond na Songas. Cha kushangaza zaidi, vigogo hao waliotubebesha zigo hilo kwa kuingia mikataba hiyo mibovu, bado wanadunda mpaka leo serikalini!

Na bado wameona hiyo haitoshi. Sasa Serikali inajiandaa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuziruhusu kampuni binafsi kufanya biashara ya kuuza umeme nchini. Yaani; Serikali inakuwa mstari wa mbele kulitafutia shirika lake (Tanesco) wapinzani wa kuliua kibiashara, tena inafanya hivyo ikiwa yenyewe tayari imeshalikamua hadi kuwa hoi bin taaban!

Na Tanesco ikifa na biashara hiyo ikashikwa na makampuni binafsi ya nje, (ambayo bila shaka baadhi ya vigogo nchini watakuwa na hisa), nani atayazuia yasipange bei ya pamoja ya kuuzia umeme (cartel) ili yanufaike zaidi kwa kuwakamua zaidi Watanzania? Na bado tunaambiwa kuna vita inayoendelea nchini ya kuwakomboa masikini.

Biashara ya chakula ipo mikononi mwa watu binafsi, nishati nayo sasa inawekwa mikononi mwa watu binafsi, maji nayo yataelekea huko huko …mwishowe sekta zote nyeti zinazohusu usalama wa taifa zitakuwa mikononi mwa watu binafsi hususan wageni. Tusisahau Nyerere alitabiri: "Mtabinafsisha hata Magereza."

Lakini yawezekanaje mambo yote haya yatokee nchini na umma wa Watanzania ukae kimya tu? Jibu ni kwamba ni kwa sababu Tanzania ni nchi 'poa', nchi ya amani. Watanzania ni watu wasiotaka makuu, na ndiyo maana kina Nolan wanaamini kwamba duniani hakuna nchi kama Tanzania . Hayo aliyoyaona Nolan akiwa Tanzania ni Made in Tanzania tu. Huwezi kuyakuta kwingineko duniani!

Jumatatu, Machi 10, 2008

SIKUKUU YA KUVUTA MARIJUANA MAREKANI

Ilikuwa saa kumi na dakika ishirini tarehe ishirini mwezi wa nne. wanafunzi wa chuo kikuu cha Brown walifurika uwanjani kwa madai eti wanasherehekea majilio ya msimu wa joto. Uwanja mzima ulifurika vimwana na maghulamu weupe wengi na weusi wachache. Kama kawaida kwota sketi zilikuwa nyingi huku baadhi ya mibabe wakiwa kifua wazi kuonyesha malaika zao. Busu zilikuwa si haba. za waume kwa waume, wake kwa wake na zingine za waume kwa wake. Kila mtu alionekana mwenye furaha iliyovuka mipaka. Vicheko havikuwa vya kawaida. Ungefika pale ndugu ungedhani wanafunzi jamani wameanza kupagawa. Wachuuzi wa vyakula walikuwa chonjo kuokota dola. Walijua hii ni siku ambayo wanafunzi hula pasipo kuweka breki.

Hali hii isiyo ya kawaida ilinipelekea kuuliza maswali mbona leo wanafunzi wa chuo kikuu wana furaha isokuwa na kifani? Wanafunzi wangu hawakuachwa nyuma pia bali waliniomba rukhsa ya kujumuika na wenzao. Waliita sikukuu ile 4:20 at 4:20 maanake tarehe ishirini Aprili, saa kumi na dakika ishirini. Kwa kawaida niliwajua Wamarekani kama watu wasokuwa na furaha; watu wanaovalia tabasamu kwa muda unapokutana nao; watu waliojawa na upweke kiasi cha kulala vitandani na mbwa wao; watu wasiojumuika na wenzao kwa urahisi labda kuwe ile waiitayo 'appointment'.

Kulikuwepo harufu aina yake katika uwanja mzima. Kila mmoja alionekana kuvuta kitu fulani chenye muundo wa sigara. Moshi wa kile walichovuta ulipeperushwa na upepo mwororo hadi nilipokuwa. Hapo nikajua kuna jambo linaendelea uwanjani. Harufu hii haikuwa ya kawaida. Nilianza basi kuchanganua matukio na kuyaoanisha. Kicheko na vitendo visivyo vya kawaida uwanjani nilivioanishwa na walichokuwa wakivuta wana wa watu. Nilipokuwa mchanga niliambiwa kwamba mtu anapovuta Marijuana huwa na tabia zisizo za kawaida. Mojawepo ya ngano nilizopashwa ni za mvutaji fulani, aliyepika ugali mkubwa kisha akapika 'kijiugali' kingine kidogo eti kiwe kitoweo cha ugali ule mkubwa.

Lakini iwapo hawa wanavuta marijuana mbona basi polisi wamejaa uwanjani? Sikuamini hadi nilpopata habari kutoka kwa Wamarekani zaidi ya watano. Kwamba siku hii inasherekewa takribani katika shule zote nchini Marekani zikiwepo shule za upili pia. Siku hii haiitwi sikukuu hadi wanaoisherehekea wavute Marijuana kupindukia. Eti kusherehekea mwanzo wa joto ni kisingizio tu; swala kuu ni kusokota Marijuana.

Iwapo utajiuliza maswali ndugu basi hivi ndivyo Marekani inawasaidia wafanyibiashara wa Marijuana. Kumekuwepo fununu pia baadhi ya madaktari Marekani wanawashauri wateja wao kutumia Marijuana. Piga hesabu huku ukitilia maanani mamilioni ya wanafunzi wanaovuta marijuana siku hii 'tukufu'. Siku hii pekee imewazalishia walanguzi wa marijuana mabilioni ya dola. Baada ya kufanya hesabu, jiulize sheria za U.N. zasemaje kuhusu madawa ya kulevya? Juzi Marekani wamevunja sheria ya U.N. na kushambulia Iraq. Hivi jana wamevunja ya madawa za kulevya kwa kuwaruhusu walanguzi kuuza na wanafunzi kununua.

MAREKANI INAOZA KWA KASI NDUGU.